
TAZAMENI NI PENDO LA NAMNA GANI ALILOTUPA BABA, TUITWE WANA WA MUNGU.
1 Yohana 3:1-3 “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
[2]Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.
[3] NA KILA MWENYE MATUMAINI HAYA KATIKA YEYE HUJITAKASA, KAMA YEYE ALIVYO MTAKATIFU.
Kuwa mtoto wa Mungu ni upendo mkubwa sana ambao Mungu alitukirimia, kupitia mwanawe mpendwa Yesu Kristo sisi wote tuliomwamini tunapokea uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”;
Hivyo tunapaswa tuishi kama watoto mbele za Mungu, tumuone Mungu kama Baba, kwani na yeye anatuangalia kama watoto wake na kututunza kama vile baba amtunzavyo mwanawe.
Usiende mbele za Mungu kama kiumbe kingine, nenda kama mtoto, usimwogope, mwambie Baba ninamazungumzo na wewe, Kaa uweponi mwake..zungumza naye anakusikia, mueleze shida zako zote, mwambie mimi niko hivi na hivi, mwambie akusaidie, mwambie mimi nina hasira, nina wivu, nina uchungu, siwezi kusamehe, mwambie nina kasoro katika hiki na kile.. mueleze madhaifu yako yote, mwambie akutengeneze.
Mueleze pia mipango yako, mwambie akushauri, akuongoze, mwambie mapenzi yako yatimizwe kwenye kazi yangu, biashara yangu, elimu yangu, familia yangu n.k mueleze kila kitu…tumia hata masaa kukukaa uweponi mwake. Fanya hivyo kila siku..tengeneza mahusiano naye utaona mabadiliko makubwa sana katika maisha yako, wakati wengine wanasumbuka wewe kila siku mnaonana na Baba, unalala naye, unaamka naye unamsalimia, unamshirikisha mambo yako na yeye anakushirikisha nia yake ..mnakubaliana kwa pamoja, hivyo ndivyo watoto wa Mungu wanapaswa wawe kwa Mungu.
Warumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Je! umefanyika mwana wa Mungu? Kama bado unasubiri nini mpaka sasa?? Acha kuteseka na kusumbuka na dunia..mpokee Yesu leo kwa kumaanisha kabisa ili upokee uwezo wa kufanyika mtoto wa Mungu na uanze kuishi kama mtoto wa Mungu.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.