
ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI;
2 Timotheo 2:22 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, PAMOJA NA WALE WAMWITAO BWANA KWA MOYO SAFI”.
Ujanani kuna vishawishi vingi,na kuna tamaa nyingi,…sasa hili andiko haliwahusu vijana ambao hawajaokoka, hapana linawahusu vijana wakike na wakiume waliookoka..kwani mtu ambaye hajaokoka hawezi kuzikimbia tamaa za ujanani kwasababu bado anazitumikia na amefungiwanavyo nira (hana nguvu ya kuzishinda).
Hivyo Mtume Paulo alimwandikia Timotheo ambaye alikuwa kijana aliyeokoka kwamba azikimbie tamaa za ujanani, na sio yeye tu bali na vijana wote pia waliookoka wanapaswa kuzikimbia tamaa za ujanani (Kwasababu wana nguvu za kuzikimbia na kuzishinda).
Kumbuka sio kwamba ukishakuwa mtumishi wa Mungu kijana basi ndio hautakutana na vishawishi/tamaa…Utakutana navyo lakini biblia imesemaje? TUZIKIMBIEEE…na sio TUZIOMBEEE…Hakuna maombi yeyote ya kuziepuka tamaa wala kuzishinda!…
Lakini tamaa za ujanani ni zipi? Ni pamoja na uasherati, ulevi, umaarufu, uhuni, starehe, anasa, n.k
Sasa huwezi kuziepuka tamaa hizi kwa kuomba tu, hakuna maombi yoyote ya kuepukana na uasherati na ulevi na uzinzi!!..HAKUNA! wala usidanganywe na mtu yeyote hata anayejiita mtumishi! …suluhisho ni kuzikimbia…maana yake ni kwamba kama ulikuwa unamahusiano au unaona kuna dalili ya kuzama kwenye uasherati na mtu Fulani, unajiepusha naye! Sio unamwomba Mungu akuepushe naye! Ni wewe ndiye unayeanza kujiepusha naye..unakata mazoea naye.…kadhalika kama ni marafiki ndio waliokuwa wanakushawishi kwenda kuzini kwa mazungumzo yao au tabia zao..unajitenga nao…huko ndiko kuzikimbia tamaa….Yusufu alimkimbia mke wa Potifa hakumwombea!.
Picha za uchi na pornografia unazoziangalia kwenye simu ndizo zilizokuwa zinakupeleka kujichua na kufanya uasherati…hakuna maombi yeyote katika maandiko ya kuiondoa hiyo tabia!…Suluhisho ni wewe kuamua kuachana na hiyo tabia…kufuta hizo picha kwenye simu yako na kama bado inakushinda unajikuta unazifungua, badilisha hiyo simu yako ya smart unayoitumia na anza kutumia simu ya tochi!..Hilo tatizo utakuwa umelitatua moja kwa moja/umelikimbia….Biblia inasema kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate, ili usije ukapoteza roho yako yote..
Usisubiri ujana wako uharibiwe na ibilisi, umri ulionao ni wa thamani, kama hutastuka leo, utafika wakati utajuta sana kwanini hukumtumikia Mungu katika ujana wako. Zinduka usingizini.
Bwana akubariki, kijana
Kama hujampa Kristo maisha yako, basi tayari yapo mikononi mwa shetani hata kama utakuwa hujui…Kuwa nje ya Kristo tayari upo kinyume cha Kristo kwasababu hukusanyi pamoja na Kristo, Na hivyo unatapanya..(Mathayo 12:30). Hivyo geuka leo mpe maisha yako, ujana wako unathamani sana katika ufalme wake…Wengi watabadilika kupitia wewe endapo utakubali kumtii Kristo, na siku ile utapewa taji ya Uzima.
Maran atha!.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.