
MSIMZIMISHE ROHO
1 Wathesalonike 5:19 Msimzimishe Roho;
Kumzimisha Roho ni kuzuia utendaji kazi wake ndani yako. Roho Mtakatifu anashirikiana na sisi kutimiza wajibu wetu kwa Mungu na hata kwa wanadamu.
Kwa mfano moja ya wajibu tuliyonayo kwa Mungu ni kumfanyia ibada katika Roho (kuomba, kusifu, kusoma Neno lake, n.k), Sasa Roho Mtakatifu anapokusukuma uingie kwenye maombi halafu unatoa udhuru hapo unamzimisha na unamhuzunisha, au upo kwenye maombi Roho Mtakatifu anakusukuma uendelee kuomba, upase sauti, unene kwa lugha, halafu unakatiza kuomba kwasababu ya kuangalia muda, au watu au sababu nyingine yoyote hapo unamzimisha Roho na nihatari sana kufanya hivyo.
Halikadhalika Roho Mtakatifu anakusukuma uamke kuomba, usome biblia, au umshuhudie mtu fulani, utoe kiasi fulani cha sadaka au umsaidie mtu fulani n.k halafu unakataa kusikiliza huo msukumo wa Roho, Roho Mtakatifu anazima ndani yako na ukiendelea hivyo kwa muda mrefu anaweza akakuacha kabisa.
Na mambo mengine yote hata ya mwilini tunapaswa kutii Roho Mtakatifu na kukubali kuongozwa na yeye.
Waefeso 4:30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
Fahamu pia kumhuzunisha Roho Mtakatifu kwa mtu aliyeokoka ni pamoja na kusikiliza/kutazama vitu vichafu vya ulimwengu huu kama miziki ya kidunia/nyimbo za kipuuzi, vichekesho visivyo na maana, filamu sisizo na faida katika roho yako, picha za uchi, hadithi za kizee, makala ya zinaa, n.k hivyo vyote mkristo hapaswi kufuatilia.. ni mambo ya kimwili na ya kidunia ambavyo vimebeba roho za mapepo.
Biblia inasema..”Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia, maana kila kilichomo duniani yaani tamaa za mwili, tamaa za macho havitoki kwa Mungu”.(1Yohana 2:15).
Roho Mtakatifu hapatani na udunia, unapovaa kidunia na wewe ni mkristo unamhuzunisha, unaponyoa mitindo ya kidunia kama denge na kuchonga pembe za kichwa chako kama wasanii wa kidunia unamhuzunisha Roho Mtakatifu na usipobadilika atakuaacha, unaposuka mtindo wowote, unapopaka makeups katika uso wako na kujipodoa kama kahaba, mdomo wako umepaka marangi kama jini, umetia wanja kama Yezebeli na wewe ni mkristo, unapoweka mapambo aina yoyote kweye mwili wako kwa lengo la kujipamba au kuwapendeza wanadamu fahamu kuwa upo hatarini sana kufa kiroho.
Je! umeokoka ipasavyo? Umepokea muhuri wa Mungu ambao ndio Roho Mtakatifu? Unafahamu kuwa parapanda italia muda wowote na mlango wa neema utafungwa?
Hebu leo, kaa kwa utulivu tafakari hatima ya maisha yako na kisha fanya maamuzi sahihi ya kuokoka kweli kweli kama hujaokoka, kumbuka muda tuliobakiwa nao ni mfupi sana na halikadhalika kifo kipo mbele yetu.
Maran atha.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.