Na uzima wa milele ndio huu.

Biblia kwa kina No Comments

Na uzima wa milele ndio huu.

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Huwezi kufurahia maisha ya wokovu (kuona furaha ya wokovu usipomfahamu Kristo kwa upana zaidi) utaona wokovu wako ni kawaida tu nk

Ili uweze kupiga hatua kila siku ya kiroho ni lazima ujifunze kuyatafakari maandiko. Unaweza ukawa ni mtu wa kusoma tu kama Wayahudi lakini usiwe mtu wa kutafakari na kumpa Roho Mtakatifu nafasi akufundishe utajikuta hali ya uchanga bado.

Wengi wetu tunafahamu uzima wa milele ni kumuamini Yesu Kristo  ni Bwana na mwokozi  basi, ni kweli kabisa na maandiko yanasema hivyo.

Lakini ukweli ni kwamba sio kuokoka tu peke yake basi, unapookoka kweli utakuwa na uzima wa milele lakini si ule ambao Kristo amekusudia ni Zaidi ya hapo kabisa.(hutakuwa na uhakika vizuri wa wokovu wako kama utaishia hapo tu)

Ndio maana Bwana Yesu anasema maneno haya…

Yohana 17
2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.

3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma

Sasa nataka tutafakari hii mistari kwa kina,
Ukianzia mstari huo wa pili anasema “…. ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele” Ikiwa na maana wote waliomwamini Yesu wanapewa uzima wa milele.

Sasa hebu tutafakari kwa kina mstari wa tatu vizuri..

Yohana 17:3
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”

Sasa anakuja kuelezea huo uzima wa milele ni upi anasema “… na huu ndio UZIMA Wakujue wewe,Mungu wa peker wa kweli, na Yesu Krist uliyemtuma
*
Uzima wa milele halisi ambao mtu ataanza kuufurahia hapa duniani mpaka kule ng’ambo ni kumjua Yesu Kristo. Kumjua Yesu Kristo si tu kusema unamfahamu na umempokea basi.

Ni zaidi ya hapo ndugu yangu inakupasa uanze safari ya kumfahamu zaidi Yesu Kristo.

Anasema “ wakujue wewe..”  si tu maarifa ya kichwani bali ni kufahamu kwa undani kuwa na uhakika na ufahamu wa juu zaidi kuhusu Kristo, uzoefu wa kiroho (spiritual experience) yaani uhusiano wa karibu na Mungu.

Yaani personal experience with Jesus.

Uzima wa milele hauhusiani tu na kuishi milele, bali ni kuingia kwenye uhusiano wa kweli, wa karibu, wa kiroho na Mungu na Yesu Kristo. Ni kumjua Mungu si kwa kusikia tu, bali kwa kumpokea, kumwamini, na kumwelewa kwa undani kupitia maisha ya kiroho .

Ukimuelewa kwa undani Yesu Kristo itakuwa ni rahisi kwa wewe kuishi maisha hapa duniani kama mpitaji utaona una muda mchache wa kukamilisha kazi ulioitiwa na Yesu Kristo kisha undone utaona kabisa hapa upo kwa kitambo kwa sababu ya jambo fulani.

Hutaogopa kupoteza ulivyonavyo kwa sababu umempata yeye alie uzima,yeye ambae ni kweli,ambae ni Nuru ambae kwake kuna kila kitu.

Ndio maana Paulo anasema maneno haya ambayo Mkristo wa kawaida tu ambae hajamfahamu Kristo hawezi kusema..

Wafilipi 3

7 Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.

8 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;

Maneno haya Paulo anayaandika si katika ufahamu wa kawaida lakini ni katika ufahamu wa ndani sana(soma nyaraka za Paulo ma Mitume utaona walikuwa ni watu wa namna gani?)

Sio Mitume walipata upendeleo sana la! Bali waliwekeza Muda wao kutafakari maandiko, kuomba na kuanza kutengeneza mahusiano ya karibu sana na Mungu ndio maana tunaona walikuwa tayari kwa lolote kwa sababu walimuelewa Kristo.

Huwezi ukamuelewa Kristo na ukabaki kama ulivyo haiwezekani”

Kusudi kubwa la Mungu kuja kutuokoa sio kubaki katika hali ya wokovu tu kwamba tumesamehewa dhambi kusudi kubwa la Mungu ni sisi tufahamu sana na tuwe na uhusiano nae wa karibu kiasi kwamba jambo ambalo tunaweza kulifanya likawa katika ufahamu wa Mungu (kama Adamu hata alipopewa kuwapa majina wanayama majina ilikuwa sawa sawa na jinsi Mungu alivyokusudia).

Tengeneza mahusiano ya karibu na Mungu(kwa neema za Mungu tutakapopata neema tutajifunza jinsi ya kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu)

Mungu akubariki sana.

Maranatha.

Mawasiliano 0613079530.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *