
ENYI WANA WA MWANAMKE MCHAWI.
Isaya 57:3 “Lakini ninyi karibuni hapa, enyi wana wa mwanamke mchawi, uzao wa mzinzi na kahaba.
[4]Mnafanya dhihaka yenu juu ya nani? Mmepanua vinywa vyenu, na kutoa ndimi zenu? Je, ninyi si wana wa uasi, uzao wa uongo;
[5]ninyi mnaowasha tamaa zenu kati ya mialoni, chini ya kila mti wenye majani mabichi; ninyi mnaoua watoto mabondeni, chini ya mianya ya majabali?
Je! wewe ni mwana wa yule mwanamke mchawi na kahaba?
Ili tuelewe vizuri huyu mwanamke ni nani, tusome tena katika…
2Wafalme 9:22 Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi?
[23]Yoramu akageuza mikono yake, akakimbia, akamwambia Ahazia, Ni uhaini, Ahazia.
Bila shaka umeelewa huyu mwanamke mchawi ni nani!, na huyu ndiye pia mama wa makahaba machukizo ya nchi (Ufunuo 17:5)

Sasa utafahamuje kuwa wewe ni mzao wa kahaba na mchawi!!. Jibu rahisi ni jinsi unavyoonekana kwa ndani na nje.
Biblia inasema..”Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake”.(Ezekieli 16:44)
Makanisa yote yanayotumia vitu bandia kama visaidizi vya imani (mafuta ya upako, udongo, maji, sabuni, keki, n.k) ni makanisa ya kichawi, kumbuka mwanamke kibiblia anawakilisha kanisa (Ufunuo 19:7). Hivyo hayo makanisa ni makanisa ya kichawi na wanaoabudu humo ni wana wa mwanamke mchawi. (YEZEBELI)
Kanisa linalosujudia sanamu ya Bikira Maria, sanamu ya Bwana Yesu ni kanisa kahaba na wote wanaoabudu humo ni wana wa mwanamke kahaba.
Kanisa linaloruhusu wanawake kutumia mapambo (hereni, vipuli, vikuku, makeups, lipsticks, kucha bandia/kupaka rangi kucha, nywele bandia, kusuka, kupaka wanja, n.k) na mavazi ya kikahaba kama makaptula, magauni ya mipasuo, nguo za kubana na kuonyesha shepu, vimini, suruali aina yoyote kwa mwanamke, nguo za mgongo wazi, kifua wazi, tumbo wazi, na mavazi mengine yanayohubiri uzinzi na ukahaba hilo ni kanisa kahaba na wote wanaoingia humo huku wakijua ukweli ni wana wa mwanamke mzinzi (YEZEBELI). (1Petro 3:3 & 1Timotheo2:9)
Je! Wewe ni mzao upi?
1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
Kama unafanana na ulimwengu..unavaa kiulimwengu, unajipamba kiulimwengu, unanyoa kiulimwengu, Unafanya uzinzi kwa siri, unajichua, unasengenya, unatukana, unafanya uchawi n.k tayari wewe ni mzao wa mwanamke mchawi na kahaba (Yezebeli).
Hivyo, maamuzi ni yako..uamue kuokoka au uendelee na ukahaba na uchawi wa mama yako kisha mkatupwe katika ule moto wa jehanumu.
Ikiwa utahitaji msaada wa kuokoka na kubatizwa basi wasiliana nasi kupitia namba uzionazo chini ya makala hii.
Maran atha (Bwana Yesu anarudi).
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.