MAENEO ANAYOJARIBIWA MWAMINI. (Eneo la kwanza analojaribiwa Mwamini.)

Biblia kwa kina No Comments

MAENEO ANAYOJARIBIWA MWAMINI.
(Eneo la kwanza analojaribiwa Mwamini.)

Shalom nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Wakristo wengi wanaangamia kwa sababu ya kukosa maarifa, ni muhimu sana kuwa maarifa/ufahamu kwa sababu hakuna vita ambayo Mkristo anaweza kushinda ikiwa hana maarifa unless Neema ya Mungu tu isimame.

Tupo katika vita na vita vyetu si juu ya damu na nyama na ni vita ambavyo vinahitaji maarifa ndio maana maandiko yanasema watu wangu “ wanaangamizwa” sio wanaangamia kama wanaangamizwa maana yake kuna kitu ambacho kinachukua nafasi ya ujinga walio nao watu wa Mungu ili kuwaangamiza..

Sasa ni muhimu kujua maeneo mwamini anayojaribiwa..

Watu wengi hufukiri majaribu labda yatakuja kwenye eneo la kifamilia,Kikazi,uchumi nk.

Ni kweli kabisa majaribu yanakuja katika haya maeneo lakini leo nataka tuangazie eneo moja tu.

1.KUJALIBIWA KWA KILE UNACHOKIJUA.
Eneo la kwanza kabisa ambalo mwamini hujaribiwa ni katika eneo la kile anachokifahamu..

Hii tunaona toka mwanzo shetani alipokuwa akimdanganya Hawa, Hawa hakudanganywa katika kitu asichokijua bali kile kile anachokijua kwa muda mrefu na alikua akiishi akijua hatakiwi kifanya kitu gani, ndio maana yeye mwenyewe hakua na uthubutu wa kufanya chochote.. na hata nyoka alipomuuliza alielezea vizuri kwamba hapaswi kufanya na alikua anajua madhara yake na ndio maana alisema madhara yake ni nini..

Kwa lugha nyingine tunaweza kusema Hawa alishawishika kutokana na sifa alizopewa baada ya kufanya kile kitendo, si kwamba Hawa alifanya lile jambo akiwa hajui kama anakwenda kinyume la! Alijua lakini kwa sababu alitamani kuzipata sifa hizo alizoelezewa..

Maana yake aliona kuna vitu kumbe Mungu kawaficha au hataki wakijue na ni kweli Mungu alikua amewaficha baadhi ya mambo kwa makusudi ya wao kuja kujua baadae maana kama wangelijua mapema kitu hicho kingewaangiza maana yake Mungu alikua tayari kuwafundisha kwa wakati ambao utakua umefika wao kujua.

Mfano wewe huwezi kuanza kumfundisha gari mtoto wako wa miaka 5 kuendesha gari lako sio kwamba hutaki ajue lakini wakati bado ukifika wakati ameshajitambua hutamzuilia kujifunza ma akajua..

Vivyo hivyo Bwana Yesu kule jangwani alijarubiwa katika vitu ajavyovijua yeye mwenyewe.

Mitume walipigwa na kutishwa kuuawa kwa ajili ya kuacha kuhubiri habari za Bwana Yesu. Lakini kwa sababu walisimama na ukweli ndani ya mioyo yao wakakubali kufa..

Walikua wanajua wakimkana Bwana hawana maisha tena watakwenda kwenye ziwa la Moto..

Matendo ya Mitume 5

28 akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.

29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.

Unaona hapo walikua wakizuiliwa kuhubiri Neno la Mungu ilihali Kristo alishawaamuru kufanya hivyo maana yake walijua wanatakiwa kufanya hivyo.

Walipewa agizo na Bwana Yesu..

Mathayo 28:19
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;”

Vivyo hivyo shetani hajabadilisha mbinu jaribu hili ndio la kwanza kabisa na ukishalishinda hili ndio hapo ataanza kugusa familia, uchumi,  kwa sababu anajua kama akikushinda katika hili eneo hata kama una kila kitu utakua hauna maana tena katika ufalme wa Mungu na uko nje na kusudi lako na ataweka kusudi lake ndani yako..

Atainuka kukujaribu kwenye eneo la ibada atataka uende kazini mpaka siku ya Bwana, unajua hutakiwi kuzini lakini ataweka vishawishi ili utende, angalia ni mambo gani unayoyafahamu na je unasimama kumpinga au unafanya tu? Omba Neema ya Bwana Yesu ikusaidie..

Hivyo kuwa makini sana na eneo unalolifahamu kwa sababu ukimpa nafasi shetani cha kwanza atakupumbaza uache kuona kama kitu ambacho kina madhara na uone ni kawaida tu.

Nakuombea katika Jina la Yesu Kristo hutayumbishwa tena na upepo wa kila namna utasimama thabiti juu ya kile unachokijua.

Waefeso 4

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.

15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.

Bwana Yesu akubariki.
Mawasiliano:0613079530.
@Nuru ya upendo.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *