Kwa nini tunaomba toba/kutubu ikiwa tumesamehewa?

Maswali ya Biblia No Comments

Kwa nini tunaomba toba/kutubu ikiwa tumesamehewa

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Yapo mafundisho ya kishetani yanayowadanganya Wakristo wengi kwamba “ sio lazima kuomba toba tayari umeshasamehewa dhambi zako kwa nini unaanza kulia tena Mungu nisamehe,Nirehemu yaani unamkumbusha Mungu akusamehe na wakati alishakusamehe nk”

ndugu yangu ikiwa umepatwa na mafundisho ya namna hii jiepushe nayo kabisa. Ni upotoshaji na watu wanaofundisha hayo wamepotoka na kuichukulia kwa juu juu neema ya Mungu hivyo wanaishi kama wanavyotaka yaani si kondoo bali ni mbuzi(wanajichunga wao) lakini sivyo.

Sasa kama Mkristo ni lazima utambue mambo makuu haya mawili. Kuna msamaha wa dhambi, na Kuna toba/kutubu.

Ni mambo mawili ambayo yanaonekana kama yanaweza kuwa sawa lakini yanautofauti mkubwa ndani yake. Na haya ukiyafahamu yatakusaidia kusimama imara katika imani yako.

Msamaha wa dhambi ni nini?
Ni pale tunaposikia injli na kuchomwa mioyo yetu kwa kuifahamu kweli(kazi ya msalaba) na kuchukua hatua ya kugeuka, kwa kuamini Yesu Kristo ndio Mwokozi wa roho zetu. Kupitia damu yake tunahesabiwa haki mbele za Mungu bure.

Na kitendo hiki kinapelekea sisi kufutiwa hukumu/adhabu ya dhambi zetu yaani kwenda katika moto wa milele(yaani kuwa mbali na uso wa Mungu milele) na kufanyika viumbe vipya kuwa na ushirika na Mungu.

Ni kuhesabiwa haki bure kwa njia ya imani yaani hiki ni kitendo cha Mungu mwenyewe kwa mapenzi yake anakuondolea dhambi zako zote.

Toba ni nini? Ni geuko ambalo sio la siku moja au siku mbili bali ni endelevu mpaka tunapoondoka hapa duniani au mpaka Kristo atakaporudi. Tutaona ni kwa namna gani?.

Toba sio maneno tu kwamba mtu anasema Mungu nisamehe, nimekosa,sitarudia tena halafu anaendelea na kitu kile kile ndani yake hashuhudiwi kuacha na kuchukia mtindo fulani mbovu wa maisha,au kitendo fulani ambacho hakimpasi kukifanya kama mtoto wa Mungu”

Toba ni geuko linaloanzia ndani moyoni halafu kile kilichoko moyoni kile kile kinatoka kinywani.

Toba ni bidii maandiko yamesema hivyo maana yake inahusisha pia jitihada zako katika hapo Mungu pia anakusaidia..

Ufunuo 3:19
“Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.”

Anaekemewa hapa na kurudiwa sio mpagani, bali ni mtu ambae tayari yupo katika Kristo ni mtu apendwaye yaani mimi na wewe.

Toba harisi ni msukumo wa Roho Mtakatifu ndani ndani yako sio juhudi zako, ambae anaweka huzuni ya Ki-Mungu ndani yako na kupelekea toba iletayo ushindi juu ya kitu hicho (dhambi)

Mfano Daudi baada ya kuzini na Bethsheba lilikua ni badiliko halisi baada ya Daudi kupokea adhabu hakurudia tena mpaka maisha yake yote hakuwahi kufanya kitendo kama hicho tena.

Toba harisi inakufanya uchukie dhambi na kutokufurahia kukaa katika dhambi.

Hivyo toba inahusisha pia moyo wako wote,sio maneno tu inahusisha hata kufunga pia(hakuna mtu anafunga apate wokovu/Msamaha wa dhambi, lakini toba inaweza ikahitaji kabisa kufunga pia na kuomboleza nk).

Yoeli 2

12 Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;

13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.

Maneno haya wanaambiwa Israeli baada ya kumuacha Mungu/kupotoka kwenda katika njia zisizofaa si kwamba hawakua watu wa Mungu la!

Toba ya Ki-Mungu inakuvuta kumrudia Mungu na unakua na amani ndani yako.

Huzuni ya Ki-Mungu ndio inayokupelekea kuona Mungu kwako ndio kimbilio kwingine hakuna msaada. Itakuonyesha ulichokifanya sio sahihi na sasa geuka toka katika njia hiyo na utaanza kuona ushindi ndani yako, uhuru fulani ndani yako au furaha utaona ndani yako na hiyo inaonyesha ulichokifanya ni cha kweli kabisa kugeuka na kimeufurahisha moyo wa Mungu.

2 Wakorintho 7

10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.

11 Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii kama nini ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.

Lakini huzuni ya kidunia yenyewe inakusukuma kufanya maamuzi mabaya kujiona hufai,unana heli ufe tu hauna maana tena ya kuishi,hasira wivu ukiona namna hii ndani yako ni roho ya adui simama imara tafakari neno la Mungu linasema nini juu yako,  hitaji msaada wa Mungu,

Usione suruhisho ni kujiua kama Yuda Iskariote.

Tunaomba toba kutokana na makosa/tunapojikwaa ndani ya wokovu maana bado tupo katika mwili wenye madhaifu hivyo kuna uwezekano wa kujikwaa/kujitia unajisi basi ni kujitahidi kutubu/kugeuka Kuacha kwa kudhamiria moyoni  na kutamka kwa vinywa vyetu kuhitaji msaada wa Mungu.

Unapoomba toba inaonyesha umetambua  kosa na udhaifu wako mbele za Mungu na haujakamilika asilimia zote na unapotambua udhaifu wako basi neema ya Mungu inatimia katika udhaifu.

Paulo anajisifia udhaifu wake(si kwamba alikua mtenda dhambi la!) Bali alifahamu yeye ni mwanadamu kuna mapungufu yapo hata kama yeye hayaoni lakini mbele za Mungu yapo mapungufu yanaonekana na kukiri anahitaji kukamilishwa na Bwana Yesu.

Unapoomba toba(unafahamu nini maana ya toba) unatambua Mungu ndio pekee anaeweza kukusaidia kwa nguvu zako mwenyewe huwezi na Mungu anataka tumfahamu ili tuwe karibu na yeye na tumfananie.

Ubarikiwe sana.
Maranatha.
@Nuru ya upendo.
Mawasiliano:0613079530.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *