NJONI KWANGU, NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KULEMEWA NA MIZIGO.

Biblia kwa kina No Comments

NJONI KWANGU, NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KULEMEWA NA MIZIGO.

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

[29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

[30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Hakuna mwanadamu anaweza kubeba mzigo wa mwingine, husuzani mzigo wa dhambi. Ndiyo dhambi ni mzigo unaomlemea mtu!.

Uchungu ni mzigo, wivu, ugomvi, hasira, chuki, kutokusamehe, kiburi, mawazo mabaya, uasherati, ulevi ni mizigo mizito sana, hazibebeki!! Mtu anayejaribu kubeba kwa namna yoyote ile ataishia shimoni.

Ni heri ulemewe na mzigo wa kuni, au maembe kuliko mzigo wa dhambi, mzigo mwingine unaweza kupata msaada kwa watu, lakini mzigo wa dhambi hakuna wa kumsaidia mwingine, na kwa nje unaweza kuonekana mwepesi kumbe ndani umechoshwa na dhambi na unaelekea kufa.

Lakini habari njema ni kwamba yupo mmoja ambaye alishinda mauti yaani YESU KRISTO WA NAZARETHI, na anasema hapa..

“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.

Hivyo, bila kuchelewa mkimbilie leo huyu YESU wa kweli akapumzishe mizigo yako, kumbuka hapa Bwana Yesu anawaita makundi yote mawili ya watu..

Kundi la kwanza ni watu WANAOSUMBUKA, wanaosumbuka na maisha haya!! Kwamba wale nini kesho, walale wapi, walipeje kodi, kwa ujumla ni watu wenye mashaka na hofu ya kuishi bila kuwa na tegemeo fulani, au kuwa fedha za kutosha.

Kundi la pili ni watu WALIOLEMEWA NA MIZIGO, kumbuka mzigo wa kwanza ambayo Bwana anamaanisha hapo ni mzigo wa dhambi, na maana nyingine ni mizigo ya maisha kama matatizo, magonjwa, umaskini, mateso, dhiki, maumivu, n.k. yote hayo Bwana anampumzisha mtu. Na anasema..

“Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

[30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Hapo hasemi kuwa tukishakwenda kwake ni kupumzishwa tu, basi na baada ya hapo hakuna kitakachoendelea..la! Hakusema hivyo, badala yake alisema “JITIENI NIRA YANGU” na tena anasema” mzigo wangu ni mwepesi “….Kumbe! Na yeye anayo nira!.. maana yake anatutoa kwenye utumwa mmoja na anataka kutuingiza kwenye utumwa mwingin!.. Tofauti ni kwamba nira yake yeye ni laini na pia mzigo wake ni mwepesi…

Lakini pamoja na hayo hasemi kwamba ” yeye atatutia nira yake,baada ya kutufungua hiyo nira ya adui ” badala yake anasema ” JITIENI NIRA YANGU ” huo ni kama “Ushauri” na siyo “amri”. Ingekuwa ni amri angesema ” njooni kwangu nami nitawapa pumziko na kuwatia nira yangu “..hapo ingeweza kuwa amri, lakini mpaka anasema sisi ndiyo tujitie nira yake… huo ni uchaguzi!!.. maana yake ukipenda kuwa huru sawa, au ukipenda kuichukua NIRA mpya ya YESU KRISTO ni vizuri zaidi.

Je leo upo tayari kuja kwa Yesu akupe pumziko na kisha akuweke katika nafasi nzuri ya kumtumikia yeye. Au utakuwa radhi kuendelea kulemewa na dhambi na kusumbuka na dunia kisha ukatupwe jehanamu ya moto? Maamuzi yapo juu yako!!

Ikiwa utahitaji msaada wa kumpokea YESU bure, basi wasiliana nasi kupitia namba uzionazo chini ya makala hii.

Maran atha (Bwana Yesu anarudi)

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *