UNAJALI KUHUSU KAZI YA BWANA
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.
Kama watu tuliomwamini Yesu Kristo lazima tuwe ni watu wa kutafakari kila siku katika maisha yetu ni kipi tulichokifanya katika kazi ya Mungu? Je tunajali kazi ya Mungu? Tunaitazama kazi ya Mungu au tuko busy na mambo yetu sisi wenyewe? Tuamkapo asubuhi tunamshukuru Mungu au mpaka tunapojisikia? Kuna jambo hapa natamani tuliangalie lwa ufupi sana kisha litufundishe jambo Fulani katika roho zetu.
Isaya 5:11-12 “ [11]Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!
[12]Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao
Bwana anazungumza kupitia mtumishi wake nabii Isaya kuwaonya wana wa Israeli anasema “ Ole wao waamkao asubuhi na mapema wapate kufata kileo…”
hapa hakuwa anazungumzia kile moja kwa moja yaani pombe, kwa sababu hata katika agano la kaleWana wa Israeli walikua wanaruhusiwa kutumia wine hivyo kileo anataka kufikisha ujumbe kwetu nk.
Kitu alichokua anakisema hapa ni watu ambao wanaamka asubuhi kufanya shughuli zao wenyewe, na kuendelea na mambo yetu yanayotukabili katika siku hiyo lakini hatuna muda wa kumtafakari Mungu hakuna muda wa Kumshukuru Bwana tuko busy nyakati zote na mambo yetu.
Leo hii Wakristo kileo kimekaa ndani yetu sana yaani muda wote tunawaza pesa,kazi,maisha nk
Sasa anasema kwenye mstari wa 12 jambo moja hapa “… lakini hawaiangalii kazi ya Bwana wala kuyafikiri matendo ya mikono yake.”
Unaona hapo anasema “ lakini hawaiangalii kazi ya Bwana….”
Kutokuiangalia kazi ya Bwana maana yake ni kutojishughulisha na kazi ya Mungu moja wapo kwetu sisi ni kutokuwahubiria watu injili ya Kristo kama jinsi tulivyoagizwa Kutenda.
Hili ni jukumu la watu wote tumepewa kulifanya wala sio jukumu la mchungaji au wale wanaitwa Idara ya injili na umisheni hapo kanisani kwenu.
Katika Idara inapaswa kuwa na watu wote kanisa zima basi ni hiyo Idara ya injili na umisheni ndio unapaswa kuwa na watu wote hapo kanisani kwenu lakini wewe umo katika Idara hiyo? Je unaifanya kazi ya Mungu?
Je? Unaumia unapoona watu wako dhambini na unajua watakwenda kuangalia unajali kuhusu hilo? Unaumia kuhusu jambo hilo?.
Je? Unaumia unapoona kazi ya Mungu haiendi mbele? Tunapoona kinahitajika kiasi cha fedha kwa ajili ya kuwapeleka watenda kazi je tunashiriki kikamilifu? Unaona umuhimu wa watu kuokoka nak ama wasipookoka unaona nini kitawapata huku mbele? Una kesh ana kuomba kwa ajili ya kazi ya Mungu? Au wewe unaamka asubuhi na mapema Kwenda kwenye kileo?
Pata muda wa kutafakari mambo haya na uone kama je unashiliki kikamilifu unajali kuhusu ufalme wa Mungu kuongezeka na watu wengi kuokolewa kutoka gizani?
Maombolezo 3:40 “ Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, Na kumrudia Bwana tena.”
Tutafakari mwenendo wetu katika Kristo juu ya kazi yake chunguza njia zako kisha mrejee Bwana kwa kuanza kujishughulisha na ufalme wake.
Tujitoe kuifanya kazi ya Mungu usiangalie una nini ndio uifanye kazi ya Mungu mshukuru Mungu katika hali hiyo hiyo uliyopo mwambie mimi nitasimama kwa ajili ya kuifanya kazi yako.
Ona sababu ya kujishughulisha na kazi ya Mungu katika maisha yako mshukuru Mungu ametenda makubwa sana katika maisha yako mengi huyaoni kwa sababu kwa sababu hatujataka kuwa ni watu wa rohoni kubali kuwa mtu wa rohoni moja ya mambo ambayo yanaweza kukufanya uwe mtu wa rohoni basi ni pale unapotafakari kuhusu kazi ya Bwana hapo utaanza kuona mambo mengi sana na utaanza kuingia kwenye moyo wa Mungu. Fikiri na jali sana kuhusu kazi ya Mungu katika maisha yako.
Bwana Yesu akubariki sana.
@Nuru ya upendo.
Mawasiliano: 0613079530
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.