LIPO LA KUJIFUNZA KWA WALE WAZALISHA WA KIEBRANIA

Uncategorized No Comments

LIPO LA KUJIFUNZA KWA WALE WAZALISHA WA KIEBRANIA

Masomo maalumu kwa waajiriwa/wafanyakazi

Nakusalimu kwa jina la Yesu Kristo Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana. Karibu tujifunze maneno yake ya uzima.

Ikiwa wewe ni mfanyakazi/mwajiriwa, basi leo utajifunza kitu kwa habari hii tunayoenda kuisoma ambayo inahusu wale wazalisha wa Kiebrania..na jambo hili ukilitendea kazi katika kazi yako mahali unapofanyia kazi/ulikoajiriwa basi utapata faida sana.

Hebu tusome kwanza hiyo habari tuone jambo lenyewe la kujifunza (Zingatia maneno yaliyoainishwa kwa harefi kubwa)

Kutoka 1:15 “Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;

16 akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.

17 LAKINI WALE WAZALISHA WALIKUWA WAKIMCHA MUNGU, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.

18 Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai?

19 Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.

20 BASI MUNGU AKAWATENDEA MEMA WALE WAZALISHA; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi.

21 ILIKUWA KWA SABABU WALE WAZALISHA WALIKUWA WAKIMCHA MUNGU, AKAWASIMAMISHIA NYUMBA.

Umeona jambo ambalo Mungu anataka ujifunze kwa hao wazalisha, si lingine zaidi ya KUMCHA MUNGU.

Je! Unataka Mungu akusimamishie kazi yako kama alivyowasimamishia nyumba hao wazalisha wa Kiebrania, basi kuwa mwamnifu kwa Mungu katika ofisi yako, mahali unapofanyia kazi.

Unataka upandishwe mshahara au cheo, kanuni ni kumcha Mungu kama Danieli ambaye alimcha Mungu akakataa rushwa, akakataa dhuluma na mwisho akapendwa na Mungu na hatimaye akawa mtu mkubwa.

Danieli 6:3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.

4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; LAKINI HAWAKUWEZA KUONA SABABU WALA KOSA; KWA MAANA ALIKUWA MWAMINIFU, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.

Vivyo hivyo kwa Yusufu naye alikuwa akimcha Mungu na kumheshimu, akakataa kujitia unajisi kwa mke wa bwana wake, akakubali hata kwenda gerezani kwa kuzingiziwa, ila tunajua hatima yake kwamba Mungu alikuja kumwinuia na kumfanya kuwa waziri mkuu.

Na wewe leo hii ukimcha Mungu na kumheshimu mahali ulipo, ukawa mwaminifu kwa kazi unayofanya hata kama unalipwa kidogo, nataka nikuambie Mungu hatacha kukuinua kama asivyoacha kwa wakina Yusufu, kama alivyowatendea mema wale wazalisha wa Kiebrania..amini kuwa atakutendea tu na wewe.

Lakini leo hii ukishindwa kuwa mwaminifu mahali ulipo, ukawa unapokea rushwa, unazini na wafanyakazi wenzeko, unaiba mali ya bwana wako, tambua kuwa umepishana na baraka za Mungu na mwisho wako itakuwa mbaya sana, kama Yuda aliyemsaliti Bwana kwasababu ya tamaa ya fedha mwisho wa siku akaishia kupasuka matumbo.

Ipo thawabu kwa waajiriwa wanaomcha Mungu na kumheshimu. Hivyo kuanzia leo anza kumheshimu Mungu upate thawabu yako, kama ulikuwa unapokea rushwa kwanzia leo kataa kabisa, na mambo mengine yote mabaya kataa..Sema kwa ujasiri mimi namcha Mungu wangu siwezi kukubaliana na hayo, usiogope kupoteza kazi maana ni Mungu ndiye akupaye.

Ikiwa kazini kwako wanakulazimisha uvae suruali na vimini wewe kama binti uliyeokoka, ukakataa na kusema Imani yangu hainiruhusu bila kuogopa kufukuzwa kazi, basi ujue, upo katika njia ya kupendwa na Mungu kama Danieli na mwisho utasimimishiwa nyumba.

Bwana akubariki sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Je! Umeokoka? Unafahamu kuwa tunaishi ukingoji mwa siku za mwisho?

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *