Nini tunajifunza kwa Tamari
Tamari ni mwanamke ambaye tunamsoma katika agano la kale, alikuwa ni mkwewe Yuda mwana wa Yakobo.
Mwanzo 38:1 Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.
2 Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake.
3 Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri.
4 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani.
5 Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa.
6 Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari.
Sasa huyu mwanamke (Tamari) baada tu ya kuolewa kabla hata hajapata mtoto, mume wake akafa, na kwasababu desturi ilikuwa mwanamke akifiwa kabla ya kupata mtoto.. ndugu yake marehemu ndiye anachukua jukumu la kumtwaa na kumfanya kama mkewe ili ampatie marahemu jina kupitia huo uzao, kwahiyo baada ya huyo mumuwe Tamari kufa, ndugu yake aliyeitwa Onani akamchukua huyo Tamari aingie kwake ili amzalie mtoto kwa jina la kaka yake aliyekufa.
Sasa alichokifanya huyu Onani kwakuwa alijua mtoto atakayezaliwa hataitwa kwa jina lake, alipoingia kwa huyo mwanamke alimwagia nje ile mbegu na Bwana akamua kwa kitendo hicho kibaya.
Na baada ya huyo naye kufa, aliyezalia katika ile familia alikuwa ni mdogo kwahiyo ilimpasa Tamari amsubirie mpaka akue.. hivyo huyo mwanamke alibaki akiwa mjane kwa kipindi chote hicho akimsubiria huyo kijana akue,
Lakini kadri muda ulipokwenda, yule kijana alikua, huku Tamari akiendelea kusubiri tu kwa muda wote huo akiwa kama mjane, hivyo alipoona hakuna dalili ya kuolewa naye, alichokifanya, alivua nguo zake za ujane, akajivika utaji, akajifunika uso, akaenda kukaa kama kahaba mahali watu wanapopita, lengo lake sio kufanya ukahaba, bali ni kumpata mtoto.
Hebu soma hiyo habari kwa umakini.
Mwanzo 38:6 Yuda kamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari.
7 Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; na BWANA akamwua.
8 Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao.
9 Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao.
10 Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa BWANA, basi akamwua yeye naye.
11 Yuda akamwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata Shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, Asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye.
12 Siku nyingi zikapita, akafa binti Shua, mkewe Yuda. Yuda akafarijika, akaenda kwa watu wake wawakatao manyoya kondoo huko Timna, yeye na mwenzake Hira, Mwadulami.
13 Huyo Tamari akapewa habari, kusema, Mkweo anakwenda Timna, akate manyoya ya kondoo zake.
14 BASI AKAVUA NGUO ZA UJANE WAKE, AKAJIVIKA UTAJI, AKAJIFUNIKA USO, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, wala hakuozwa awe mkewe.
15 YUDA ALIPOMWONA ALIMDHANIA KUWA NI KAHABA, MAANA AMEJIFUNIKA USO.”
Umeona hapo, Yuda alipomwona Tamari ambaye ni mkwewe alimdhania kuwa ni KAHABA na ukiendelea kusoma alimchukua na kwenda kulala naye.
Nini tunajifunza kwa huyu Tamari?
Japo kuna mazuri ya kujifunza kwa huyu mwanamke ila leo hatutazungumizia hayo.
Lakini kuna jambo nataka ujifunze wewe binti/mwanamke unayevaa mavazi yasiyo na heshima, na kutia mwili wako vitu vinavyomchukiza Mungu ambavyo wewe unaona ni urembo.
Nataka nikuambie hayo masuruali unayovaa na unasema haina shida ni nguo tu, hizo gauni na sketi fupi unazovaa na kusema haufanyi uzinzi, ni kweli huwenda ukawa haulali na wanaume, ila nataka nikuambie leo, hata Tamari alivyovaa yale mavazi ya kikahaba, sio kwamba alikuwa ni kahaba ila kwa mavazi yake tu alionekana kama kahaba, na wewe vivyo hivyo.
Unapovaa hizo suruali, na vimini, na nguo zote zinazoonyesha sehemu ya mwili wako ambayo haitakiwi ionekane kama mapaja, kifua, tumbo, mgongo na yale yanayochora makalio yako hayo yote ni mavazi ya kikahaba, na unapovaa hautakuwa tofati na kahaba haijalishi haufanyi ukahaba.
Vilevile unapoweka mekaup kwenye uso na kupaka rangi mdomoni, machoni, n.k ni sawa na kufunika uso kama alivyofanya Tamari.
Kwanini Yuda alimdhania Tamari kuwa ni kahaba, kwasababu alikuwa amejifunika uso.
Mwanzo 38:15 ”Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, MAANA AMEJIFUNIKA USO.”
Dada/Mama acha ukahaba, leo jivue hayo mapambo yote kweye uso wako na hayo mavazi yote ya kikahaba uyachome moto.. maana watu watendao mambo ya jinsi hiyo (ukahaba) hawana sehemu katika ufalme wa Mungu, sehemu yao ni lile ziwa liwakalo moto na kibiriti wasipotubu na kuacha ukahaba (Ufunuo 21:8).
Biblia inasema..wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisriri pamoja na adabu nzuri (1Timotheo2:9), na sio kuvalia mavazi ya nusu uchi na kujipamba kwa mapambo ya kiulimwengu (1Petro3:3)
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.