FUKUZA MAWAZO MABAYA NDANI YAKO

Biblia kwa kina No Comments

FUKUZA MAWAZO MABAYA NDANI YAKO

Watu wengi wamekuwa watumwa wa zinaa kwasababu ya kukubaliana na mawazo mabaya ya zinaa yanapokuja ndani yao, hivyo wanajikuta kwa nje wanajizuia kuzini lakini kwa mioyo yao wanazini.

Ni vizuri kufahamu kuwa hakuna maombi yatakayokusaidia kutoka katika huu utumwa, isipokuwa ni wewe kufukuza/kuondoa na kukataa kabisa uzinzi ndani yako. Biblia inaposema “Ikimbieni zinaa” (1Wakorintho6:18), haimaniishi tu kukimbia kwa nje…lakini pia unaanza kukimbia mapema ndani ya moyo wako, unapoona mawazo hayo yanakuja ndani yako.

Utauliza.. “nitakimbiaje”.. Wazo linapokuja kichwani la kwenda kufanya hivyo, unaanza kulikataa likiwa huko huko kichwani, unapuuzia hayo mawazo, unaacha kufikiria fikiria, unafikiria kufanya mambo mengine,

Lakini ukijilegeza na kusema acha niwaze kidogo…nione mwisho wake, nakuambia utaishia kwenda kujichua, au kuendelea kuzini na mwishowe itakuwa ndiyo tabia yako hiyo..utaishia kusema mimi ndio niko hivi, ni udhaifu wangu.. kumbe wewe ndio umekubaliana na mawazo hayo ndani yako.

Kumbuka kamwe hauwezi kushinda zinaa kama hujaokoka kweli kweli kwa kuzaliwa mara ya pili, na halikadhalika baada ya kuokoka unapaswa kujitenga na vichocheo vyote vya zinaa ikiwemo mazungumzo mabaya, miziki, picha za uchi, filamu zenye maudhui ya zinaa n.k.

1 Wakorintho 7:8 “Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.

[9]Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.”

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *