KUTOKUJUA DHAMBI HAKIKUFANYI USIPOKEE MSHAHARA WAKE!!

Biblia kwa kina No Comments

KUTOKUJUA DHAMBI HAKIKUFANYI USIPOKEE MSHAHARA WAKE!!

Ndugu yangu fahamu kuwa ukitenda dhambi kwa kutokujua kuwa umetenda dhambi au ukitenda dhambi kwa kujua…zote mbili zinaleta matokeo yanayofanana…na matokeo yenyewe ni mauti…kwasababu biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti. Ni sawa na mtu aliyepanda mbegu yake shambani na mwingine aliiangusha pasipo kujua mtaroni na kuendelea na shughuli zake…wote wawili mbegu zao zitamea tofauti ni kwamba mmoja atakuwa anaona na kufuatilia hatua za ukuaji, mwingine atakuwa haoni wala hafahamu kuwa alichokipanda kinaendelea kuota huko…lakini utakapofika msimu wa mavuno, mavuno yote yatakomaa kwa wakati mmoja.

Wengi wetu tunafikiri mkulima ni Yule tu aliyetoka na mbegu zake nyumbani na kwenda kuzipanda shambani..lakini ni zaidi ya hapo, mkulima ni hata Yule aliyeangusha mbegu njiani pasipo yeye kujijua na ikamea…Naye pia anastahili kupata malipo ya kazi yake..Ni majibu ya Mungu kwa kile alichokipanda…hata kama alikuwa hajui..Mungu ameshamjibu! Ndio maana ile mbegu ikamea hata kama alikuwa hajui.

Hali Kadhalika na sisi katika maisha yetu..Yapo mambo mengi tunayapanda ambayo aidha kwa kujua au kwa kutokujua..hiyo haizuii chochote ni lazima yalete majibu. Ukipanda mbegu njema utavuna mema…na ukipanda mbegu mbaya utavuna hizo hizo..

Kama wewe ni mwasherati, na unajua kabisa uasherati ni dhambi, au ni mlevi, au mtazamaji pornography, au mwizi, au mlawiti, au mfanyaji masturbation, au msagaji, au mtoaji mimba, au msengenyaji..na unafanya hayo kwa makusudi kabisa..kuwa na uhakika kabisa mbegu hizo Mwisho wa siku mbegu hizo zitakuzalia mauti..

Halikadhalika kama mwingine ni mwizi, au muasherati, au mfanyaji masturbation, au mtukanaji au mlevi, na hana habari kuwa mambo hayo ni mabaya na ni dhambi mbele za Mungu..huyo naye ni sawa na mtu aliyeiangusha mbegu yake kwenye mtaroni kando ya barabara pasipo kujijua..ambapo itamea na wakati ukifika kazi yake itaonekana na watu wote hata kama yeye hajui..Hivyo na yeye pia mbegu zake zitamzalia MAUTI!! Atakufa katika roho na katika mwili.

Mfano leo hii ukienda kubaka mwanafunzi, serikali haitaki kujua kuwa ulikuwa unaifahamu sheria au la, hiyo si kazi yao…Kazi yao ni moja tu kukuhukumu kulingana na sheria inavyosema ,utakwenda gerezani miaka 30.

Biblia inasema katika

Wagalatia 6: 7 “MSIDANGANYIKE, MUNGU HADHIHAKIWI; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele”.

Unaona? Mungu hadhikiwi biblia inasema hivyo…uwe umepanda kwa bahati mbaya au kwa makusudi, kwa kujua au kwa kutokujua…sheria ni ile ile ni lazima uvune ulichokipanda ni sheria Mungu aliyoiweka katika mambo yote hata mambo ya asili.

Biblia inaposema mshahara wa dhambi ni mauti…haimaanishi adhabu ya dhambi ndio mauti!…hapana bali MSHAHARA! Zingatia hilo neno “mshahara”…adhabu maana yake unapewa mateso kulingana na kile kitu kibaya ulichokifanya…mshahara maana yake ni “unalipwa kulingana na kazi uliyoifanya”….Kwahiyo dhambi ni “kazi”..na ina mshahara haina adhabu bali mshahara…

Ndio maana Bwana Yesu alisema katika Ufunuo 22:12..

Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, KUMLIPA KILA MTU KAMA KAZI YAKE ILIVYO.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.

Kwahiyo kitakachotokea siku ya hukumu sio watu kwenda kusomewa adhabu, bali kwenda kulipwa MISHAHARA YAO. Kila mtu kama kazi yake ilivyo…waliofanya kazi ya dhambi ndio watalipwa mauti ya milele, kadhalika waliofanya haki watalipwa uzima wa milele.

Kwahiyo ndugu, unayesoma ujumbe huu ambaye bado upo mbali na Kristo, na unafanya dhambi za makusudi au pengine sio za makusudi bali kwa kutokujua…Nataka nikuambie maisha nje ya Yesu Kristo, ni sawa na kuangusha mbegu barabarani na kwenda zako pasipo kujua kuwa zinaendelea kujiotea zenyewe huko ulikoziangusha. Na ujira wako upo! Vivyo hivyo dhambi zako ziwe za kwa kujua au kwa kutokuja zitafikishwa HUKUMUNI! Na zitapewa ujira wake.

Ni maombi yangu kuwa Bwana atakujalia kuliona hilo na kuweka mambo yako sawa sasa na kujitengenezea mshahara ulio bora wa uzima wa milele, kumchagua Yesu Kristo kuwa fungu lako lilolo bora, mkuu wa uzima, Biblia inasema mkumbuke muumba wako siku za ujana wako, kabla haijakaribia miaka utakaposema sina furaha katika hiyo. Hii ikiwa na maana kuwa utafikia miaka fulani hutaweza tena kumkumbuka muumba wako, kama unamsikia sasa na kumkataa.

Bwana akubariki katika Jina la Yesu, naye akupe kila haja ya moyo wako wewe uliyemchagua yeye.Amina.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *