Shalom!, UTII kwa kiingereza Obedience. Ni kufuata amri, ombi, au sheria au uwasilishaji kwa mamlaka ya mtu mwingine. Au mamlaka ya juu zaidi na kuyafuata pasipo kujali ama kuangalia linakubaliana na maamuzi yako ama linakinzana na maamuzi ama mawazo yako. Lakini si kila jambo tunaloambiwa kutii tunafaa kulitii la! Hususani katika mambo yanayokinzana na imani ..
Author : magdalena kessy
“kujazi” katika maandiko linamaana ya “kulipa” linahusu kutoa au kutoa sadaka bila nia ya kuonekana mbele za watu. Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. 3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto ..
Daawa ni madai, shitaka, malalamiko, au hukumu inayoweza kutokea pale mshirika mmoja anapomdhulumu au amekufanyia jambo baya. 1Wakorintho 6:1 “Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu? 2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! ..
JIBU… Embu tusome Yohana 18:28 “Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile praitorio,wasije wakanajisika,bali wapate kuila Pasaka”. Ukumbi wa hukumu ambao ndio Praitoria,ambao unakuwepo ndani ya majumba ya wafalme, wahalifu wenye kesi ambazo zilipaswa ziamuliwe na Mfalme .. au liwaji wa mji, basi walipelekwa ..
Kombeo Ndio hiyo hiyo teo, hi moja ya silaha ya kurusha iliyotumika kipindi cha zamani wakati wa vita.. Kombeo/teo ilitengenezwa kwa Ngozi au Kamba, na jiwe lilikuwa likiwekwa katikati yake na kurushwa kumwelekea adui. Kwa ulimwengu wa sasa Silaha ya manati ndio inayotumika kama mbadala ya teo. Hivi ni vifungu ambavyo utakutana na neno hilo; ..
Jehanamu au Jehanum, ni neno lenye asili ya Kigiriki , limetafsiriwa kutoka kwa lugha ya Kiyahudi, Ge-hinnom, linalomaanisha bonde la mwana wa Hinomu. Eneo hili lipo kusini mwa Yerusalemu lilitumiwa na watu ambao walikuwa hawamchi Bwana,.walitumia eneo hilo kwa kuwatoa watoto wao dhabihu kwa kuwapitisha kwenye moto kwa miungu waliyoipata Kanaani. Jambo hili lilikuwa chukizo ..
JIBU…. Sifa ni kitendo cha kumshuhudia Mungu, au kuyasimulia matendo makuu ambayo ameyafanya au aliyonayo, na sifa huwa inaambata na mguso wa ndani unaomfanya mtu arukeruke, acheze, afurahie, aimbe, ashangalie, apige kilele kwa nguvu, kwa hayo aliyoyaona kwa Mungu wake… Kwamfano tunapoona jinsi, mbingu na nchi, jua na mwezi, na milima na bahari, vilivyoumbwa kwa ..
JIBU… Ufisadi kibiblia ni tofauti na jinsi watu wanavyoitafsiri, kikawaidia ufisadi unatafsirika kama kuhujumu uchumi wa nchi au shirika fulani Lakini kibiblia ufisadi hautafsiriki hivyoUfisadi kibiblia unamweleza mtu mwenye tabia ya uzinzi na uasherati uliozidi kupita kiasi kwa maana nyingine kundi hili linajulikana kama makahaba au Malaya Hivyo unapoona neno hili katika biblia moja kwa ..
JIBU… Shekina au shekhinah /schechinah, Ni neno la kiyahudi linalomaanisha, “kutua” au “kuweka makao” au “makazi” ya uwepo wa Mungu duniani… Basi utukufu wa shekina maana yake ni kujifunua kwa uwepo wa Mungu kwa dhahiri duniani, na kujifunua kwake kunaweza kuchukua mfumo wa vitu mbalimbali vya asili kama vile moto, wingu,moshi,mwanga, kijiti kinachoteketea n.k.,.. Shekina ..
JIBU… Mpango wa Mungu wa kurejesha uhusiano wake na mwanadamu ulianza na taifa moja tu, Israeli ambalo liliundwa na Ibrahimu na Isaka. Jumuiya ya Waisraeli ilikua ni kuwa jeshi kubwa la makabila 12, na watu wa mataifa walikuwa watu wa jamii nyingine. Mungu amekuwa akitembea na Israeli pekee kwa zaidi ya miaka 1,500, bila kushughulika ..