Nehushtani ni nani, ufunuo wake ni upi? 2wafalme 18:4

Biblia kwa kina No Comments

Mungu alimpa maagizo Musa atengeneze nyoka wa Shaba, ili kila mtu alieumwa na wale nyoka wa moto akimtazama huyo nyoka apone. Kama maandiko yanavyosena…

Hesabu 21: 8 ‘’Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.

9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi’’.

Lakini Mungu hakuwahi kusema kwamba Wana wa Israeli kuwa muda au mazingira yeyote yale watakapo patwa na magumu au shida basi ndo wamsimamishe nyoka wa shaba wamtazame ili wapone, hakuwahi kusema hivyo, lakini wana wa Israeli walifikiri wakaona kuna SIRI ndani ya Ile, wakawaza kuwa ni lazima kutakuwa na uponyaji Fulani kwenye nyoka wa shaba kama si hivyo Mungu asingemwambia Musa kuifanya, basi ngoja tujiwekee utaratibu wetu, wa kujifanyia ibada, na kumwomba Mungu kupitia ile nayeye Mungu atatujibu maombi yetu.

hivyo wana wa Israeli walichukulia kama kanuni na wakaamini huyo nyoka wa shaba ana uponyaji wakati wote. Wakashindwa kutambua ni kwa wakati fulani tu.

Basi sasa jambo lilikuja kuendelea hivyo kwa muda wa miaka Mungu mbele, mpaka wakalijengea madhabahu kubwa na likawa jambo linalojulikana sana Israeli, watu wakawa wanakwenda kuisujudia ile sanamu ya nyoka wa shaba na kumwomba Mungu wa Israeli kupitia ile awaondole shida zao, na wakaifukizia uvumba..

Lakini wao hawakutambua kuwa hilo ni chukizo kubwa sana kwa Mungu ndilo lililowapelekea hata kukumbana na ghasia yote ile ikiwemo kupelekwa utumwani tena.. ila sasa baada ya miaka mingi sana kupita akaja mfalme mmoja anayeitwa Hezekia huyo ndiye aliyefanikiwa kuliondoa hilo chukizo katika Taifa la Israeli ambalo liliwaghalimu Pakubwa sana wana wa Israeli. Sasa Hezekia mfalme huyu ndie alieliondoa kabisa.

2 WAFALME: 18:1 ‘’Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea, mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia, mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala

.2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na kenda katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Abiya, binti Zekaria.

3 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, mfano wa yote aliyoyafanya Daudi, baba yake.

4 Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ILE NYOKA YA SHABA ALIYOIFANYA MUSA; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake NEHUSHTANI

5 Alimtumaini Bwana, Mungu wa Israeli; hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda, wala katika hao waliomtangulia’’.

Hebu tutafakari kwa makini hapa kuna jambo kubwa sana la kujifunza. Kuna agizo hapo, lilikuwa ni la Mungu mwenyewe lakini sasa linageuka kuwa mwiba na kikwazo kikubwa sana kwa watu…

kwa namna ya kawaida tunaweza tukaona ni kawaida tu na tukafikiri na kusema “hawa watu ni wajinga sana hawana akili waliwezaje kufanya vile?”

ndugu yangu nataka nikuambie kuwa si kwamba hawakuwa na akili la!, ila sisi watu wa kizazi hiki ndio kabisa wengi tumepungukiwa nazo kwa namna gani? Tunaona hapa.

Mungu alimwambia Musa achonge nyoka wa shaba kama ISHARA tu! ya kitu Fulani tu rohoni, hicho ndicho tunakuja kukijnua sisi watu wa agano jipya, kuwa jambo lile Mungu alilipa ruhusa lifanyike vile kumfunua Bwana wetu Yesu Kristo atakapotundikwa msalabani kwamba kila mtu atakayemwamini aokolewe, hilo tuna liona kwa maneno yake mwenyewe.

Yohana 3:14 ‘’Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyohivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye’’.

lakini hakukuwa na jambo lolote la maana katika ile SHABA, uponyaji mwenyewe haukuwa ndani ya shaba ile bali ulitoka kwa Mungu mwenyewe..sasa badala yake watu wakaacha kumuomba Mungu ambaye ndiye mponyaji wao wakaigeukia shaba isiyoweza kusema, wala kuona, wala kuzungumza

Lakini Leo hii tunajua ni kweli kabisa Mungu alimwagiza Elisha achukue CHUMVI na kuiweka katika chemchemi ya maji iliyokuwa inazaa mapooza..Na baadaye maji yale yakawa matamu,.Lakini fahamu kwamba sio chumvi iliyotibu maji bali ni Mungu ndiye aliye ponya vile, lakini ni kwanini sasa leo hii tunaihusisha chumvi na mambo ya ibada ikiwa hatujaongozwa na kuambiwa kuitumia?.Nasi tunasema vile vile kama wana wa Israeli, Mungu kaweka uponyaji wa kiungu ndani ya chumvi.

tunasema kuna nguvu fulani ndani ya chumvi kama sivyo kwanini Mungu alimwagiza Elisha aiweke katika maji?…Tunamtia Mungu wivu pasipo sisi kujijua..

tunafanya vitu sio kwa ufunuo na muongozo wa Roho Mtakatifu bali kwa kufuata kile tunachokiona pasipo hata kumuomba Mungu hii ni mbaya sana sana.

Vile vile tumeyapa MAJI heshima, na kusema maji yana nguvu ya kusafisha mtu na kumponya ndani yake, na kumtakasa, hatumpi kipaumbele Mungu tunayapa maji kipaumbele na heshima, ndugu Huko ni sawa kuiabudu sanamu ya Shaba.

Na hata hivyo na vitu vingine vyote, tunasema UDONGO unabeba uhai, kwahiyo tukiuweka kwenye biashara zetu, utazifufua, huku tukishikilia kile Bwana Yesu alichokifanya alipotengeneza TOPE ardhini na kumpaka Yule kipofu machoni, na macho yake kufumbuka, tunasema kama udongo usingekuwa na uponyaji Fulani Yesu asingeagizwa kutengeneza tope na kumpa kipofu..na kibaya zaidi mno mpaka tumeshavipa majina kama VITENDEA KAZI VYA KIROHO.

Tuna iweka MISALABA katika Ibada zetu. Kama unapenda msalaba wako kwanini usiunig’inize nyumbani kwako kama kumbukumbu lako la Bwana kukufia msalabani, lakini ni kwanini unakwenda kuuinamia,kuisujudia,kuomba kupitia huo, unadhani unampa Mungu utukufu hujui kuwa ni SANAMU hilo umeiweka moyoni mwako.

Na mambo mengine mengi, tunayafanya hatufahamu kuwa ndivyo tunavyomtia Mungu wivu. Washa tochi yako, utoke kwenye Giza zito la kiroho, ikiwa Mungu amekuongoza kutumia mojawapo ya vitu hivyo kama ishara ya kitu Mungu anachokifanya rohoni ni sawa, kama amekuongoza kutumia maji tumia, amekuongoza kutumia mafuta tumia, na uthibitisho wa kuwa umeongozwa na Mungu kufanya hivyo, ni kwamba hakitakuwa cha kujirudia rudia

Elisha halikuwa hatumii chumvi kila tatizo linalokuja mbele yake…Wala sio kila mgonjwa aliyekuja mbele yake alikuwa anamwambia akaoge mto Yordani mara saba. Alikuwa anafanya vile pale alipokuwa anaongozwa tu! Na sisi tunapaswa tuwe hivyo hivyo.

tuwe ni watu wa kuomgozwa na Roho anasema nini na sio

lakini sasa kama tunaibadilisha Imani yetu tokea katika utukufu na nguvu pamoja na uweza wa DAMU YA YESU iliyo na uwezo wa kufua na kutoa kila kitu na kuvipa vitu hivyo visivyo na utukufu uhai pamoja na heshima Fulani ya kiroho kwamba vina nguvu Fulani au uwezo Fulani wa kutenda mambo, basi tufahamu moja kwa moja tunamtendea ibada shetani. Na Mungu apendezwi nazo Sana kwa jinsi ile ile alvyochukizwa na waabudu baali na Jua.

Na matokeo yake ni kwamba, Mungu atatupa mapigo kwa kukosa kwetu maarifa, wakati mwingine badala ya kuta tua tatizo na kulimaliza ndiyo Kwanza lina ongezeka, kwasababu biblia inasema ni heri ungekutana na ghadhabu ya Mungu kuliko WIVU wake, na ibada zote za sanamu zinaleta wivu mbele za Mungu

Wimbo uliobora 8: 6“..wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.”

Huu ni wakati wa kutubu (yaani kugeuka), na kumwabudu yeye katika Roho na Kweli.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele. Amina.

 Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *