Fahamu siri iliyopo katika Neno la Mungu.
Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Sehemu ya pili 02(Mwisho wa somo hili).
Katika somo lililopita tulijifunza tukaona Neno la Mungu ni nini? Tuliona kuwa Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe, ni uzima,ndio lililoumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Lakini leo tutajifunza kanuni za kufanya Neno la Mungu liwe hai au uone uhalisia wake katika maisha yako. Ukifata kanuni hizi basi amini kabisa litakuwa hai..
1.Kulitafakari Neno.
Hii ni kanuni muhimu sana kutafakari Neno wengi tuna habari nyingi za Biblia kwenye akili zetu tunazijua lakini hatujawahi Kuzitafakari tukapata kitu kilichoko nyuma ya hizo habari. Unapotafakari ndio unapata mlango mpana wa kuwa na uelewa na ujasiri juu ya maandiko.
Watu hawayaamini maandiko mengi kwa sababu hawajawahi kukaa na kuyatafakari.. maandiko yanasema “Mtafufua wafu, mtaweka mikono juu ya wangojwa nao watapata afya(Hasemi mtawaombea anasema mtaweka mikono “simaamishi tusiwaombee lakini inabidi uamini inawezekana hivyo na sio nadharia ni halisi),yote yanawekezekana kwa kila aaminiye, umehesabiwa haki bure nk”
Hivyo maandiko kama haya watu wanayafahamu juu juu tu lakini hajui/haamini kama akiweka mkono wake juu ya mgonjwa atapona. Anashindwa kutambua kuwa kuna nguvu ndani yake inayosababisha uponyaji nk.
Usipotafakari Neno hata kama una mistari yote ya Biblia bado utaendelea kuteseka na kuwa na wasi wasi juu hata ya imani yako unapo kaa chini na kutafakari ndio nguvu ya lile Neno inahuika ndani yako maana kumbuka Neno la Mungu ni hai.
Ili uelewe vyema jaribu kutafakari unapokula chakula kikaenda tumboni halafu kisifanyiwe digestion (kumeng’enywa) nini kinatokea. Kwa sababu chakula unachokula kinaenda Kumeng’enywa na baada ya hapo ndio kinasababisha mwili uwe na nguvu maana hapo kuna wanga,glucose, protein, fati nk vinavyosababisha mwili uwe na nguvu.
Bila hivyo chakula kikiingia tumboni kisifanyiwe hivyo mwili utaendelea kuwani dhaifu daima.
Mungu anamwambia Yoshua ayatafakari.
Yoshua 1:8 “Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.”
Unaona hapo? “upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.”
Anasema ndipo utakapoifanikisha njia yako, na kusitawi sana. Haleluya.
Ndivyo ilivyo unapotafakari Neno linakupa nguvu na ujasiri wa kutembea katika mapenzi ya Mungu. Unapata siri iliyoko ndani ukisema umesamehewa unauelewa msamaha wa Mungu vizuri ikiwa ni uponyaji nk ufahamu wako unapokuwa mkubwa ndio unapozidi kufanana na Mungu maana huwezi ukamfahamu Mungu kwa kina ukabaki kama ulivyo lazima utafanana nae tu.
2.Maombi .
Unapotafakari na kupata ufahamu wa kina zaidi hata maombi yako yatakuwa ya kitofauti sana hutaomba dakika 10 au 20, hutaomba juu juu tu utaomba katika ufahamu mpana zaidi na katika Roho Mtakatifu. Maombi yako yanategemea sana pia ufahamu wako juu ya Kristo.
Maombi ndio yanayotengeneza nguvu pia ya wewe kuendelea Mbele.
3.Soma Neno na Mshirikishe Roho Mtakatifu.
Kusoma ni Muhimu pasipo kumshirikisha Roho Mtakatifu yatabaki maneno tu lakini hutakuwa na ufahamu juu ya neno Roho ndio anaekufunulia maandiko.
4.Fanyia kazi unachojifunza ama ulichokifahamu .
Ni muhimu baada ya Yote fanyia kazi Neno la Mungu utaanza kuona mabadiliko makubwa. Ni wajibu wetu sisi kuingia gharama kulifanyia kazi Neno(maana huwezi kulifanyia kazi neno kama usipolielewa.) Umeshalielewa liingize katika utendaji kazi.
5.Kiri
Jizoeshe kuyakiri maandiko hata unapokuwa mwenyewe kwa kinywa chako. Maandiko yanakwambia wewe ni Mwana wa Mungu kiri kwa kinywa kuwa ndio wewe ni mwana wake. Maandiko yanasema Kristo amekupa mamlaka kiri mamlaka hiyo iko ndani yako na ndivyo ilivyo.
Maandiko yanasema hatukupewa roho ya uoga bali ya nguvu kiri ndio ulivyo kwa kinywa chako mwenyewe katika maombi nk hili jambo lina nguvu sana sana jaribu kulifanya utaona matokeo yake.
Usijisemee moyoni tamka kwa kinywa nenda sehemu upo mwenyewe kiri au hata unapokuwa na watu kiri.
Hivyo kanuni hizi ukizifata kwa uaminifu kabisa amini Neno hilo utaanza kuwashuhudia watu na kuwafundisha na utaimalika imara usisome ukayaacha hivi hivi chukua hatua Mungu yuko na wewe.
Omba maombi haya kwa ufupi.
“Baba yangu wa Mbinguni (Yesu Kristo)Asante kwa kunifundisha siku ya leo kanuni za kulifanya Neno lako liwe na matokeo katika maisha yangu, ninakushukuru kwa upendo wako Baba najua unaniwazia mema, Ninaomba unipe nguvu ya kuyatendea kazi yote haya niliyojifunza siku ya leo. Ninaomba nikiamini ni katika Jina lako Yesu Kristo unipendaye Amina.”
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Mawasiliano 0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.