Namna ya kuvishinda vita vya kifikra.

Biblia kwa kina No Comments

Namna ya kuvishinda vita vya kifikra.

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Vita vikubwa vya Shetani juu ya watoto wa Mungu si uchawi,uganga,nk lakini vita vikubwa Shetani anavyopigana na watoto wa Mungu na kuwadhoofisha kwa namna isiyokuwa ya kawaida na kuona hawafai tena mbele za Mungu basi ni vita vya kifikra/Mawazo/Ufahamu.

Shetani anajua fika hawezi akakudhuru kwa uchawi wala uganga maana maandiko yameweka wazi hilo..

Hesabu 23:23“Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!

Sasa kitu anachokifanya ni kuvuruga ufahamu wako/Fikra zako na kama usipofahamu namna ya kutoka katika kifungo hiki basi Shetani atakutesa kwa muda mrefu sana. Kama usipoamua kutoka hapo au kama usipofahamu mkakati wa adui juu yako.

Kumbuka imani yako Shetani anaiwinda sana na akishafanikiwa tu kukuangusha basi tena.

Sasa Shetani anawashambulia watu katika maeneo mengi tu.

Wakati fulani nazungumza na baadhi ya watu wananiambia changamoto wanazopitia moja kwa moja nikafahamu adui yupo kazini.

Mtu mmoja aliniambia “mtumishi nahisi kama sijaokoka vizuri nahitaji kuokoka vizuri nikamuuliza kwa nini unasema hivyo? Akajibu nahisi sijaokoka kutokana na mambo yanayoendelea katika maisha yangu lakini nampenda sana Yesu Kristo ila mawazo mabaya yananitawala, ninaona kabisa sina Yesu Kristo ndani yangu,  nikamuuliza tena umeokoka? Au uliongozwa sala ya toba? Akajibu ndio lakini nilichomwambia wewe si kwamba hujaokoka la! Umeokoka lakini adui anacheza na fahamu zako tu lifahamu hili.”

Sasa Shetani kitu anachokifanya ni kuweka mawazo mabaya katika ufahamu wako. Na kama usipofahamu na kuyapinga atakutaabisha sana.

Umekaa au ukatafakari jambo fulani mara umaanza kusikia/mawazo yanakuja “hivi unauhakika Yesu Kristo akija utaondoka naye yaani utanyakuliwa? Kwa upande wako urahisi tu ni mawazo lakini ni shetanu yupo kazini”

Unaposema ndio utanyakuliwa ataanza kukuonyesha madhaifu yako mengi sana uko hivi na hivi jana ulidanganya,uliiba,au ulimtamani yule mwanamke nk unafikiri Mungu anaweza kuchukua mtu kama wewe? Haiwezekani wewe hutaenda hata ufanye nini.

Au atakwambia hivi unafikiri kweli umeokoka wewe? Angalia jinsi ulivyo wewe umeokoka wewe? Hujaokoka unafanya kazi bure wala Mungu hakutambui kabisa.

Yote haya yanakuja katika ufahamu wako na utajikuta yanakuvuruga sana..

Ili kufahamu hila za adui lazima ufahamu Shetani anapokuja anakuja kukuhukumu,kukufadhaisha,kukutisha na kukuchanganya mwisho ukate tamaa.

Roho Mtakatifu haji kwa namna hii, Roho Mtakatifu atakurekebisha na kukwambia kabisa “hiki unachokifanya sio hebu kiache mara moja, hii tabia sio sawa geuka, tubu,omba rehema si sawa hiki fanya hivi na hivi”

Sauti ya Roho Mtakatifu hata kupitia fikra inakuja kukuonya na kukurekebisha na sio kukutuhumu,kukutisha,kukufadhaisha na kukukatisha tamaa. Na Roho Mtakatifu sauti yake/katika ufahamu wako atakwambia jambo na utaona kweli natakiwa kubadilika na kupitia hivyo utakuwa na furaha na kuwa motivated kupiga hatua.

Ukisoma Waraka wa Paulo kwa waglatia(soma waraka wote) Adui alikuwa anawataabisha watu wale mpaka wafate matendo ya sheria ndio watakubaliwa na Mungu (ilihali tayari Mungu alishawakubali baada ya kuhubiriwa Paulo juu ya ukombozi walielewa vyema kabisa ndio maana Paulo sehemu nyingine anasema “Kristo aliwekwa wazi machoni penu” kumaanisha walifunuliwa wanaokolewa kwa njia ya imani kupitia Yesu Kristo wakaamini na wakapata wokovu)

Sasa kitu alichokifanya shetani ni kuwachanganya na kuwaambia mmedanganywa hapo Mungu hajawakubali mpaka mtahiriwe kwanza nk hivyo ikawachanganya wakajikuta wanaiacha kweli na kufuata uongo.

Na ndio anachokifanya Shetani hata sasa ni kuhakikisha anacheza na ufahamu wako ili akuvuruge kataa..

Wakati mwingine utakuwa ukiwaombea watu na kabla hata hujaanza kuwaombea utaanza kusikia “una uhakika watapona? Wewe una nguvu gani ya kuponya mtu?” Fikra kama hizi zikianza kuja zikatae moja kwa moja kumbuka wewe una mamlaka ndani yako ya kuponya watu na kutoa pepo.

Wakati mwingine huenda utaombewa juu ya ugonjwa na hata baada ya kuombea Shetani ataanza kukunong’oneza una uhakika huo ugonjwa umeondoka umepona? Huo ugonjwa haujapona bado upo umepoteza Muda tu. Na ukianza kukubali usipokataa kweli Shetani atakushinda(kumbuka asili yako sio kushindwa.)

Lazima ufahamu mbinu za adui ili uweze kumpinga.

Sasa ni kwa namna gani Fikra zako unaweza kuzilinda dhidi ya adui.

1.kupitia kusoma Neno la Mungu. 

Kuwa mtu wa kusoma Neno kila siku hakikisha kuna kitu kinaingia ndani yako. Neno linapoingia ndani yako linakwenda kuleta mabadiliko, kumbuka Neno la Mungu ni hai,lina nguvu.Waebrania 4:12.

 

2.Tafakari.

Wakristo wengi ni wavivu wa kutafakari lakini nataka nikwambie kusoma na kutafakari vinaenda kwa pamoja.

Unapotafakari unaanza kuruhusu ufahamu wako ukubaliane na kile maandiko yanachosema kuwa wewe ni nani katika Kristo una haki gani na mamlaka gani”

Kuna Wakristo bado hawaamini kama wamesamehewa dhambi zao zote,hawaamini Mungu anawawazia mema ndio maana wanapopatwa na shida wanaanza kunung’unika.  Hiyo yote ni kukosa kutafakari.

Unapotafakari ufahamu wako unabadilishwa kutoka katika hali ya kuwa na mashaka au kutokuamini na kukufamya uwe jasiri,  na kupitia kutafakari ufahamu wako utakuwa unaona yote yanawezekana.

Lakini bila hivyo kuna Mengine utaona yanawezekana mengine hayawezekan.

3.Kili

Hili jambo ni Muhimu tamka kwa kinywa chako kwa kukili wewe umekombolewa hakuna linaloshindikana, umepewa mamlaka ndani yako, kili wewe ni Yesu duniani,kili dhambi haina nguvu juu yako,kili Yesu anakupenda,kili wewe ni kiumbe kipya, kili kwa kila maandiko yanayokuonyesha wewe ni nani kimaandiko unapofanya hivyo unalifanya andiko au Neno La Mungu kuwa hai katika maisha yako.

Kubali kila siku wewe ni Yesu duniani.

Watu wengi wanataabika wanapopita katika changamoto wanachukua andiko wanasimama nalo ingali hawajalitafaro lole andiko na kuwa sehemu ya maisha yao na kulielewa kwa undani matokeo yake wanahindwa”

4.Maombi.

Hayo yote bila maombi bado utakuwa hujakamilisha ni kama kazi Bure yote unaposoma Neno, baada ya kutafakari (ufunuo ulioupata) kili vinahitaji maombi. Na maombi sio kutimiza ratiba au kupokea tu kitu maombi ni zaidi ya yapo.

Mtafakari Eliya baada ya kumwambia mfalme hakutakuwa na mvua kwa miaka mitatu na nusu halafu akaondoka Angalia ni nini alikwenda kufanya alikua kutamka kwangu huku kwa imani ni sawa lakini ilimbidi akaombe ili abadilishe mazingira yote.

Hakusema halafu akatoka hapo akaendelea kuwa na mambo yake alikwenda kuomba.

Tafakari tena baada ya kumwambia mfalme kutakuwa na mvua ni kipi alikwenda kufanya? Hakusema hivyo akaendelea na mambo yake alienda kuomba tena kwa bidii.

Maombi sio jambo la kidini au kutimiza ratiba au kuomba kwa muda mrefu lazima ujue maombi ni kubadilisha mfumo nk”

Maombi ni zaidi ya unavyofikiri Mungu akitupa neema tutaangalia tena upana zaidi wa maombi.

Ukiyafata haya yote kwa uaminifu na kutaka Mungu akusaidie basi Utakuwa umeshinda vita vyako na Shetani atakapokuja utamwambia kama Bwana alivyosema “NENDA ZAKO SHETANI

ubarikiwe sana.

Maranatha.

Mawasiliano: 0613079530.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *