TUJIFUNZE KUJISTIRI KWA MALAIKA WA MUNGU.

Biblia kwa kina No Comments

TUJIFUNZE KUJISTIRI KWA MALAIKA WA MUNGU.

Malaika watakatifu waliopo mbinguni, wanaompa Mungu utukufu usiku na mchana, ni WAALIMU wazuri kukufundisha sisi jinsi ipasavyo kujistiri mbele za Mungu.

Malaika wa watakatifu, (yaani Maserafi na Makerubi) wanaompa Mungu sifa na utukufu mchana na usiku sehemu kubwa ya mbawa walizopewa wanazitumia kujisitiri.. na wanajisitiri kuanzia kichwani mpaka miguuni…wanaposimama mbele za MUNGU KUMPA UTUKUFU..

Isaya 6:1“Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.

2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; KWA MAWILI ALIFUNIKA USO WAKE, NA KWA MAWILI ALIFUNIKA MIGUU YAKE, NA KWA MAWILI ALIRUKA”

Soma tena..

Ezekieli 1:11 Na nyuso zao na mabawa yao yalikuwa yametengana kwa juu; mabawa mawili ya kila mmoja yaliungana, hili na hili, na mawili YALIFUNIKA MIILI YAO.

Ikimaanisha kuwa kabla ya kupeleka sifa mbele za MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi, kigezo cha kwanza ni KUJISITIRI!!. Lakini leo hii watu watasimama mbele za MUNGU kumwabudu na kumsifu, vifua vikiwa wazi, mgongo ukiwa wazi, mapaja yakiwa wazi, mauongo yakiwa wazi..na wanawake vichwa vikiwa wazi..huku wakisema Mungu haangalii mwili anaangalia roho.

Swali la kujiuliza je ni nani amewafundisha hayo????.. kuabudu, na kusifu wakiwa nusu uchi, je wamefundishwa na nani?..na Malaika watakatifu wanaomwimbia Mungu au nani?

Jibu rahisi ni kwamba wamefundishwa na shetani, na wanayempa sifa si MUNGU wa Mbinguni bali ni shetani wa duniani na kuzimu!.

Hivyo wewe dada unayesema umeokoka na huku unatembeza mwili wako uchi, unavaa vimini, masuruali, na nguo za kubana fahamu leo kuwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi ni MTAKATIFU sana..sio wa namna hiyo kama unavyomchukulia.

Malaika hawana dhambi lakini wamejistiri miili yao kuanzia juu mpaka chini.. sisi wenye miili ya dhambi tunapaswaje kujistiri mbele zake!!.

1Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

[10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.

Hebu leo amua kubadilika na kutii Neno la Mungu..acha kusikiliza mafundisho ya mashetani yanayokuhubiria kuwa Mungu haangalii mwili anaangalia moyo.. fahamu kuwa mwili wako ni wa thamani sana mbele za Mungu, ni hekalu lake (1Wakorintho3:16 & 1Wakorintho6:19).

Vaa mavazi ya kujistiri, funika kichwa chako kama biblia inavyoagiza kuwa wanawake na wafunike kichwa wakiwa katika ibada (2Wakorintho11:5)

Usikubali kukosa mbingu kwasababu ya watu au mashetani, litii Neno la Mungu..fuata njia nyembamba.

Hizi ni siku za mwisho.. Unyakuo upo karibu sana.

Maran atha. (Na uje Bwana Yesu)

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Je umempokea Yesu ipasavyo?

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *