JE NI ALAMA GANI UMETIWA?

Biblia kwa kina No Comments

JE NI ALAMA GANI UMETIWA?

Shalom. Karibu tujifunze biblia.

Ezekieli 9:3-4 Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni.

[4]BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, UKATIE ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO VYA WATU WANAOUGUA NA KULIA KWA SABABU YA MACHUKIZO YOTE YANAYOFANYIKA KATI YAKE.

Ndugu, ni vizuri kufahamu mapema kuwa tunaishi katika nyakati ambazo watu wote wanatiwa alama (chapa) katika roho.

Hii inamaana usipotiwa alama/muhuri wa Mungu, basi utatiwa muhuri wa shetani (chapa ya mpinga-kristo) ambao tunaisoma katika…

Ufunuo 13:16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe CHAPA katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;

[17]tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

[18]Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.

Kuipokea chapa ya mnyama/Alama ya Mnyama ni kuukataa muhuri wa Mungu ambao ni Roho Mtakatifu (Waefeso 4:30), hapa duniani kuna pande mbili tu, upande wa Mungu na upande wa shetani, hivyo ukikosa kuwa na Roho wa Mungu, maana yake ni una roho ya shetani nayo ndiyo chapa ya mnyama…tofauti na wengi wanavyodhania kuwa kuna siku moja watu watapigwa chapa ya 666 katika nyuso zao.

Chapa ya mnyama (mpinga-Kristo), inatenda kazi sasa hivi katika roho. Na watu wanaendelea kutiwa pasipo hata kujua, lakini hivi karibuni baada ya wateule wa Mungu waliotiwa alama/chapa au muhuri wa Mungu kunyakuliwa, ndipo wote waliokuwa wametiwa muhuri wa shetani (roho ya mpinga-kristo), watadhihirisha chapa yake kwa nje.

Hivyo ndugu mteule, huu ni wakati wa kuhakikisha umepokea muhuri wa Mungu ambao ni Roho Mtakatifu kwa nguvu zote, kwani usipopokea muhuri wa Mungu…utapokea wa shetani.

Na kama unavyojua shetani hana pa kukupeleka…kwani yeye mwenyewe anasuburia kutupwa katika ziwa la moto pamoja na wote wanaomfuata.

Kwahiyo amua leo kuchagua njia ya uzima ili upokee Roho Mtakatifu aliye muhuri wa Mungu. Kumbuka muda tuliobakiwa nao ni mfupi sana, Unyakuo utapita muda wowote!!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *