Bwana wetu Yesu na asifiwe.
Awali ya yote kabisa, ili kupata maana sahihi ya ndoto yako na kuepuka udanganyifu wa tafsiri za ndoto, unapaswa ujue aidha ndoto yako inadondokea kundi Gani kati ya haya matatu
1. Ndoto zinazotokana na Mungu
2. Ndoto zinazotokana na Shetani
3. Ndoto zinazotokana na Mtu mwenyewe (Shughuli, kazi, mazingira yanayomzunguka n.k)
hili Huchukua sehemu kubwa zaidi (95%). Hivyo Epuka kuhangaikia kutafuta maana zake maana hazibebi Ujumbe wowote. Bali ni kumbukumbu zilizoujaza ufahamu wako kutwa kucha zinarudi katika Ulimwengu wa ndoto.
Tukirudi katika ndoto yetu lengwa, Mtu anaweza kuota anapewa pesa na kazi yake inahusisha sana kupewa au kutoa pesa (mfanyabiashara, benki, m-pesa n.k) hivyo ndoto kama hizi ni za kawaida kwake na haziwi na ujumbe wowote kiroho au kimwili, ni Ufahamu wake ushajijengea mazoea hayo hata katika ndoto.
Lakini ikiwa umeota unapewa pesa katika mazingira au uzito au Amani isiyo ya kawaida , Na ulikuwa Katika Maombi ya kumwomba Mungu jambo fulani, Basi kuna Ujumbe katika ndoto hiyo maana kibiblia pesa inawakilisha “chombo Cha kuleta thawabu”.
Mhubiri 10:19 Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na FEDHA huleta JAWABU la mambo yote.
Hivyo ni ishara kutoka kwa Mungu kuwa Amekupa jawabu lako au Haja yako.
Lakini jawabu linaloongelewa katika biblia si la mambo ya kiroho Bali ni ya mwilini vinahudumiwa kwa fedha kama chakula, nyumba, Biashara n.k
Lakini si kama inavyosemekana kwamba huenda mtu akaja kukupa fedha karibuni, La! Inaweza ikawa au isiwe hivyo, au ikaja kwa muktadha tofauti yaani kupata kibali kazini kwako labda Boss akakulipa vizuri zaidi, mkopo n.k Ambapo ukiangalia utagundua ni vitu ulivyokuwa ukimwomba Mungu, hivyo ametumia ndoto hiyo kuonesha amesikia haja yako.
Majibu ya ndoto hii si kwa Maombi ya vitu vya rohoni kama karama, Roho mtakatifu ama Nguvu za Mungu, badala yake mtu anaweza kupata maono ya Mbinguni, kukutana na malaika ndotoni, kuota anahubiriwa, kusikia sauti ya Mungu n.k
Hivyo Unatakiwa kukaa katika matarajio ya majibu yako huku ukiulinda Utakatifu na Ukamilifu wako.
Ukiota ndoto hii na upo nje ya Yesu, ni ishara mbaya! Aidha upotevu wa pesa zaidi au kupata ili upotee zaidi. Tusome
Mithali 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na KUFANIKIWA kwao wapumbavu KUTAWAANGAMIZA.”
Mpendwa usiache udanganyifu wa fedha na Mali vikuangamize, Mrudie Mungu wako.
Tubu dhambi zako Leo, tafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la YESU KRISTO kama ulikuwa bado, Kisha Mwangalie Mungu wako akitembea na wewe katika njia zako.
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.