NUNUA SHAMBA LAKO IWE URITHI KWA WATOTO WAKO NA MAHALI PA KUZIKIA

Biblia kwa kina No Comments

NUNUA SHAMBA LAKO IWE URITHI KWA WATOTO WAKO NA MAHALI PA KUZIKIA.

Je! Unalo shamba la kuzikia?

Mwanzo 23:3 Akaondoka Ibrahimu kutoka mbele ya maiti wake, akasema na wazawa wa Hethi, akinena,

4 Mimi ni mgeni, ninatembea kwenu; nipeni mahali pa kuzikia kwenu, pawe pangu, nimzike maiti wangu atoke mbele yangu.

5 Wazawa wa Hethi wakamjibu Ibrahimu, wakamwambia,

6 Utusikie, Ee bwana, ndiwe mtu mkuu sana kwetu, uzike maiti wako katika kaburi lile utakalochagua katika makaburi yetu. Hapana mtu kwetu atakayekuzuilia kaburi lake, usizike maiti wako.

7 Ibrahimu akaondoka, akainama mbele ya watu wa nchi, mbele ya hao wazawa wa Hethi.

8 Naye akazungumza nao, akisema, Ikiwa nia yenu nimzike maiti wangu atoke mbele yangu, mnisikie, mkaniombee kwa Efroni bin Sohari,

9 ili kwamba anipe pango ya Makpela, iliyo katika mpaka wa shamba lake, na anipe kwa kima kilicho kamili, katikati yenu, IWE MILKI YANGU YA KUZIKIA.

10 Basi Efroni alikuwa akiketi kati ya wazawa wa Hethi. Efroni Mhiti akamjibu Ibrahimu, na wazawa wa Hethi wanasikiliza, hata watu wote waingiao mlango wa mji wake, akisema,

11 Sivyo, bwana wangu, unisikilize. Lile shamba nakupa, na pango iliyomo nakupa; mbele ya wana wa watu wangu nakupa, uzike maiti wako.

12 Ibrahimu akainama mbele ya watu wa nchi.

13 AKAMWAMBIA EFRONI, NA WATU WA NCHI WANASIKILIZA, AKISEMA, TAFADHALI UNISIKILIZE; NITATOA KIMA CHA SHAMBA, NAWE UKIPOKEE KWANGU, NAMI NITAMZIKA HUMO MAITI WANGU.

14 Efroni akamjibu Ibrahimu, akamwambia,

15 Bwana wangu, unisikilize. Sehemu ya nchi, ambayo thamani yake ni shekeli za fedha mia nne, n’nini hii baina yako na yangu? Basi uzike maiti wako.

16 Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu AKAMPIMIA EFRONI ILE FEDHA ALIYOTAJA MASIKIONI MWA WAZAWA WA HETHI, SHEKELI ZA FEDHA MIA NNE ZA NAMNA ILIYOTUMIKA NA WENYE BIASHARA.

17 Basi shamba la Efroni lililokuwa katika Makpela kuelekea Mamre, shamba, na pango iliyokuwamo, na miti yote iliyokuwamo shambani, iliyokuwa katika mipaka yake pande zote, vyote viliyakinishwa

18 kuwa mali yake Ibrahimu, mbele ya wazawa wa Hethi, mbele ya watu wote waingiao katika mlango wa mji wake.

19 Basi baada ya hayo Ibrahimu akamzika Sara mkewe katika pango ya shamba la Makpela kuelekea Mamre, ndiyo Hebroni, katika nchi ya Kanaani.

20 NA LILE SHAMBA, NA PANGO ILIYOMO, ILIYAKINISHWA KUWA MALI YAKE IBRAHIMU NA WAZAWA WA HETHI, KUWA MAHALI PA KUZIKIA.

Kwanini Ibrahimu hakukubali kupewa hilo shamba bure, ingawa wamiliki walikuwa radhi kumpatia bure?

Ni kwasababu Ibrahimu alitaka iwe milki yake kabisa, kama tunavyojua ukishalinunua shamba, linakuwa la kwako daima (linakuwa urithi wako)

Kwahiyo Ibrahimu aliliona hilo, kwamba ni kweli angepata bure ila huenda baadaye likaja kunyanganywa tena, na yeye alitaka liwe la kwake mazima kwa ajili ya maziko ya familia yake na urithi wa watoto wake.

Hivyo njia pekee ni kulinunua, na tunaona baadaye Ibrahimu alipokufa, watoto wake walimzika hapo hapo kwenye hilo shamba.

Mwanzo 25:8 Ibrahimu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.

9 Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni bin Sohari Mhiti, lielekealo Mamre.

10 KATIKA LILE SHAMBA ALILOLINUNUA IBRAHIMU KWA WAZAWA WA HETHI, huko ndiko alikozikwa Ibrahimu na Sara mkewe.

Na familia yote ya Ibrahimu, walizikwa hapo kwenye hilo shamba, Isaka na mkewe Rebeka, Yakobo na Lea wote walizikwa kwenye lile shamba alilolinunua Ibrahimu.

Mwanzo 49:29 Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;

30 katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.

31 Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea;

32 shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi.

Ni nini tunajifunza hapa?

Yapo mengi ya kujifunza, ila leo tujifunze umuhimu wa kuwa na shamba lako mwenyewe, ambalo unaweza ukalitumia kwa ajili ya familia yako ikiwemo KUZIKIA, na shughuli zingine kama kujenga, kulima n.k

Sasa shamba ni nini?

Shamba ni YESU KRISTO mwenyewe, ndiye shamba letu na urithi wetu ambalo Baba alitununulia kwa gharama.

Unapokuwa na Yesu, ni sawa na kuwa na shamba ambayo ni mali ya thamani kubwa (ni kama lulu ya thamani)

Vilevile unakuwa na uhakika wa kuishi, na hata ukifa unazikwa humo(ndani ya Yesu) na unakuwa salama, wewe na watoto wako na vizazi vyako vyote, Haleluya.

Kwahiyo Bwana wetu YESU ndiyo urithi wetu na shamba letu la kuzikia na kujengea n.k

1 Petro 1:3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;

4 TUPATE NA URITHI USIOHARIBIKA, USIO NA UCHAFU, USIONYAUKA, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu.

Je! Unalo hili shamba? Au umeliuza! Kama Esau alivyouza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula tu! (Mwanzo 25:32)

Nabothi aliposhurutishwa na Mfalme auze shamba lake la urithi, alikataa kabisa ijapokuwa angepata fedha nyingi sana kiasi cha kununua mashamba mengine mengi, lakini yeye hakuona fedha na mali nyingine kuwa kitu, alishikilia urithi aliyoachiwa na baba zake.

1 Wafalme 21:1 Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria.

2 Ahabu akasema na Nabothi, akamwambia, Nipe shamba lako la mizabibu nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake.

3 NABOTHI AKAMWAMBIA AHABU, BWANA APISHE MBALI NIKUPE WEWE URITHI WA BABA ZANGU.

Sio kwamba Nabothi alipenda kumdharau mfalme, au hakuwa na shida na mali hapana, lakini alijua kuwa shamba la urithi haliuuzwi, haijalishi ni nani amesimama mbele yake, ni mkuu,au sio mkuu, ni tajiri au sio tajiri, kanuni ni ile ile shamba la urithi haliuzwi… Nabothi alikuwa tayari kufa lakini sio kuachia shamba lile liende nje ya ukoo wake.

Sasa cha kushangaza leo hii utaona watu wengi wanasema wao ni wakristo, wameokoka, lakini wapo tayari kuuza urithi huu kirahisi rahisi tu, mtu yupo tayari kumwacha Kristo kwa ajili ya mali, yupo tayari kumwacha Kristo kwa ajili ya wazazi, au ndugu, yupo tayari kumwacha Kristo kwa ajili ya mwanamke au mwanaume…Yupo tayari kurudi nyuma ki-wokovu kwa ajili ya rafiki zake, kwa ajili ya wafanyakazi wenzake, kwa ajili ya boss wake, kwaajili ya ujana wake, kwaajili ya umaarufu wake…Kirahisi rahisi tu, jambo lolote likijitokeza ambalo anaona kabisa ni kinyume na imani yake yupo tayari kuacha mara moja, akidhani kuwa Imani hiyo akishaichia ipo siku ataipata tena,,Ndugu yangu usidanganyike biblia inatumbia IMANI hii tuliyonayo tunakabidhiwa mara moja tu, hakuna cha mara mbili wala mara tatu..soma…

Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu”.

Na hiyo ndio inatufanya tuwe makini sana kuilinda kwasababu tukishaipoteza kuipata tena ni ngumu..

Ni sawa na mtu anayeliuza shamba, akishaliuza mara moja, basi hatakaa alipate tena milele, linakuwa ni milki halali ya mtu mwingine..Vivyo hivyo na leo hii wewe unayeuuza wokovu wako kirahisi rahisi tu, unarudi nyuma kirahisi rahisi tu, siku Roho Mtakatifu akiondoka kwako basi ndio moja kwa moja hivyo , hakuna toba hapo..

Shamba la urithi haliuzwi!! Na kama hauna hili shamba fanya juu na chini ulinununue.

Na gharama inayohitajika ili ulipate ni wewe kukubali kutubu na kuacha dhambi kabisa, hiyo ndiyo gharama ambayo unapaswa uingie na hiyo inaambatana na kujikana nafsi na kuchukua msalaba wako na kumfuata Yesu ambaye ndiye shamba lenyewe.

Kumbuka, usiponunua shamba hili leo, utakuja kujuta mbeleni, majuto makubwa sana kwani ukifa na kuzikwa nje ya shamba hili (Yesu Kristo) hautakuwa na usalama hata kidogo huko uendako.

Na vilevile leo hii ukiuza hili shamba kwa raha za kitambo tu, hakika utakuja pia kujuta huko mbeleni…kama Esau baadaye alipotaka urithi hakupata tena japokuwa alilia sana, lakini haikusaidia kwasababu huko nyuma tayari aliuza.

Waebrania 12:16 Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.

17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.

Nunua shamba hili (Yesu Kristo) na ulitunze sana!.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *