UNATAWALA KAMA MFALME?

Biblia kwa kina No Comments

UNATAWALA KAMA MFALME?

Shalom nakusalimu katika jina la Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu.

Umewahi kufikiri kwa nini sehemu nyingi sana biblia inatuita sisi tulio zaliwa mara ya pili kuwa ni wafalme? Kwa nini isiseme tutawale kama maraisi au kama majemedali nk, katika muktadha au mazingira ya zamani hakukua na maraisi,wala wabunge nk ndio maana kipindi kicho neno “mfalme” au “Wafalme” lilitumika kwa sehemu kubwa sana lakini  nataka tuangalie kwa undani kidogo juu ya hili jambo, kuna mambo muhimu sana ya kuelewa hapa.

Maandiko yanaposema sisi ni wafalme tunatakiwa kufahamu kwanza kuitwa mfalme sio jina tu au cheo la! Bali ni nafasi yenye mamlaka, nafasi hiyo anapokaa mtu hata kama mwazo alikua ni mtu wa kawaida  tu lakini anakua ni mtu wa tofauti kabisa kwa sababu ya ile nafasi.

Sasa tunapoitwa wafalme sio jina tu basi bali ni mamla tuliyonayo baada ya kumwamini Yesu Kristo ni muhimu sana kuelewa hili kama usipoelewa basi utaishi kama mtumwa ilihali maandiko(uhalisia) yanasema wewe ni mfalme na tangu mwanzo asili yak o ni kutawa/kumiliki soma Mwanzo 1:26-28 utaliona hilo.

Sasa ni muhimu kuelewa character/sifa za mfalme ni zipi  ukizielewa hizo kwa undani kwa ufunuo wa Roho wa Mungu maisha yako yataanza kuwa na mabadiliko makubwa sana.

1. Mfalme anaposema neno haliwi kama Sheria bali linakua amri.

Neno la mfalme ni sheria/amri haijalishi amesema katika hali ya furaha ama hali ya huzuni maana yake neno la mfalme ni mamlaka ambayo inatakiwa kutekelezwa bila majadiliano ya kwa nini imekua hivyo bila kuangalia madhara yake ni yapi au ni nini? Kwa sababu Neno la Mfalme lime beba Mamlaka.

Mfalme anaposema lifanyike jambo Fulani hajiulizi au kuwa na wasi wasi kuwa huenda amri yake ikafanyiwa kazi au isifanyiwe kazi, haombi watu watii bali watu watatii hata kama hawataki.

Neno la Mfalme ni amri ambayo inatekelezwa bila kukosolewa au kurekebishwa unless mfalme mwenyewe atangue lakini kidemokrasia mamlaka ya raisi inaweza kukosolewa na kupingwa na wanasheria na wadau mbali mbali ya haki za binadamu lakini sivyo inaweza kufanyika kwa mfalme.

Mfalme anakuwa yuko juu ya sheria sio kama raisi anakuwa chini ya sheria, mfalme hatawali kwa kipindi Fulani labda cha muhula la bali yeye anatawala hata mpaka wakati atakapokufa haendi kugombea na kuomba uongozi ana lithi( tumerithi kwa Kristo)nk

Ukisoma katika maandiko tunaona wafalme kama wakina Dario,Nebukadneza,Daudi nk
Wakati Daniel aatupwa kwenye tundu la simba ni amri ya kifalme ilitoka ambayo hakuna alieikosoa  wala kuitengua kwa sabababu ya kipindi hicho amri ya kifalme ilikua haitenguliwi.

Danieli 6:16” Basi mfalme akatoa amri , nao wakamleta Danielii, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.”

unaona hapo anasema “Mfalme akatoa Amri” hasemi “Mfalme akaomba au akatoa pendekezo nk”

Ukisoma pia Nebukadneza alitoa amri Shedrack,Meshack na Abednego kutupwa katika tanuru la Moto ni Amri ambayo ilitekelezwa kikamilifu hakuna mahali ambapo Mfalme alitoa amri na isifanyiwe kazi.

Lengo langu sio kukupa historia za wafalme lakini nataka uelewe kwa kina maandiko yanavyotuita kuwa sisi ni wafalme. Maana yake iko mamlaka ndani yetu sisi.

Sasa tumeona character/sifa moja ya mfalme sasa tuhamishe ufahamu huo huo katika mambo ya rohoni ndio uhalisia huo ulivyo.

Hivyo chochote tutakachoomba au tunachotamka kinakua lakini hatuoni matokeo ya matamko tunayoyatamka kwa sababu hatujui uhalisia wetu sisi ni wakina na nani, maeneo amabayo tunatakiwa kutamka tunaomba magonjwa nk hatuombi we command/tunaamuru.

Mamlaka inakua haina nguvu kwa sababu tunatamka kwa mashaka na wasiwasi kwamba huenda ikawa ama isiwe lakini leo mtumishi wa Mungu weka ufahamu wako kuwa wewe ni mfalme na chochote utakachokitamka kitakua kwa sababu neno lako unalolitamka katika ulimwengu wa Roho haliendi bure linakwenda kutendewa kazi.

Hakuna neno unalolitamka lisitendewe kazi na ndio maana maandiko yanatuonya sana katika eneo la kuchunga vinywa vyetu maana humo tukitamka neno baya litakuwa au tukitamka zuri linakua kwa sababau sisi ni wafalme na maneno yetu hayawi maneno bali amri na wapo wakuitendea kazi (ukitamka maneno mabaya juu yako umeamuru ufalme wa giza ufanye kazi katika maisha yako).

Yesu Kristo maandiko yanasema alikua akitamka kama mtu mwenye amri na sio kama waandishi na mafarisayo walivyokua wakifundisha Kristo alikua akifundisha kama mwenye amri.

Yesu alikua akiamuru mambo mengi yanakua  kwa sabababu alijua yeye ni nani hivyo wewe na mimi kuelewa kwa kina sisi ni wa kinanani hiyo itatupa kubadilisha mwenendo wetu na maisha yetu kwa ujumla.

Mfalme haombi anaamuru, yako mambo ambayo tunaomba mbele za Bwana Rehema na Neeema hatuamuru nk lakini kwenye eneo la maisha yakow wewe unasimama kuamuru ikiwa ni swala la kifedha,kazi,biashara,afya yako, shetani na mapepo yake n haya yote tunaamuru.

Usijiangalie wewe, ukijiangalia wewe utashindwa lakini angalia mamlaka iliyoko ndani yako iko mamlaka ikubali kwanza na kisha anza kutembea katika hiyo utaanza kuona mabadiliko.(watu wengi hatukubali uhalisia wetu katika maandiko japo tuna kiri kwa vinywa)

Luka 10:19” Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”

Unaona hapo? Hasemi “ atatupa mamlaka ” bali ametupa mamlaka.

Waefeso 2:6 “Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;”

Unaona hapo? Hasemi “ _atatuketisha_ ” bali anasema “ Ametuketisha” maana yake tayari ameshakwisha kufanya hivyo tumeketishwa Pamoja na Kristo kwa namna ya mamlaka iliyoko katika Kristo Yesu ipo ndani yetu pia.

Katika somo lijalo nitafundisha juu ya namna gani tumepata mamlaka katika upana ili tusiendelee kutembea kama watumwa.

Bwana Yesu akubariki sana
Contacts:+255613079530
@Nuru ya upendo.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *