Shalom, karibu tujifunze Maneno ya Uzima ya Mwokozi Wetu Yesu Kristo..
SWALI:
Naomba kufahamu, je upo uthibitisho wowote wa mateso ya kuzimu kwa wale watakaokufa Katika dhambi,
Hebu tusome..
Luka 16:22 “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, ALIPOKUWA KATIKA MATESO, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu NINATESWA KATIKA MOTO HUU.
25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe UNAUMIZWA.”
Maandiko hayo yanathibitisha kwamba ni kweli yapo mateso kwa wale watakaokufa Katika dhambi, na hii inatokea pale ambapo mtu amemkataa Kristo Katika maisha yake, na mwisho wa siku anakwenda moja kwa moja kuzimu kwenye mateso makali, unapofanya mambo maovu, yaliyo kinyume na Neno la Mungu, mwanamke unavaa nguo za ajabu, unavaa nguo zisizo sitiri mwili wako, unavaa suruali, unajipodoa kwa mawigi na hereni, wakati maandiko yanasema miili yetu sisi ni hekalu la Roho Mtakatifu, bali wewe unalichafua, biblia imeelezea wote wayatendao hayo mwisho wao ni Katika ziwa la moto wa milele,
Na Maandiko sehemu nyingine yanasema kuzimu haishibi watu wala haijai, ni sehemu kubwa na pana huwezi kulinganisha hata na hii Dunia tunayoishi,
Mithali 27:20 “KUZIMU NA UHARIBIFU HAVISHIBI;….”.
Mithali 30:15 “……………Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi!
16 KUZIMU; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!
Fahamu kabisa, kuzimu haina kikomo cha watu, na tena kila siku inapokea, biblia haiwezi kusema uwongo..
Unapoendelea kufanya dhambi, ni mzinifu,unasema uwongo, tabia zako ni mbaya,mtu wa anasa na Mambo ya ulimwengu huu,pombe unakunywa, elewa kabisa sehemu yako itakuwa ni kwenye ziwa la moto, kama hutabadili njia yako na kumrudia Yesu Kristo kwa kutubu kwa kumaanisha,maana ndivyo Bwana Yesu anavyotaka kutoka kwako leo,
Unakula rushwa, umekuwa ukiishi na mume,mke asiye wa kwako, ni mgomvi, na walawiti wote sehemu yao ni kwenye ziwa la moto, ni neno la Mungu linasema hivyo
Kumbuka ndugu kuzimu haina mlango wa kutokea, ukishaingia huko umeingi milele, mateso yake ni makali sana, utatamani utubu lakini haitawezekana, umeshapoteza nafasi hiyo, ni kilio na kusaga meno, utalia lakini hakuna atakayekuonea huruma, utaita lakini hakuna wa kukuitikia, wenye kiburi kitawaisha, na majuto,wakijutia mambo yote maovu waliyokuwa wakiyafanya,
wakati huu watu hawamuoni shetani,ila wakiwa kwenye mateso,kwa uchungu mwingi ndipo watagundua adui ndiye aliyewadanganya,na kuwapofusha waendelee kujifurahisha kwenye dhambi, na hiyo itapelekea kumchukia shetani lakini kiuhalisia ni kama itakuwa ni kazi bure kwasababu umeshachelewa,ilitakiwa uchukue maamuzi mapema kabla hayajakukuta hayo..
Kibaya zaidi watu wanadhania kuna maombi yoyote yanayofanyika, kutoka kwa mwenye dhambi kwenda kwa Mungu, ndugu,huu ni uwongo mkubwa wa shetani wa kudanganya ili uendelee kutenda maovu, fahamu hakuna kilio chochote kitokacho kuzimu na kumfikia Mungu, hata useme unapeleka sifa,za kumsifu Mungu,haziwezi kufika wala kufanya chochote, hakuna mawasiliano yoyote Kati ya kuzimu na Mbinguni, waliongia huko kuzimu kumbukumbu lao tayari limeshasahaulika kabisa..
Isaya 38:18 “Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako. 19 Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu..”
Zaburi 6:5 “Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?”
Yapo Mafundisho mengi yenye kupotosha yanayowatumainisha watu kuwa kuna tumaini la Kutoka kuzimu baada ya kufa, wakiaminisha kuwa mtu anaweza kutoka kwenye mateso na kuingia paradiso, Uwongo, lazima ufahamu hakuna nafasi ya pili ya kutubu kuzimu, waliopo hai hawawezi kufanya chochote kwa mtu aliyekufa, kumwombea au kumtoa kuzimu, au kupelekea mashauri kwa Mungu ili waliopo kuzimu watoke huko..
Mhubiri 9:10 “ Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, HUKO KUZIMU UENDAKO WEWE”.
Wewe unayesoma ujumbe huu, Kumbuka kuzimu ipo, ni halisi kabisa, maandiko yanasema haya mambo yote ya mateso aliandaliwa shetani na malaika zake, lakini sio wewe, hivyo anachokifanya anafanya kila njia ili aende na kundi kubwa la watu..shtuka
Mwache aende yeye na malaika zake maana ndilo fungu lao waliloandaliwa, ikiwa umeupokea ujumbe huu kwa moyo wa unyenyekevu, ni wakati wako wa kugeuka, anza kuchoma hizo nguo zisizo mpendeza Mungu, tupa chini, hereni na mawingi,acha kujichubua, kaa mbali na pombe hata kwenye kampani za marafiki usishiriki tena, anza kuliweka hekalu la Roho Mtakatifu Katika utakatifu, kwasababu kuzimu hauendi na kundi la watu, unakwenda peke yako, penye giza,na kilio,na majuto makubwa ukiunguzwa sana.. itafika wakati utatamani utubu Ili hayo yote yasingekupata lakini utakuwa umechelewa,hutapata Msaada wowote..
Ni uamuzi wako leo kumrudia Yesu Kristo ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako,nafasi ya kutubu na kutengeneza na Mungu unayo ndugu, waliopo huko wanaitamani lakini hawaipati, maanisha kusimama na Bwana,kwa kuishi maisha yanayompendeza,na kusikia Neno lake, baada ya kutubu hakikisha unaupata ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo (Yohana 3:23) Matendo 2:38, Matendo 8:16, nawe utapokea Roho Mtakatifu atakayekuongoza Katika njia zako zote Katika kumjua Yesu Kristo..
Bwana akubariki
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.