MAANA SIJUI NIFANYALO!!

Biblia kwa kina No Comments

MAANA SIJUI NIFANYALO!!

Warumi 7:14-25 “Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.

[15]Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.”

Je umewahi kufanya jambo au hata sasa unafanya na hulipendi lakini ni kama unatumikishwa hivi.

Kwa mfano huwenda hutaki kuzini/kujichua lakini kila ukisema sitorudia tena ndio kwanza baada ya muda unaenda kufanya kile kitendo. Sasa kama una hili tatizo leo nitakusaidia na maisha yako yatabadilika ukizifiata hizi kanuni

Kwanza ni vizuri kufahamu kuwa sio wewe nafsi yako inataka ufanye hivyo, lakini ni mwili wako. Na kwanini unashindwa kujitawala..ni kwasababu ya dhambi iliyo ndani yako inakutumikisha. Utauliza mtumishi mbona nimeokoka! Na dhambi inawezaje kunitumikisha? Na kwani dhambi ni nini?

Ndiyo dhambi inamtumikisha mtu na kisha inamlipa kabisa..biblia inasema..

Warumi 6:23 Kwa maana MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Umeona dhambi inalipa mtu mshahara haimtumikishi tu bure, lakini ingekewa ni heri ingelipa uzima lakini mshahara wake ni mauti (ziwa la moto).

Sasa tutandokaje kwenye huu utumwa mbaya wa dhambi? Hakuna njia nyingine isipokuwa ni kumpokea YESU, yaani namaanisha kuokoka.

Sasa ninaposema kuokoka…achana na ile tunayoijua kwamba unakiri makosa yako kisha unaomba rehema na unajiunga kanisani na kuwa mshirika, hiyo kila mtu ameshaokoka kwa namna hiyo. Lakini wokovu ninaouzungumzia hapa, namaanisha wokovu wa kujikana nafsi na kuacha dhambi kabisa kabisa. Labda bado hujanielewa.

Yaani namaanisha kujikana nafsi ni kuacha maisha yote ya kidunia…raha za kidunia, starehe, vitu vya kidunia kama miziki ya kidunia, nguo za kidunia (sizostiri mwili), mapambo ya kidunia, muonekano wa kidunia, unafuta picha zote chafu kwenye simu yako, unafuta namba za wazinzi wote, wasengenyaji, na makundi yote mabaya unafuta,hiyo ndio maana ya kutubu na kuokoka. Wakati mwingine ni kama utaonekana kichaa lakini hapo umemaanisha kumfuata YESU, na baada ya hapo unatafuta kanisa la kweli unaenda kubatizwa kwa maji mengi kisha unaanza safari ya kuukulia wokovu kwa kusoma biblia, kuomba na kujifunza makala ya kiroho…huku ukijitenga na marafiki wa kidunia, ndugu zako ni wale wenye njia moja na wewe.

Unaweza ukapitia vita, ndugu wakakuchukia, ukaitwa mjinga, mshamba, mulokole, mbibi kwa kuwa unavaa magauni marefu na umeacha kujipodoa, au unaweza hata ukafukuzwa kazi na bosi, lakini Kristo atakukuwa na wewe kukutia nguvu na kukupa raha pande zote.

Nakuakikishia ukiamua kuokoka kwa namna hii, dhambi yoyote ile iwe ni tamaa ya mwili inakufa ndani yako, utaona tu kuishi bila kufanya hayo mambo ni sawa tu..leo hii unasema haiwezekani, inawezakanikaje mtu kuishi miaka mitano na kuendelea hajawahi kukutana na mwanaume/mwanamke na hajichui. Unasema hivyo kwasababu bado hujaonja nguvu za Roho Mtakatifu, siku ukipokee utakuja kuona kwamba dhambi ilikuwa inakudanganya tu. Nakuambia hivi kwasababu hata na mimi nilikuwa natumikishwa na dhambi lakini baada ya kupokea wokovu wa kweli nikafa kwa habari ya dhambi.

Warumi 8:10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.

Na hii haimaniishi utakuwa umekufa kabisa kwa habari ya tamaa, kwamba hautotamani tena… hapana kutamani utatamani lakini utakuwa na uwezo wa kusitawala tamaa zako, hautapelekeshwa na kutumikishwa, kwamba ukisikia tu kuzini unaenda kuzini hapana haitakuwa hivyo vinginevyo bado hujaokoka.

Je leo upo tayari kuokoka na kuanza maisha mapya ndani ya YESU. Kumbuka mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu. Ni heri dada/, kaka ukampa Yesu maisha yako leo ingalipo bado unayo nafasi, kumbuka hakuna nafasi ya pili kule ng’ ambo na Kristo amekaribia kurudi sana.

Bwana Yesu akubariki sana na akupe neema ya kufanya maamuzi leo.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *