ISOME BIBLIA YAKO KATIKA UFAHAMU HUU.

Biblia kwa kina No Comments

ISOME BIBLIA YAKO KATIKA UFAHAMU HUU

SEHEMU YA 01

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakri maneno ya uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Neno la Mungu sio hadithi au story Fulani ambayo inatuelezea nini kilitokea katika historia nk Neno la Mungu ni zaidi ya hivyo…

Neno la Mungu ni  hai ni neno ambalo ni uzima, ni neno ambalo ndani yake kuna nguvu kubwa sana na ya ajabu ikiwa mtu ataliamini Moyoni mwake.

Tunashindwa kuona nguvu na uwezo ulio ndani ya Neno la Mungu kwa sababu tunalisoma katika ufahamu usio sahihi na hiyo inapelekea kuona ni maandiko matakatifu tu ambayo yaliandikwa na watu wa Mungu zamani na ndio maana tunapofanya ukiri wa Neno la Mungu juu ya maisha yetu ni kama tunacheza na hatuoni mabadiliko ni kwa sababu kwanza ya ufahamu tulionao kuhusu Neno la Mungu(namna tunavyolisoma) maana yake tukiwa na ufahamu sasa wa neno la Mungu basi tutaona matokeo.

pia kukosa ufahamu sahihi wa kuisoma biblia kunapelekea pia kuwa na ufahamu usio sahihi na matokeo yake ufahamu usiokua sahihi basi hakuna pia madhirisho.

Sasa unatakiwa kuisoma biblia yako katika ufahamu upi?

Kwanza ni Muhimu kufahamu biblia ni Neno la Mungu ambalo ni kweli na hakika ikiwa utaliamini ndani yako.

Sasa biblia imeandikwa katika wakati uliopo,wakati uliopita na wakati ujao nk ni muhimu sana kuelewa haya maeneo kwa sababu yatakua na msaada kwako ikiwa utaelewa nyakati ambazo biblia imezitumia lakini usipotambua nyakati ambazo biblia imezitumia katika kuwasilisha ujumbe kwetu  basi kuna vitu vingi sana utavikosa.

Tutaangalia nyakati mbili zote kwa Pamoja kwa Neema za Mungu. ni muhimu sana mtumishi wa Mungu maana hii itakupa kujua kipi tayari ni haki yako na kuendelea kukikiri na kukidai mpaka kionekana lakini kama usipofahamu maana yake hutajua hata kipi kilicho cha kwako na hutaweza kusimama na kudai haki yako kwa ujasiri.

1.WAKATI ULIOPITA.

Wakati uliopita ni wakati wa unaotumika kuelezea vitendo, matukio, au hali za kuwepo ambazo tayari zimetokea. wakati huu Unaonyesha kwamba muda wa tendo hilo uko katika wakati uliopita na umekamilika.

Kwa nini ni muhimu kuelewa mambo madogo madogo kama haya kwa sababu haya ndio yanatupa kufahamu ni mambo gani amabayo tayari Kristo alishayafanya na tuwapo katika hali zozote katika maeneo ya maombi na ukiri basi tuwe na ujasiri wa kutamka ambapo Imani itajengeka imara.

sasa tutaenda kuona namna gani Wakristo wanakaa katika hali za utumwa ilihali tayari Kristo alishakwisha kumaliza kitu hicho.

Tutaangalia maeneo kadhaa..

i.Uponyaji na ukombozi.

hili ni tukio ambalo Kristo alishakwisha kulifanya tangu pale msalabani, ni jambo ambalo limeshakwisha kufanyika yaani limekamilika.

Isaya 53:5” Bali ALI jeruhiwa kwa makosa yetu, Ali chubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.”

Unaona hapo hiyo sentensi hapo mwandishi anatumia anasema “bali alijeruhiwa….” ni wakati uliopita kumbe Kristo alishakwisha kupigwa kwa sababu ya maovu yetu na makosa yetu na anatumia wakati uliopo na endelevu kwamba “kwa kupigwa kwake sisi tumepona” kupigwa kwa Yesu katika wakati uliopita kumepelekea uponyaji endelevu kwetu hata sasa.

Sasa wakristo wengi utaona wanaomba “ Baba naomba uniponye, niepushe na hukumu/adhabu, na watumishi wengi wanasema “Usijali Bwana atakuponya au ikiwa ni mapenzi ya Mungu basi atamponya tuendelee kumuomba” ukiangalia katika mstari huo uponyaji  tayari umeshakwisha kufanyika ni sisi kukiri kwa Imani.

kumbuka ukiri sahihi sawa sawa na Neno la Mungu kunatengeneza ujasiri ndani ya mioyo yetu na Imani.

Ukombozi dhidi ya dhmabi.

Maadiko yanasema hivi

Warumi 6:17-18 “17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;

18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.”

Unaonah apo? Maandiko yansema “tulikuwa watumwa wa dhambi” ni wakati uliopita.. maana yake tayari tunao msamaha wa dhambi hatutakiwi tena kujiona kama watu wenye dhambi lakini tunapaswa kukiri ndani yetu nguvu ya ushindi juu ya dhambi Kadiri unavyokiri ushindi juu ya dhambi ndivyo ambavyo unazidi kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi..
(haiji kwa siku moja fanya kuwa ni maisha yako ya kila siku ukiri endelevu)

Dhambi inakua na nguvu juu ya mtu pale yeye mwenyewe anavyojiona ni dhaifu hawezi kuishinda dhambi. lakini maandiko yanasema tulikuwa watumwa na sasa tumewekwa huru. Haleluya….

Unaoana mstari wa 18 unavyosema? “ mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi mkawa watumwa wa haki..” bado kuna watu wanaona hawajasemewa dhambi, dhambi ina nguvu juu yao.

Lakini sio kweli sema “ *mimi nimewekwa mbali na dhambi na mimi  sio mtumwa wa dhambi”* haijalishi bado unaona ndani yako kuna dhambi inakutesa umejaribu kuacha umeshindwa nk unapofanya ukiri sawa sawa na Neno la Mungu unakwenda kuvunja mapingu na utumwa wa kila namna utaanza kuona ndani yako hata ufahamu wako unakaa katika namna ya ushindi..

Ushindi unaanzia katika eneo linaloitwa ukiri, ukisoma vita vya Daudi na Goliati ni vita ambavyo vilikua katika eneo linaitwa ukiri na ukiri wa Daudi ulikua na nguvu kwa sababu alikua anakiri juu ya Neno la Mungu na juu ya yale ambayo ameona Mungu akumtendea mambo makuu katika maisha yake..

Unataka kutembea katika ukiri wa Neno la Mungu zima kabisa hisia zako washa Imani utembee katika Neno utaanza kuona ushindi mkubwa sana ndugu yangu.

Tutaendelea kuchambua zaidi namna gani tuzifahamu nyakati zilizoandikwa kwenye maandiko na kutembea nazo ili uweze kuona mabadiliko ndani yako. Na kuanzia leo katika jina la Yesu Kristo nakutamkia neem ana baraka ya kutembea katika ushindi, tawala,miliki na shikilia kile maandiko yamesema ni cha kwako usikose sehemu ya pili..

Ubarikiwe sana.

@Nuru ya upendo.

Mawasiliano: 0613079530

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *