TUPO UKINGONI MWA NYAKATI 

Siku za Mwisho No Comments

TUPO UKINGONI MWA NYAKATI 

Shalom ndugu, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe milele. Nakukaribisha tuyatafakari kwa pamoja maneno ya uzima, maadamu rehema zake ni mpya kila siku asubuhi(Maombolezo 3:22-23). Leo tutajifunza tena jinsi ule mwisho wa mambo yote ulivyokaribia sana.

Watu wengi wanajua tunaishi katika siku za mwisho.. hata watoto wadogo wanajua, hata wapagani wanajua na zaidi hata wanyama wanafahamu.

Lakini cha kuhuzunisha ni kwamba wengi hawajui ni kwa jinsi gani mwisho umekaribia sana, wengine wakisikia kuwa hii dunia itaharibiwa kwa ghadhabu ya Mungu..moja kwa moja akili zao zinawapeleka miaka mingi mbeleni. Na hii ni kwasababu wamezaliwa wakasikia kuwa kuna siku za mwisho, na tunaishi katika siku hizo… lakini shetani amewafunga wasitafute kujua huu mwisho utakuja lini, mbona tangu enzi za mababu zetu wanasikia tu kuwa hizi ni siku za mwisho, lakini hatufikii huo mwisho wenyewe.

Ndugu, mwisho umekaribia sana!. Ni kweli siku za mwisho zilianza zamani, lakini sisi hatuishi tena katika siku za mwisho, bali tunaishi katika ile siku ya mwisho enyewe, Nifuatilie utaelewa.

Ukisikia mahali popote katika biblia inasema tunaishi katika siku za mwisho,/wakati wa mwisho , Huo wakati kibiblia haujaanza leo wala jana bali ulianza rasmi takribani miaka 2000 iliyopita,..

1Yohana 2:18 “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.”

Na Mambo hayo kwa mara ya kwanza yalianza kuhubiriwa na Yohana Mbatizaji pamoja na Bwana wetu Yesu Kristo wakisema, TUBUNI kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia…Kwasababu walijua tayari wameshaingia katika majira ya siku za mwisho.

Lakini swali unaweza ukajiuliza kama ni hivyo, kwanini basi Bwana Yesu akiwa katika mlima wa Mizeituni alianza kuwaeleza tena dalili za siku za mwisho ikiwa tayari anafahamu kuwa yupo katika siku za mwisho, dalili nyingine za nini tena? Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa Bwana Yesu alikuwa hazungumzii habari za SIKU za mwisho kwani tayari wakati ule ilishajulikana kuwa zile ni siku za mwisho…Bali alikuwa anazungumzia habari ya SIKU ya mwisho jinsi itakavyokuwa…dalili zitakazoonesha kuwa ule mwisho wa yote utavyokuja ..

Ni sawa tu na kusema mwaka 2030 ni mwaka wa uchaguzi, lakini uchaguzi wenyewe utafanyika mwezi wa 10, hivyo kwa namna ya kawaida mwaka wa uchaguzi unapoanza, kunakuwa na vuguvugu la kampeni, vyama vinajiweka tayari, vinaanza kufanya kampeni za nyuma ya mgongo, dalili ndogo ndogo zitaonekana kwa tabia zao, sera zao n.k. lakini kampeni rasmi hazijafunguliwa bado.. hivyo ule wakati ukifika miezi 2 kabla ya uchaguzi wenyewe kufika, ndipo Kampeni rasmi zinafunguliwa na hapo ndipo utaona mambo yanavyofanyika kwa kasi na kwa nguvu ambazo hujawahi kuziona ni kwasababu wanajua muda waliopewa na waliobakiwa nao ni mchache sana kabla ya siku yenyewe kufika..

Na ndivyo Bwana Yesu alivyokuwa anafanya, ni kueleza dalili rasmi za kukaribia kwa “siku” ile ya mwisho na sio kukaribia kwa “siku za mwisho”…akasema mtakapoona wimbi kubwa na manabii wa uongo limejitokeza, wanafanya kampeni ili kukusanya magugu matita matita basi mjue ule mwisho ule umekaribia….hayo mambo hayakuwahi kuonekana katika wakati wowote katika historia tangu kipindi cha mitume hadi kizazi hichi cha karne ya 21, kutokea kwa wimbi kubwa la manabii wa uongo namna hii, yaani kuanzia mwaka 2005 kupanda juu mambo haya ndio yameanza kujitokeza kwa kasi….hii inaonyesha kuwa tunaishi ukiongoni kabisa mwa wakati,.. kipindi cha utimilifu wa wakati.

Alisema watakuja wengi kwa jina langu wakisema mimi ni Kristo,.yote hayo tunayaona kila kukicha.. Hizi ni dalili za kukaribia kwa siku ile kuu ya kuitisha,

Alisema kutaongeza maasi, na upendo wa wengi kupoa,..Leo hii tunaona jinsi teknolojia ya simu na mitandao jinsi ilivyoleta maovu karibu na watu kuliko kipindi chochote cha nyuma, ndani ya simu ndogo tu mtu anaweza akapata mambo yote maovu yanayoendelea ulimwenguni kote, mpaka watoto wadogo sasa hakuna jambo lolote la siri kwao. Mambo hayo yameanza kutokea kuanzia kipindi cha mwaka 2005 kupanda juu wala hata sio siku nyingi….Ulimwengu umeshajua kuwa siku zake zimebaki chache hivyo unafanya kampeni kwa nguvu kuielekea ile siku yake kuu ya kuangamizwa.

Na dalili nyingine kubwa Bwana Yesu aliyoizungumzia katika (Mathayo 24:32)ni kuchipuka kwa “mtini” ambao huo unawakilisha taifa la Israeli..Alisema jambo hilo likishaanza kuonekana basi tujue kuwa kizazi hicho hakitapita mpaka hayo yote yatakapotimia… Kwa upana wa somo hili la kuchipuka kwa Israeli tuandikie ujumbe inbox kupitia namba uzionazo chini ya makala hii.

Hivyo unaweza kuona hapo kuwa sisi ndio watu tuliofikiliwa na miisho ya zamani/mwisho wa nyakati, ndio watu ambao sio tu tunaishi katika siku za mwisho, bali pia ni watu tunaoishi katika ukingo kabisa wa siku hizo…

Umewahi kumuona mtu aliyeathirika na ugonjwa Fulani, labda HIV. Katika siku za mwanzoni ni vigumu kutambua kuwa anaumwa, lakini kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo dalili zinazidi kujitokeza na hatimaye kujulikana. Au mtu aliyepata mimba ni vivyo hivyo.

Ndivyo ilivyo katika habari ya siku za mwisho, zamani ilikuwa ni vigumu kutambua na kuamini kuwa mwisho unakuja kweli, kwasababu dalili zilikuwa bado hazijaonekana, lakini kuanzia miaka ya 90, zile dalili zikaanza kujitokeza..vita na tetesi za vita, matetemeko makubwa, njaa, tauni n.k, na kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo dalili zinajitokeza kwa kasi.

Je! Bado mambo ya ulimwengu yanakusonga?. Bado upo njia panda? Bado unazini na mke ambaye si wako au mume ambaye si wako?, bado ni mlevi, bado ni mfanyaji mustarbation, bado ni mtazamaji pornography? Bado ni mfanyaji anasa?,bado ni mtoaji mimba, bado mla rushwa? bado tu upo buzy huna muda na injili za wokovu?… Hizi ni nyakati mbaya..Kama bado upo nje ya Kristo jitahidi uingie kabla mlango haujafungwa. Anasema..

“20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”(Ufunuo 3:20-22)

Maran atha (Na uje Bwana Yesu).

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *