DHAMBI NI KAZI INALIPA!!

Dhambi No Comments

DHAMBI NI KAZI INALIPA!!

Shalom mtu wa Mungu karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu.

Ni vizuri kufahamu kuwa biblia inaposema mshahara wa dhambi ni mauti…haimaanishi adhabu ya dhambi ndio mauti!…hapana bali MSHAHARA! Zingatia hilo neno “mshahara”…adhabu maana yake unapewa mateso kulingana na kile kitu kibaya ulichokifanya…mshahara maana yake ni “unalipwa kulingana na kazi uliyoifanya”….Kwahiyo dhambi ni “kazi”..na ina mshahara haina adhabu bali mshahara…

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Kwenye vifungu hivyo tunaonyeshwa kuwa Mungu hutoa zawadi (karama), lakini dhambi inalipa mshahara.. Na mpaka ilipe mshahara ni lazima kazi fulani ilifanyika..

Watu wengi hawajua kuwa kila tendo moja la dhambi, huhesabu mshahara fulani na mwishoni mtu huyo hulipwa wote, hata kama hakujua.

Unapokwenda kuzini leo, unarudia tena na kesho, na kesho kutwa hivyo hivyo, mshahara unajilimbikiza, siku isiyo na jina utashangaa tu ghafla mshahara wako huo hapo umekufikia…

Ndio hapo mauti ya kiroho au ya kimwili au ya jambo fulani humfikia mtu.

Sasa inapofikia wakati wa mshahara wengi hujifanya haiwahusu, lakini utaupokea tu.. upende usipende…wengi humdharau Yuda kwanini alijinyonga, si kwamba alipenda lakini ulikuwa ni wakati wa mashahara, ukiona leo watu wanakutana na madhara makubwa kwasababu ya dhambi zao, sio kwamba wana bahati mbaya, bali ni wakati wa mshahara.

Ndio maana Bwana Yesu alisema katika Ufunuo 22:12..

Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, KUMLIPA KILA MTU KAMA KAZI YAKE ILIVYO.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.

Kwahiyo kitakachotokea siku ya hukumu sio watu kwenda kusomewa adhabu, bali kwenda kulipwa MISHAHARA YAO. Kila mtu kama kazi yake ilivyo…waliofanya kazi ya dhambi ndio watalipwa mauti ya milele, kadhalika waliofanya haki watalipwa uzima wa milele.

Epuka dhambi, ikimbie dhambi.

Na namna pekee ya kukimbia dhambi na kuuweza ni kumpokea YESU ipasavyo, yaani unadhamiria kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi zote na vyanzo vyake vyote kisha unatatafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina lake Yesu, hapo unapokea uwezo wa kushinda dhambi kabisa kabisa na namna zote za udunia.

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *