Jibu: Uvungu wa paja ni sehemu ya juu ya paja penye makutano ya mfupa wa paja na kiuno. Tunaona katika maandiko Yakobo akishindana na malaika usiku kucha na hakutaka kumuacha aondoke bila kumbariki. Malaika alipoona kuwa hamshindi akamtegua uvungu wa paja lake. Tukumbuke kuna tofauti ya kuvunjika na kuteguka, kitu kinachovunjwa kinahitaji matengenezo mapya lakini ..
Author : magdalena kessy
Kamsa ni kelele zinazoashiria moto au vita (kwa kingereza kelele hizo huitwa battle cries) Tusome baadhi ya vifungu, Umeona hapo,ni vitabu vinavyoelezea siku ile kuu ambayo Bwana atakuja,utaona inafananishwa na siku ya kelele za vita ambazo huja ghafla. Wakati ule wana wa Israel waliuzunguka ukuta wa Yeriko kwa siku saba wakipiga kelele (kamsa) kuashiria vita ..
Ikiwa unasoma biblia mara kwa mara utakuwa umekutana na neno hili katika vitabu kadhaa. Shokoa maana yake vibarua, yaani watu waliotekwa na kulazimishwa kufanya kazi kwa nguvu. Mfalme Sulemani aliwachukua watu Shokoa 2Nyakati 2:7-8Vifungu vingine vinavyozungumzia juu ya shokoa ni 1Wafalme 5:13, Yoshua 17:13, Waamuzi 1:28, Waamuzi 1:30 Hivi leo shetani anawachukua watu shokoa, anawateka ..
Hapa Biblia inatuonyesha bidii inamkweza/mpandisha mtu, bidii inayozungumziwa hapa kwenye maandiko imeenda mbali zaidi ya ile bidii ya kufanya kazi kwa kipindi kirefu, lakini ni ile bidii ya kutoa na kutumia ujuzi na ufanisi kwa jambo ulilopewa kulitenda kwa muda, wenye utashi kama huo mara nyingi wanachukua usikivu na kuwateka macho wenye vyeo na wafalme ..
Msemo huu umekuwa ukionekana umeekwa kwenye sehemu mbalimbali ya vifungu vingi vya maandiko, Tuangalie hapa, Kutoka 23:18-19[18]Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi. [19]Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika ..
JIBU: Vyano ni wingi wa neno chano maana yake ni sinia. Katika andiko hilo tunaona mwandishi anasema neno linenwalo wakati wa kufaa ni kama machungwa katika vyano vya fedha akimaanisha ni kama machungwa katika masinia ya fedha. Utajiuluza iweje mwandishi afananishe neno linalofaa na machungwa katika masinia ya fedha? Kuna aina ya machungwa yanayopatikana katika ..
Maana ya Neno mintarafu,lina maanisha “Kuhusiana na” mfano mzuri ukitaka kutamka sentesi inayosema, Sielewi chochote kuhusiana na kurudi kwa Yesu Kristo, unaweza kusema” Sielewi chochote mintarafu kurudi kwa Yesu Kristo, hivyo kiwakilishi cha Mintarafu ni sawa na Neno, Kuhusiana na, Ndani ya biblia takatifu yenye vitabu 66, Neno hili limeonekana mara mbili, kwenye kitabu cha ..
Adhama maana yake ni ‘uzuri wa hali ya juu sana’. Uzuri huu wa hali ya juu upo kwa Bwana Yesu peke yake, hakuna mtu wala kiumbe chochote chenye uzuri wa hali ya juu kama alivyo Bwana Yesu Kuna vifungu kadhaa katika Biblia vinavyozungumzia neno hili, ‘adhama’. Zaburi 104:1[1]Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.Wewe, BWANA, Mungu wangu,Umejifanya ..
Neno KUHUTUBU chanzo chake ni HOTUBA , Hotuba ni maneno yaliyoandaliwa na mtu kwa ajili ya kuyazungumza mbele ya mkutano au kusanyiko la watu. Kitendo cha kutoa hotuba ndicho kinajulikana kama KUHUTUBU. Maneno ya hotuba yanaweza kuwa ya kimaendeleo au ya kimkakati. Kuna tofaut kubwa ya kuhutubu kawaida na kuhutubu kibiblia , watu wa ulimwengu ..
Kuhadaa ni neno lenye maana ya kudanganya au kulaghai, kuhadaa ni kutumia njia ya mkato au isiyo sahihi ili kuweza kufanikisha jambo fulani au kulipata.. Tunaliona neno hili kwenye baadhi ya vifungu.. Mwanzo 31:20[20]Yakobo akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia. Mithali 12:5[5]Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ..