
JE WAJUA KUWA MWILI WAKO NI HEKALU LA MUNGU?
Yohana 2:19 “Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.
[20]Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?
[21] LAKINI YEYE ALINENA HABARI ZA HEKALU LA MWILI WAKE”.
Hapa Bwana Yesu alinena mwili wake kuwa ni hekalu, lakini tusome tena maandiko mengine tuone..
1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
[19]Au hamjui ya kuwa MWILI WENU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe
“Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.(1Wakorintho3:17).
Umeona, mtu akizaliwa tu mara ya pili (akiokoka kweli kweli), mwili wake unakuwa sio mali yake mwenyewe bali ni hekalu la Mungu na Roho Mtakatifu anakaa ndani yake.
Hivyo tutunze sana miili yetu, achana na injili inayokuambia Mungu haangalii mwili anaangalia tu moyo… kwahiyo unaweza ukaweka mwili wako utakavyo, ukavaa utakavyo hata nusu uchi, au ukajipamba utakavyo hata kubadilisha asili yako. Hiyo ni injili iliyobuniwa na lusifa kwa ajili ya kuwapeleka wengi kuzimu hasa wanawake.
Funguka leo na ondoa mapambo yote na rangi zote ulizopaka mwilini mwako maana unaharibu hekalu la Mungu, baki kama Mungu alivyokuumba maana unapendeza na Mungu anakupenda hivyo hivyo..usitake kuwapendeza wanadamu wala usimpe ibilisi nafasi ya kukuharibia mahusiano yako na muumba wako.
YESU ANAKUPENDA NA AMEKARIBIA KURUDI!!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.