TUSIIFUATISHE KAWAIDA YA ULIMWENGU HUU

Biblia kwa kina No Comments

TUSIIFUATISHE KAWAIDA YA ULIMWENGU HUU

Waefeso 2:1-7] “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;

[2]ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata KAWAIDA YA ULIMWENGU HUU, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;

[3]ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.

[4]Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;

[5]hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

[6]Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

[7]ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.

Neno la Mungu hapa linasema zamani kabla hatujaokolewa Kwa neema..kumbe tulikuwa wafu kwasababu ya dhambi zetu!! Maana yake, mfu kumbe siyo tu yule aliyezikwa kaburini hata yule mtu anayeishi katika dhambi ambaye hajaokolewa naye ni mfu, na ndivyo nasi tulivyokuwa, tulikuwa wafu. Lakini kwa upendo wa Mungu tukafufuliwa kupitia kifo chake Yesu Kristo pale Golgotha.

Hivyo kama tumekuwa hai kwa Mungu kwasababu ya neema… basi hatupaswi tena kufuata kawaida za ulimwengu huu, na kutumia neema vibaya.

Huu ulimwengu una kawaida zake, na hivyo sisi kama wateule wa Mungu hatupaswi kufuatisha kawaida zake. Kwa mfano katika ulimwengu kuvaa nguo za utupu ni kawaida, kuzini kabla ya ndoa ni kawaida, kuoa wake zaidi ya mmoja ni kawaida tu, kuchukia asiyekupenda ni kawaida, kusalitiana ni kawaida, kuoneana wivu ni kawaida za ulimwengu huu, kushabikia mipira, kucheza magemu, kubeti, kusikiliza nyimbo za mapenzi, kujichua, kutumia mkorogo, kuwa na ubabe, kusengenyana, kubishana, kutukana, kutoa rushwa, kusema uongo n.k vyote hivyo ni kawaida za ulimwengu huu wala usishangae kuona watu wa kidunia wakiwa hivyo…ni kawaida yao na hawajapokea neema ya Mungu hivyo ni wafu. Lakini sisi kawaida yetu ni kuishi sawa sawa na Neno la Mungu linalotuelekeza katika upendo wa kweli, kuishi kwa amani na watu wote, kuchukia udunia, kusamehana, kuombeana na kuishi maisha yanayompendeza Mungu hiyo ndiyo kawaida yetu, hatuna kawaida ya kuwa wabinafsi, hatuna kawaida ya kubeba uchungu, hatuna kawaida ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi kiholela holela, siyo kawaida yetu kutalakiana kwenye ndoa..hiyo siyo kawaida yetu.

Warumi 12:1-2 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

[2] WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Hivyo ndugu uliyeokoka, kamwe usitake kumpendeza mtu, ukafaraka na Mungu. Mambo mengi ya ulimwengu huu yamefaraka na Mungu..Huo ndio ukweli, Ukiupenda ulimwengu ukasema unampenda na Mungu pia hapo unajidanganya.

1Yohana 2:15-17 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

[16]Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

[17]Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

Chagua leo ni kawaida ipi, unasimama nayo..Je! ile ya mbinguni au ya duniani hii. Kamwe usijaribu kuwa hapo katikati, yaani vuguvugu..una hatari kubwa sana ya kutapikwa..kumchanganya Mungu na udunia, ni hatari kubwa sana.

Bwana akubariki

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *