Hauko hapa duniani kwa bahati mbaya.

Biblia kwa kina No Comments

Hauko hapa duniani kwa bahati mbaya

Shalom nakusalimu katika jina la Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Hakuna mwanadamu anaeishi hapa duniani kwa bahati mbaya yaani kama ajali tu akajikuta yupo la! Kila mmoja duniani hapa haijalishi alipatikana kwa njia gani lakini hayupo kwa bahati mbaya.

Ikiwa umeokoka upo ndani ya Yesu Kristo basi jua kabisa kuwepo kwako hapa duniani na kuokoka kwako hapa duniani basi si kwa bahati mbaya au ilitokea tu la!  tutaangazia zaidi kwa sisi tulio katika Yesu Kristo

Kitu cha kushangaza na kutafakari Mungu anakujua vizuri kabla ya kuanza kuishi kwako hapa duniani. Yaani kabla hujaanza kuishi hapa duniani Mungu alikuwa anakujua tayari na sio kuishia kukujua tu bali tayari kuna kusudi ambalo yeye mwenyewe kwa mapenzi yake anataka ulitimize. 

Yeremia 1:5
“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.”

Maana yake Mungu kabla hujazaliwa,kabla ulimwengu haujaumbwa, yeye alishakufahamu kabla na kuna mahali ulikua unaishi (ulikua unaishi katika wazo na mpango wa Mungu mkamilifu) na kuja kwako hapa duniani ni kwa ajiri ya kutimiliza kusudi lake ndani ya Kristo.

Wakristo wengi wanaishi katika hali ya kukata tamaa na kuona wao ni wanabahati mbaya tu! Na Mungu yuko mbali kiasi kwamba wanaishi kama yatima. Wanaishi kama vile hawana msaada wala tumaini lolote. Wanaona Mungu hayupo pamoja nao wamekata tamaa huenda wametafuta kazi,ndoa nk havijaja kwa wakati basi wanaona fungu lao ni la kukosa ndugu si hivyo Mungu ana mikakati na wewe mikubwa mno katika sehemu yako. Katika Yesu Kristo hakuna bahati mbaya ikiwa utaanza kuishi Ukristo vizuri. Na kujitambua wewe ni nani ndani ya Kristo.

Na hakuna anaeweza kuutimiza ila wewe kila mtu kaumbwa kwa ajili ya kusudi maalumu la Mungu na mimi usipotimiza kusudi hilo siwezi kulitimiza wala mimi nisipotimiza kusudi Langu hakuna mtu anaweza kutumiza(ni sawa na mtu mwingine duniani azaliwe ana alama za vidole/fingerprint kama za kwangu haiwezekani).

Mwanzoni nilikua nafikiri Mungu kuna vitu kaviumba ilimradi tu basi viwepo lakini sivyo Mungu hatengenezi kitu tu basi ilimradi hapana vyote anavyovitengeza vina kazi maalumu.

Wakati fulani nilikua natafakari kuhusu bahari kuhama(Ocean tides) nikawa na tafakari ni kwa nini inatokea hivi kuna nini hasa? Nikaingia mtandao kusoma nikakuta ni nguvu ya mwezi(moon gravity) ndio inayofanya hivyo.

Nikajua ndio kazi ya mwezi huenda lakini nikaendelea kuangalia zaidi kwa undani nini hasa kazi ya mwezi? Na vipi kama mwezi usipokuwepo? Na je vipi kama gravity ya mwezi ikiwa ni ndogo ikaweza kuvuta maji mengi zaidi nini kitatokea? Katika jambo moja nilijikuta na maswali mengi sana. Nikaanza kujifunza kimoja baada ya kingine sitavielezea vyote lakini nilitaka tufahamu kazi kuu ya Mwezi.

1.Mwezi hudhibiti mawimbi ya bahari(tides)

Mwezi huvuta maji mengi ya bahari kwa njia ya mvutano yaani gravity.

Na hii inasaidia kupanda na kushuka kwa maji.

Hii ni Muhimu kwa maisha ya viumbe wa baharini,mzunguko wa hewa ndani ya bahari na hata wakati mwingine duniani.

2.husaidia kuthibiti mzunguko wa dunia.

Unasaidia kuifanya dunia isitetereke sana katika muhimili wake(unaofanya kuwe na usiku na mchana na tunapata majira ya kiangazi nk).

Na pasipo mwezi dunia isingekuwa imara katika mhimiri wake na hii ingeathiri sana hali ya hewa na majira kwa ujumla.

3.hutupa nuru.

Na hii husaidia sana wakati wa usiku(kusingekua na jua hii dunia ingekua giza nene sana, ndio maana siku ya mwisho jua litatiwa giza na mwezi pia dunia yenyewe haina mwanga wa kwake) ku akisi mwang wa jua.

Na hii imekua ikifanya kazi tangu zamani kwa kuwasaidia watu kufahamu majira kwa kutumia kalenda ya mwezi.

Kusingekua na mwezi Bahari zingekosa mzunguko wake wa kawaida.
Hili lingeathiri maisha ya viumbe wengi wa baharini.Hali ya hewa ingekuwa isiyotabirika.

Majira yangekuwa ya mabadiliko makubwa sana  huenda hata yasiwepo kabisa.

Hivyo mambo mengi niliyatafakari ikanipa kufahamu kwa kina hakuna kitu ambacho kipo hapa duniani alichokifanya Mungu kikawa kama pambo tu la!.

Je si zaidi sana mimi na wewe alietuumba kwa sura na mfano wake(haishii hapo tu na anakufa kwa ajiri yangu mimi na wewe? Ikiwa umeokoka usiishi tu kama unaishi basi tambua hujaokoka kwa bahati mbaya au haijatokea tu ukajikuta umeokoka tu. Unapopita katika changamoto fulani kwa ajili ya Kristo usinungu’unike si kwa Bahati mbaya unapitia katika hiyo hali shangilia na furahia juu ya hilo maana hupitii kwa bahati mbaya.

Waefeso 2:10
“Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”

Ukisoma kwenye biblia ya “The passion Translation” inasema kwa wazi zaidi kwamba…

Ephesians 2:10 We have become his poetry, a re-created people that will fulfill the destiny he has given each of us, for we are joined to Jesus, the Anointed One. Even before we were born, God planned in advance our destiny and the good works we would do to fulfill it!

Maana yake..

Waefeso 2:10”Sisi tumekuwa kazi ya mikono yake ya ajabu  watu aliowaumba upya ili kutimiza kusudi alilotuwekea. Kwa kuwa tumeunganishwa na Yesu, Mpakwa Mafuta. Hata kabla hatujazaliwa, Mungu alipanga kwa mapema maisha yetu na matendo mema tunayopaswa kuyatenda ili kutimiza kusudi hilo.”

Unaona hapo? Tumeumbwa upya katika Yesu Kristo baada ya kuokoka tu lipo kusudi ambalo Mungu amelikusudia tulitimize kila mmoja mmoja .

Ikiwa umeokoka tumia muda mwingi kukaa na Mungu ili ufahamu kusudi lako ni nini hasa na kisha uanze kuliishi. Usiwe Mkristo amabe unaishi tu basi wewe hujui kusudi lako ni lipi!. Upo tu kama watu wa kidunia.

Mungu yeye aliekuumba ndio anajua unatakiwa ufanye nini, maelekezo yote na uwezesho wa kutimiza hicho kitu vyote vipo ni wewe kufanya juhudi katika kulijua kusudi.

Kuwa na ufahamu huu, usijione huwezi,wala usiwe mnyonge, Mungu anakusudi na wewe,msaada wa Mungu upo kwa ajili yako,ulinzi wa Mungu unalindwa usiku na mchana na hautakufa bila kutimiza kusudi lako(ukilifahamu hili hutakua na hofu hata ya kufa na wakati utakapolimaliza kusudi lako utajua tu kama Paulo anasema “mwendo ameumaliza salama imani ameilinda” nk na anatazamia taji ya uzima.

Huyu mtu hakusema hivi ili mradi lakini kwa kujua na hata alipokua anapita kwenye changamoto alijua hawezi kufa kabla mpango wa Mungu haujafika.

Hakuna anaeweza kukuua ukiwa katika mpango wa Mungu kutimiza kusudi lake na habari njema kila alieokoka ana kusudi la kutimiza hapa duniani.

Hivyo usiwe na hofu ya kufa au kushindwa? Kwa nini ushindwe? Katika Kristo tunashinda tu hakuna kushindwa yaweke haya akili na tembea katika njia za Mungu kwa kuimarisha mahusiano yako na Mungu, kuwa karibu sana na Mungu.

Kuwa karibu na Mungu sio muda wote kuomba tu(kuomba ni muhimu na lazima ufanye hivyo muda mwingi) lakini ni zaidi ya hapo, anza kuujenga ufahamu wako unapendwa na Mungu, Mungu yupo pamoja na wewe kila mahali unapoenda,hakuwazii mabaya bali mema. Hawezi kukuacha kamwe jenga ufahamu katika maeneo hayo utaanza kufurahia wokovu wako.

Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Mawasiliano:0613079530.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *