JIJARIBUNI WENYEWE.

Uncategorized No Comments

JIJARIBUNI WENYEWE.

2 Wakorintho 13:5 “Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa”.

Wokovu wa kweli sio ule tunaokuona huku nje, au uwapo Kanisani, bali ni pale unapokuwa mwenyewe… kwasababu huku nje tunaweza kukuona uko vizuri, unaonyesha matendo ya utakatifu, unavaa kwa kujistiri vizuri, unahubiri na kukemea dhambi, unaonyesha upendo kwa watu, ni mpole, ni mnyenyekevu. Lakini kumbe wewe mwenyewe unajijua hali yako ukiwa mwenyewe, huwenda ukiwa mwenyewe chumbani unajichua/unajisaga, huwenda ukiwa mwenyewe sirini unatatazama picha za ngono, unasoma makala ya zinaa, kwenye simu yako unajua kilichopo, huwenda usiku wa manane kuna watu unachati nao isivyopaswa, huwenda ukiwa mwenyewe unavuta sigara au unakunywa pombe kidogo. Hivyo biblia inasema JIJARIBUNI WENYEWE KWAMBA MMEKUWA KATIKA IMANI.

Wokovu wa kweli unajithibitisha kwanza mwenyewe kwamba umeokoka kweli kweli kisha huku nje matendo yako yatasema, hauhitaji kuelezea sana.. na hata wakisema uko hivi na vile..haujaokoka, haina haja ya kubishana nao kwani we mwenyewe unajijua jinsi ulivyo…umekwisha kujithibitisha.

1 Petro 3:16 Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.

Jithibitishe mwenyewe, je ukiwa peke yako unawaza nini? unatazama nini kwenye simu yako?unafanya nini? Je unaweza kukumbuka kuomba ukiwa peke yako? au mpaka upigiwe simu na kukumbushwa, je unakumbuka kusoma biblia na kujifunza? au mpaka siku ya ibada ndio unakuja kufungua? Je! wewe mtumishi unakiishi kile unachokifundisha? au unahubiri tu kuwapendeza wanadamu na huku mwenyewe unajua maasi unayoyafanya sirini.

Bwana Yesu amekaribia kurudi.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *