MIMI NAMI NITACHEKA SIKU YA MSIBA WENU. Jina la Bwana Yesu libarikiwe daima, karibu tuendelee kuyatafakari maneno ya Mungu. Mambo mengi yanayoendelea hapa duniani yamebeba ufunuo wa mambo yalivyo rohoni. Kwa mfano hukuku wanazotoa wanadamu kwa wanadamu wenzao katika mahakama yao, ni ufunuo wa hukumu ambayo Mungu ameandaa kuwahukumu wanadamu, ambao kila mtu atahukumiwa kulingana ..
Author : Yonas Kisambu
ENYI WAPUMBAVU, LINI MTAKAPOPATA AKILI? Zaburi 94:7 “Nao husema, BWANA haoni; Mungu wa Yakobo hafikiri. [8]Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini; Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili? Mpumbavu ni nani kibiblia? Mpumbavu ni mtu asiye na akili, na hapa hatuzungumzii akili ya darasani au kuwa na maarifa ya kidunia, hapana, unaweza ukawa na degree zote au ukawa namba ..
JIHADHARI NA MAFUNDISHO YA YEZEBELI Yezebeli ni nani? Yezebeli alikuwa ni mwanamke mwenye asili ya nchi ya Lebanoni, mahali pajulikanapo kama Sidoni (1Wafalme 16:31), karibu sana na mji wa Tarshishi, ule ambao Nabii Yona alienda kuhubiri, na alikuwa ni binti wa kifalme, hivyo alitokea katika familia tajiri. Mwanamke huyu hakuwa Mwisraeli, ila aliolewa na Mfalme ..
LANGO LI WAZI Mtunzi wa tenzi namba 121 aliimba kwa ufunuo wa Roho, akisema.. 1. Liko lango moja wazi, Ni lango la mbinguni; Na wote waingiao Watapata nafasi. Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi. 2. Yesu ndiye lango hili, Hata sasa ni wazi, Kwa wakubwa na wadogo, Tajiri ..
MTUMISHI WANGU AITWAYE CHIPUKIZI Zekaria 3:8 “Sikiliza sasa, Ee Yoshua, kuhani mkuu, wewe na wenzako waketio mbele yako; maana hao ni watu walio ishara; kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi.” Huyu mtumishi aitwaye chipukizi ni nani? Huyu sio mwingine zaidi ya Mwokozi wetu YESU KRISTO, ndiye aliyetabiriwa kutokea kama chipukizi katika shina la ..
TUPO KATIKA ILE SAA YA KUHARIBIWA. Jina la mwokozi wetu YESU KRISTO litukuzwe mpendwa, karibu tujifunze habari za uzima. Kama wewe ni msomi mzuri wa BIBLIA utakuwa unafahamu kuwa kuna saa ya kujaribiwa na kuharibiwa kwa huu ulimwengu. Bwana Yesu alisema mwenyewe.. Ufunuo 3:10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke ..
JILINDENI NA CHACHU YA MAFARISAYO NA MASADUKAYO. Mathayo 16:6 “Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. Chachu ni nini?. Chachu kwa lugha ya sasa ni HAMIRA, na kwa kawaida ukiitazama hamira unaweza ukadhani ni unga Fulani hivi, lakini kiuhalisia ule si unga bali ni mkusanyiko wa wadudu wenye uhai kwa lugha ya ..
ONJENI, MWONE KUWA BWANA YU MWEMA Zaburi 34:8 Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini. Ulishatembelea soko la vyakula, na kukutana na wafanya-biashara wengi, halafu kila mmoja anakuvutia upande wake ununue bidhaa yake. Kwakawaida si rahisi kuchukua maamuzi, kwa hofu ya kuuziwa kitu kusicho bora. Wafanyabiashara wengi hulijua hilo, hivyo wanachokifanya ni ..
UMEFANYA HIVYO KWA KUTOKUJUA Jina la Bwana na Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe daima. Karibu katika mafundisho ya biblia, Neno la Mungu wetu lililo Taa na Mwanga wa Njia zetu (Zab.119:105). Katika biblia tunasoma habari ya mtu mmoja aliyeitwa Abimeleki, huyu alikuwa ni mfalme wa nchi iliyojulikana kwa jina la Gerari ambayo ilikuwa inapatikana kule ..
ASILI YA KUJIPAMBA KWA WANAWAKE Asili ya mapambo kwa wanawake ni kutoka kwa MAMA WA MAKAHABA, ndiye alionekana akiwa amejipamba kwa dhahabu na lulu, sasa huyu mama wa makahaba ni nani? Turejee.. Ufunuo wa Yohana 17:1 “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule ..