
TUNATAZAMIA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
2Petro 3:13 “Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”.
Ipo mbingu mpya na nchi mpya ambayo wana wa Mungu wameandaliwa, ni nchi ya raha ya milele.
Isaya 65:17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.
Ufunuo wa Yohana 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
[3]Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
[4]Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
*Katika mbingu mpya na nchi mpya hakuna kupigwa jua wala baridi..kwani mambo hayo hayatakuwamo humo!!.
Ufunuo wa Yohana 21:23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.
[25]Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.
👉Huu ndio mji ambao Ibrahimu alikuwa akiutazamia, hivyo akaishi kama mgeni na mpitaji hapa duniani.
Waebrania 11:9 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
[10] MAANA ALIKUWA AKIUTAZAMIA MJI WENYE MISINGI, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
👉Kumbuka sio kila mtu anayejiita mkristo au mpagani ndiye atakayeingia humo, bali ni wale tu walioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima cha mwana-kondoo.
Ufunuo 21:27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
Je! Jina lako limeandikwa katika kitabu cha uzima?
2 Petro 3:14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
“Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao”. (Waebrania 13:14)
YESU KRISTO ANARUDI MUDA WOWOTE!!
Kama bado hujaokoka kweli kweli…basi leo amua kubadilika na kupokea wokovu wa kweli kwa kumaanisha kutubu dhambi zako na kuziacha, kisha ukabatizwe kwa maji mengi na kwa JINA LA YESU upokee na Roho Mtakatifu uishi maisha ya utakatifu.
Muda tuliobakiwa nao ni mfupi sana.. hukumu imekaribia na mwisho wa mambo yote.
Maran atha (Na uje Bwana Yesu).
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.