FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUNZA KITU.

Biblia kwa kina No Comments

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUNZA KITU.

(Ndoto ya dada Marry kutoka Kenya)

Bwana Yesu asifiwe mtumishi, naomba nisaidie kupata tafsiri ya hii njozi maana imenijia kwa uzito sana:

Nilikuwa nasoma kitabu cha ufunuo…nilipomaliza nikaenda kupumzika, Nikaota nipo katika njia mbili, moja ilikuwa pana na nyingine nyembamba (kama biblia inaposema kuwa ipo njia pana iendayo upotevuni, na njia nyembamba iendayo uzimani (Mathayo 7:13), nilimwona mama mmoja akitembea katika njia hiyo pana, na hiyo njia pana (barabaraba) kulikuwa na maji machafu mbele yake lakini yule mama ni kama hakujali.. aliponiona akaniambia “kuna joka mkubwa yupo mbele yetu, nilipoangalia nikaona kweli joka mkubwa mwekundu, mwenye miguu mingi, nikageuka kupita katika ile njia nyembamba lakini yeye hakujali aliendelea mbele bila wazi wazi, mimi nikawa natembea katika njia hiyo nyembamba, mbele nikakutana na kundi la mbuzi ambao walikuwa wametawanyika bila mchungaji, nikawaza sasa hao mbuzi si watamezwa na yule joka!!.. baada ya hapo nikazinduka katika uzingizi.

Ni wazi kuwa Bwana amekuonyesha hali halisi inayoendelea katika nyakati hizi..Na ujumbe huu nitaweka mtandaoni ili ikawasaidie wengine pia..

Bila shaka ujumbe huu unalenga hali ya wakristo katika nyakati hizi za mwisho, Bwana Yesu alisema..

Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.

[14]Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache”. (Mathayo 7:13-14).

Ndicho kitu Bwana amekuonyesha, kuwa kuna wakristo wanatembea katika njia pana…ndio yule mama uliyemuona…lakini kati yao kuna wengine wakiona hatari iliyo mbele yao wanakuwa wepesi kugeuka na kutembea katika njia ya uzima mfano wa wewe, lakini kinachohuzunisha ni kwamba.. leo hii wakristo wengi wanajua kabisa njia wanayoiendea kuna hatari mbele (kuna JOKA), lakini wanafumba macho yao wasione kama Bwana Yesu alivyosema katika..

Mathayo 13:15 “Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, NA MACHO YAO WAMEYAFUMBA; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya”.

Kumbuka hawajafumbwa na ibilisi, wao wenyewe wameyafumba, kwasababu gani? Kwasababu wameipenda giza kuliko nuru ndio tafsiri ya yale maji machafu ikifunua uovu wa ulimwengu, lakini watu wanaifurahia kama vile huyo mama hakuona hata shida na yale maji wala hakujali hatari iliyo mbele yake. Biblia inasema

Yohana 3:19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu WAKAPENDA GIZA KULIKO NURI; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

Sasa huyu joka anafunua nini? Bila shaka biblia imetoa tafsiri katika kitabu cha ufunuo ambacho ulikuwa ukikisoma kabla ya kulala, maandiko yanasema..

Ufunuo wa Yohana 12:3-4,9 “Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, JOKA KUBWA JEKUNDU, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.

[4]Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.

[9]Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, AITWAYE IBILISI NA SHETANI, AUDANGANYAYE ULIMWENGU WOTE; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Umeona hapo, tafsiri ya yule joka anafunua ibilisi mwenyewe, na katika siku hizi ibilisi amekwisha andaa mfumo wake ambao kipindi kifupi baada ya unyakuo wa watakatifu, atapewa mamlaka ya kuitawala hii dunia kwa muda wa miaka mitatu na nusu, na katika kipindi hicho atahakikisha amewameza watu wote na kuwaingiza katika mfumo wake ndio ile chapa ya mnyama (ufunuo 13)

Kumbuka sasahivi shetani haangaiki na watu walio nje ya imani au wakristo vuguvugu, bali anawekeza nguvu zake zote kutafuta wakristo waliosimama kweli kweli ili wawameze , ndio maana biblia inasema katika…

1 Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu AMMEZE“.

Sasa wale mbuzi uliowaona ndio wale wakristo jina ambao wamemwacha Mchungaji mkuu Yesu Kristo, na hivyo wapo hatarini kumezwa na yule joka. Kumbuka tunaposema wakristo jina hatumaanishi wale wakristo wasiojishughulisha na kazi ya Mungu kabisa, sio wale ambao hawaendagi kanisani, hapana! Wengi wao wanaenda kanisani vizuri, ni waimbaji wa kwaya vizuri, ni watoaji wazuri, wengine ni watumishi lakini hawaishi sawa sawa na Neno la Mungu, uvaaji wao hauna tofauti na watu wengine wa nje, wanaweza wakavaa kwa kujistiri kanisani lakini huko nje wanatembeza miili yao uchi ili wafanane na walimwengu wengine, na kibaya zaidi wengi wao wanajua ukweli kuwa hawapo sawa na Kristo lakini wameipenda giza kuliko nuru.

Ndugu yangu unayesoma ujumbe huu, hebu leo jitathimini upo katika kundi lipi la wakristo? Bwana Yesu alisema siku ile atawatenga mbuzi na kondoo akimaanisha makundi mawili ya wakristo.

Mathayo 25:31-33,41 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

[32]na mataifa yote watakusanyika mbele zake; NAYE ATAWABAGUA KAMA VILE MCHUNGAJI ABAGUAVYO KONDOO NA MBUZI;

[33]atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.

[41]Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

[41]Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

Tunaishi ukingoni mwa nyakati, Kristo amekaribia kurudi sana, na maandalizi ya mpinga Kristo yapo tayari!!

Kama hujampokea YESU ipasavyo, basi tambua upo hatarini sana, unachungulia ziwa la moto. Tubu sasa mgeukie Bwana Yesu kwa kumaanisha kabisa kabisa..na Bwana atakupokea na kukurehemu.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *