VAA MAVAZI YA KUJISTIRI 

Mwanamke No Comments

VAA MAVAZI YA KUJISTIRI 

Neno la Mungu linasema..

1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa MAVAZI YA KUJISTIRI, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

[10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”.

Ili tujue mavazi ya kujistiri ni mavazi ya namna gani, kwanza tufahamu maana ya neno KUJISTIRI.

Kujistiri maana yake ni kufunika kitu isionekane kabisa/kusitiri au kuficha.

Tunavaa mavazi ili kufunika na kusitiri mwili, na tunaposema mwili tunamaanisha kuanzia shingoni mpaka kwenye unyayo wa miguu tunapaswa kufunika kwa mavazi.

Sasa mpaka hapo natumai umeanza kuelewa mavazi ya kujistiri ni mavazi ya aina gani!!.

Kwa mfano huwezi kuvaa vinguo vya mpira ukasema umejisitiri. Mpira kazi yake ni KUBANA. Sasa unavyovaa nguo ya mpira je! umejisitiri au umebana mwili?. Nguo ya mpira inakubana mwili wote, inachora ramani ya maungo yako na kuyaanika hadharani. Sasa hapo hujajistiri bali umefunika tu rangi ya ngozi yako. Ni heri hata ukatembea uchi kabisa ili ueleweke?

Lengo la kujistiri sio fashion au desturi fulani kwamba kila mtu anayo tamaduni yake ya kuvaa, tunavaa mavazi ya kujistiri ili kuficha maumbile yetu yasiwe kwanzo kwa watu wengine.

Walio wengi lengo lao la kuvaa vinguo vya mipira/ kubana ni ili ajionyeshe, watu waone shepu yake..atamaniwe au asifiwe.

Sasa kwa watu wa kidunia ambao hawajapata kumjua Mungu wa kweli…kuvaa namna hiyo ni kawaida kwao wala hata haishangazi.

Lakini ni matusi kujiita mkristo halafu unavaa nguo zinazobana na kuchora maungo yako (nguo za kizinzi), Ni kumdharau na kumchafua Mungu ukivaa namna hiyo na huku unasema unampenda Bwana Yesu.

Ukiwa kama binti/kijana uliyeokoka, vaa mavazi ya kujistiri na ya heshima kwa Mungu na watu wanaokuzunguka.

Na ukweli ni kwamba huwezi kusema umeokoka na unayo Roho Mtakatifu ndani yako halafu ukavaa kikahaba (ukavaa vimini, kaptula, magauni ya kubana, masuruali), hapo hujaokoka, na hauna Roho Mtakatifu bali unayo roho ya ukahaba. Kwahiyo acha kujidanganya.

Amua kuokoka kweli kweli leo, amua kuchoma hayo mavazi ya kikahaba na tafuta mavazi ya kujistiri. La, sivyo utaishia jehanumu ya moto.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *