SAA YA UFUFUO UMEKARIBIA!!

Siku za Mwisho No Comments

SAA YA UFUFUO UMEKARIBIA!!

Yohana 5:25 “Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.

[26]Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.

[27]Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.

[28]Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.

[29]Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.

Kuna siku moja wafu wote waliokufa watafufuliwa, lakini ni vizuri kufahamu kuna ufufuo wa aina mbili, upo ufufuo wa wenye haki ambao utatangulia…huu unahusisha ufufuo wa watakatifu waliolala katika Bwana Yesu watafufuliwa siku ile ya parapanda (siku ya unyakuo), watafufuliwa na miili yao ya asili kisha watavikwa miili miili mingine wataungana na wale watakatifu walio hai kisha watanyakuliwa kwa pamoja kumlaki Bwana Yesu hewani (soma 1Wakorintho15:50- & 1Wathesalonike 4:13-)

Lakini ufufuo wa pili ni ule ambao utahusisha wafu wote waliosalia ..huu ufufuo utahusu wale waliokufa nje ya haki (katika dhambi), watafufuliwa kisha na kuhukumiwa ziwa la moto (soma ufunuo 20:15-).

Kumbuka kwa sasa mtu akifa katika dhambi (nje ya wokovu) moja kwa moja anashuka mahali pa mateso(kuzimu), huko atakaa akingojea siku ile ya ufufuo wa hukumu…huko kuzimu ni kama mahabusu ambao watu wanakaa kwa muda wakingojea siku ya hukumu mahakamani ambao watasomewa mashitaka na kupelekwa jela.

Lakini mtu leo akifa ndani ya YESU (aliye mkristo kweli kweli), anapelekwa mahali pa raha (peponi), huko watakaa kusubiria ile siku ya unyakuo ambao watasikia parapanda na kisha watatoka na kwenda kumlaki Bwana Yesu na moja kwa moja wanapelekwa huko juu sana mbingu za mbingu MUNGU aliko.

Tukiyajua hayo…tutatengeneza maisha yetu leo na YESU kwasababu hamna mtu ajuaye mwisho wake na halikadhalika unyakuo upo karibu sana (Yesu amekaribia kurudi.)

Biblia inasema heri na mtakatifu aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza (ufunuo 20;6)

Bwana Yesu atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *