JE UMEFUNDISHWA KUPENDANA?

Biblia kwa kina No Comments

JE UMEFUNDISHWA KUPENDANA?

Neno la Mungu linasema..

1 Wathesalonike 4:9 “Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.

Upendo ni jambo ambalo linahitaji darasa, sio kitu kinachotokea tu mara moja baada ya kuokoka.

Baada ya kuokoka.. Roho Mtakatifu anaanza kukupitisha kwenye hili darasa la upendo, atakuletea wale watu usiowapenda..waje wakukwaze. Ukiona hivyo.. wakati mwingine usikimbilie kuwaona kama maadui walioletwa na shetani. Ni kweli huwenda ni shetani lakini Mungu karuhusu ili akufundishe kupenda.

Hivyo ndugu fahamu tu haya madarasa huwezi kukwepa, na mtu mwenye upendo kwa watu wote ni mtu aliyekomaa kiroho, wala kukomaa kiroho sio kutoa pepo au kufanya miujiza.

Hivyo tuombe Bwana atufundishe kupendana, kumbuka pasipo upendo sisi sio kitu, haijalishi tunamfanyia Mungu nini, haujalishi tumeshinda uasherarati, haijalishi tunajistirii kwa namna gani!!, haijalishi tunafunga na kuomba kila week, haijalishi tunatoa zaka zote, haijalishi tunahubiri kweli yote na watu wanafunguliwa. Kama hatuna upendo sisi ni shaba iliayo na upatu uvumao. Yote mazuri tunayomfanyia Mungu haitufaidii kitu.

Upendo ndio kifungo cha ukamilifu (Wakolosai 3:14)

Bwana Yesu atusaidie.

Je umempokea Yesu??

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *