
USIYAREJEE TENA MAFUNDISHO YA KWANZA!!
Wagalatia 4:8 ‘Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.
[9]Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena?
Ikiwa umeokoka kweli kweli na ukajua njia ya kweli hapaswi tena kurudi nyuma na kurejea mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge. Biblia inasema..
2 Petro 2:20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
[21]Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa”.
Usikubali kurejea tabia za kwanza sizizompendeza Mungu (wivu, uchungu, ugomvi, uongo, usengenyaji, uchonganishi, uasherati, ulevi, n.k), usikubali kurejea kuabudu miungu ya wazazi wako, usikubali kurejea tamaa za kidunia, usikubali kurejea kuvaa vimini, nguo za kubana, nguo za kiume/suruali, usirejee kusuka au kupamba kichwa chako na kuondoa utukufu wa Mungu, usirejee kuvaa hereni, usirejee vile vipodozi ulivyoviacha, usirejee kupaka rangi kucha, ni machukizo kwa Mungu, usirejee kusikiliza miziki ya kidunia, usikubali kurejea kutazama picha za ngono/pornography, usirejee kujichua/masterbation, usirejee kucheza magemu, kubeti na kufuatilia filamu zenye maudhui ya kidunia, usikubali kurejea mafundisho manyonge yanayohubiri kuwa siku fulani ndiyo takatifu zaidi ya zingine, usikubali kurejea kuabudu na kutumikia sanamu za mapepo (sanamu za watakatifu waliokufa), usikubali kurejea kuabudu miungu ya Allah, White Hellen, bikira Mariam n.k, usirejee mafundisho yanayohubiri kuwa Mungu hana haja na mwili anaangalia moyo tu, usirejee mafundisho ya mashetani.
Dumu katika Neno la Mungu na kufuata njia kuu (utakatifu).
Maran atha(Bwana anarudi)
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.