FIKIRI KAMA JINSI MUNGU ANAVYOFIKIRI
Shalom nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu.
Kufikiri kama anavyofikiri Mungu ndio kunakompa uhalisia mtu kumuelewa Mungu na kutembea katika ushindi. Wakristo wengi tunafikiri kwa namna tofauti kabisa Mungu anavyofikiri ama anavyoona ndio maana tunajikuta tunapitia maisha magumu kuanzia rohoni mpaka mwilini.
Sasa kufikiri kama Mungu anavyofikiri unaweza ukajiuliza ni kwa namna gani ilihali maandiko Yanasema Mawazo yetu ni tofauti kabisa na Mawazo yake yeye inawezekaneje ikawa hivyo?
Isaya 55:8-9 “8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.
9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.”
Sasa inawezekanaje ikiwa tayari maadiko yamesema hivi na kufikiri huko ni kwa namna gani? Je inawezekana tukafikiri/kuona sawa sawa na Mungu jinsi anavyoona/fikiri.? Tuone maandiko pia yanasemaje?
Wakolosai 3:1 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi”
Unaona hapo anasema “.. YAFIKIRINI YALIYOJUU…” kwa hiyo kumbe inawezekana na kupitia kufikiri huku kunabadilisha kabisa mtazamo wetu na maisha yetu kwa ujumla kuanzia rohoni mpaka mwilini.
Maandiko pia yanasema…
2 Wakorintho 2:16 “ Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.”
Unaona hapo tunayo nia ya Kristo ndani yetu maana yake tunao ufahamu,akili ya Kristo ndani yetu yaani tunaweza kufikiri kama yeye na tunaweza tukatembea kama yeye jinsi alivyotembea.
Sasa kusema kufikiri kama Kristo anavyofikiri maana yake sio kufikiria katika Mawazo kama tuliyonayo bali ni kuona ukweli na uhalisia katika Neno la Mungu. Kuelewa Kristo amezungumza nini juu ya maisha yako? Wewe ni nani ndani ya Yesu Kristo, una uwezo upi katika Yesu Kristo nk
Wakristo wengi tumejenga ufahamu katika mambo ambayo sio kweli kimaandiko na tumejenga ufahamu wetu hapo kiasi kwamba tumeona kuwa hivyo ni vya kweli “ iko hivi ukijenga ufahamu katika kitu ambacho sio sahihi maana yake unakifanya kile kitu kiwe kama kweli katika maisha yako kwa sababu ya udanganyifu wa shetani.”
Yaani ukijenga ufahamu katika kitu ambacho sio sahihi kuamini kwako pia kunakua sio sahihi na unaweza kujikuta kwenye Kamba za shetani kwa sababu ya kukosa maarifa.
Hivyo haimaaanishi kweli una Kristo ndani yako lakini ukikosa maarifa utaangamia.
Leo hii Wakristo wengi wamejengewa Imani kwenye vitu ambavyo sio kweli mfano leo kuna wimbi kubwa la Wakristo ambao wanaamini bado kuna laana za ukoo katika maisha yao na wanapambana kila siku kuzivunja madhabahu ziwaachie.
Kuna Wakristo wanaamini na kuaminishwa hivyo kuwa mara Nyota zao zimeibiwa, bado mizimu ya mababu inawafatilia wasipofanya vitu Fulani watauwawa na nguvu za nmababu, wameaminishwa wanatakiwa kutoa sadaka za ukombozi ili kujitoa kwenye laana hizo, wanatoa sadaka za kujikomboa na kujiachanisha na madhababu nk.
Lakini hebu turudi kwenye maandiko je yanasema hivyo? Au kuna maelekezo kama hayo mitume waliyatoa au Bwana Yesu aliyatoa? Je kuna mahali ambapo Bwana Yesu alisahau kabisa kuzugumzua kitu kama hiki? Au kuna jambo Yesu katika huduma yake alilisahau? Mitume walifundisha watu namna kama hizi.?
Utagundua ukisoma kwenye maandiko utaona kwamba hakuna kwenye nyaraka zozote kabisa hilo jambo halipo. Kitu walichokuwa wanakisisitiza na kukirudia mara nyingi sana ni kuhusu ukombozi kupitia Yesu Kristo.
Kwa nini kwa sababu ukiielewa kazi ya Yesu Kristo aliyoifanya pale msalabani huwezi kupoteza muda wako na kutapeliwa kwa sababu ya mambo ambayo sio ya kweli na maandiko hayajaangazia wala kuyazungumzia kama yangekua na umuhimu sana basi yangewekwa hakuna kitu cha muhimu kwenye maandiko ambacho kimesahaurika.
Wekeza muda wako mwingi sana kuelewa kazi ya Yesu Kristo kama ukiielewa hapo ndio utaanza kufikiri kama Mungu anavyofikiri maandiko yanasema yeye alitukomboa katika laana.
Kama maandiko yanasema
Wagalatia 3:13 “ Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;”
Sasa kama yeye alituokoa katika laana hiyo laana ambayo inakufata ni laana ipi naya ya wapi?, kama sio uongo?
Maandiko yanasema ametuhamisha kutoka katika nguvu za giza wewe unaambiwa nguvu za giza zimekushika toa sadaka funga na kuomba zitoke how?
Wakolosai 1:13 “ Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;”
Umehamishwa kwenye ufalme wa giza unaambiwa umeshikwa tena kwenye ufalme wa giza inawezekanaje.
KUFIKIKIRI KAMA MUNGU NI KUKUBALI NA KUELEWA MAANDIKO YAMESEMA NINI? Amini maandiko kile yamesema ndio fikra za Mungu za kweli zinavyoona kuhusu wewe umezaliwa mara ya pili na umekua kiumbe kipya ya kale yamepita na tazama yamekua mapya usikubali kufikiri inje na maandiko uhalisia wako wewe uko kwenye nyaraka za mitume wewe ni nani na unaweza kufanmya nini na nimshindi tafakari na kili kila siku ushindi.
Ubarikiwe sana.
mawasiliano:0613079530
@Nuru Ya Upendo.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.