
WATU HAWA NI WATU WA DUNIA HII TU.
1Yohana 4:5 “HAO NI WA DUNIA; kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia
[6]Sisi twatokana na Mungu. YEYE AMJUAYE MUNGU ATUSIKIA; YEYE ASIYETOKANA NA MUNGU HATUSIKII. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu.
Ni vizuri tufahamu wana wa Mungu kuwa hapa duniani tupo makundi mawili, kuna watu wa dunia hii ambao Daudi anasema katika..
Zaburi 17:14 Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, WATU WA DUNIA HII ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
[15]Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, NIAMKAPO NISHIBISHWE KWA SURA YAKO.
Lakini kundi la pili ni watu wa miliki ya Mungu..watu wa taifa la Mungu, ambao ni sisi tuliokombolewa kwa damu ya Yesu Kristo Bwana wetu. (1Petro2:9-10). Na hatuna ushirika kati yetu sisi na watu wa dunia hii.
Watu wa dunia hii mioyo yao yote ipo hapa duniani, wanayawaza tu ya dunia, wanayanena ya dunia na dunia huwasikia kwakuwa wao ni wa dunia hii tu….hivyo fungu lao li katika mambo ya dunia hii tu.. hawana sehemu katika ufalme Mungu, wanachotafuta ni kujaza matumbo yao na kutafuta uridhi wa mambo ya dunia hii tu basi. Na Mungu anawafanikisha katika hayo kwasababu fungu lao liko hapa hapa, kwahiyo hatushangai hata wakifanikiwa sana.
Biblia imetuagiza tusichangamane nao wala kutamani maisha yao, lakini anasema..
“Sisemi msichangamane kabisa na WAZINZI WA DUNIA HII, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.
[11]Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.” (1Wakorintho5:10-11).
Wazinzi wanaozungumziwa hapo ni watu wa dunia hii, mtu yoyote ambaye hajakombolowa kwa nguvu ya msalaba (hajaokoka) ni mzinzi hata kama hafanyi hicho kitendo kwa nje.
Watu wa namna hii hatupaswi hata kula nao…yani kushirikiananao, SI katika mambo mema lakini kuiga na kufuatisha namna yao ya kidunia. Biblia imetuagiza tusifuatishe..
Warumi 12:2 Wala MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Kwahiyo sisi kama wana wa Mungu, watu wa ufalme wa mbinguni, tujitenge na namna zote za kidunia ikiwemo uvaaji wa kidunia/kizinzi, mapambo ya namna zote, TUSIVAE kama watu wa dunia hii, TUSISUKE wala KUNYOA kama watu wa dunia hii, TUSIZUNGUMZE kama watu wa dunia hii tusielekeze mioyo yetu katika mambo ya dunia hii, kwa ufupi tuwe tofauti na watu wa dunia hii katika mwenendo wote.
Yuda 1:17-21Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo,
[18]ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu.
[19]Watu hao ndio waletao matengano, WATU WA DUNIA HII TU, wasio na Roho.
[20]Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,
[21]JILINDENI katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate UZIMA WA MILELE.
Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.
Maran atha (Bwana Yesu anarudi)
Waweza kuwasiliana nasi kwa namba zilizopo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.