
MWE NA HASIRA ILA MSITENDE DHAMBI.
Shalom Mtu wa Mungu, karibu tujifunza Maandiko..Leo kwa Neema za Bwana tutajifunza kwa ufupi juu ya HASIRA YA KIMUNGU…Tusome Mstari ufuatao kabla ya kuendelea ambao utatusaidia kuelewa kiini cha somo letu.
Waefeso 4:26-27 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;
[27]wala msimpe Ibilisi nafasi”.
Hasira inayoruhusiwa hapo si ya kidunia ambayo mwisho wake ni madhara, bali ni hasira ya kiMungu ambayo mwisho wake ni kuleta faida katika ufalme wa Mungu.
Hii inatokea pale unapoona watu wanafanya maasi ndani ya nyumba ya Bwana, wanaleta misahaa, wanafanya mambo yasiyompendeza Mungu kwa makusudi, au wengine unawahubiria njia ya kweli wanakataa wazi wazi, hata Bwana wetu Yesu kuna mahali alishikwa na hasira alipoona watu wanafanya mioyo yao migumu hawataki kuelewa.
Marko 3:5 “Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao,..”
Kwahiyo mwisho wa hasira ya namna hii ni kuombea tu wale watu, au kuwakemea/kuwahubiria neno la kweli. Lakini pamoja na hayo tunapaswa tuwapo katika hii hali tujihadhari sana tusitende dhambi. Ikiwa mtu umemwonya mara ya kwanza na ya pili haonyeki mara ya tatu muache usibishane naye…we muombee tu.
Na halikadhalika pia kuna mazingira unaweza ukakutanavyo ukajikuta uchungu umekuingia, lakini unapaswa kupambana mpaka uchungu na hasira yote itoke ndani yako..jua lisizame, kwasababu ukiendelea kukaa nayo inaanza kuweka mizizi na kadri inavyoendelea…inachipua na hatimaye inakuwa shina, na ikikomaa ni ngumu kuondoa tena inahitaji msaada wa Mungu.
Waebrania 12:14-15 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
[15]mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; SHINA LA UCHUNGU lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
Tusimpe ibilisi nafasi, Kataa uchungu mapema inapoingia ndani yako, tafuta amani na watu, jishushe, hata kama huyo mtu ndiye mwenye makosa we jishushe patananaye kwa amani, omba Roho Mtakatifu akusaidie, Kataa mawazo mengine yanayokufanya umchukie huyo mtu maana hayatoki kwa Mungu, pia usikubali kukaa na jambo moyoni usilolipenda.. ni heri useme wazi wazi kwa hekima.
Bwana akubariki sana, naamini utakuwa umepata kitu…
Ukiwa bado hujampa BWANA YESU Maisha yako, basi jua Upo kwenye hatari kubwa kuliko hata hatari ya kupata ajali yoyote ile…Bwana Yesu ndio Njia, na kweli na Uzima..Mtu hafiki mbinguni bila njia yake yeye..Hivyo nakushauri ufanye maamuzi sahihi leo ya kumkaribisha moyoni mwako..atakusamehe bure pasipo gharama yoyote na atakufanya kuwa kiumbe kipya, kwasababu ndicho anachokitaka kwako..
Hivyo unachopaswa kufanya hapo ulipo, ni kujitenga kwa muda mchache na kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kutozifanya tena…unakusudia kuacha uasherati moja kwa moja, ulevi moja kwa moja, anasa na mambo yote mabaya ya ulimwengu huu…na ukishakusudia kufanya hivyo…Bwana ataona umemaanisha kumfuata kwa moyo..hivyo atakuandalia zawadi ya Roho wake Mtakatifu ambaye atauzika kabisa ule utu wako wa kale ambao ulikuwa unakufanya ushindwe kuishinda dhambi, na atakuvika utu upya ambao katika huo utaweza kuishinda dhambi kiurahisi kabisa..Lakini hilo ni mpaka umekusudia kweli kweli kumfuata yeye.
Hivyo mkaribishe leo, moyoni mwako kabla mlango wa Neema haujafungwa..
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.