SISI TU MANUKATO YA KRISTO 

Biblia kwa kina No Comments

SISI TU MANUKATO YA KRISTO 

2 Wakorintho 2:15-16 “Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;

[16]katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo?

Ukiona kuna watu wakikaa na wewe wanakereka, wengine ukikutanao wanaweza hata wakabadilisha njia, wengine walikuwa marafiki zako wa kuifana sana lakini tangu ulipookoka ni kama wamekukinai, hawakutaki tena, au hata ni ndugu zako wa karibu ni kama umekuwa mwiba kwao..ukishaona hivyo ujue wewe ni harufu ya mauti kwao, hivyo usione labda wewe ndio unashida…hapana sisi ni manukato ya Kristo.

Sasa kwa kawaida manukato (marashi) inakuwa na harufu ambayo kwa wengine ni njema lakini kwa wengine ni kikwazo.

Nimewahi kukutana na watu katika kuwapelekea injili, waliponijua..ikawa kila wakiniona wanaondoka mahali walipo, nikajua mimi nimekuwa harufu ile ya mauti kwao, wakati huo huo kuna wengine wakikuona wanafurahi sana…wanakusihii uzidi kukaa nao na kuzungumza nao..hawa nimekuwa harufu ya uzima kwao.

Jiulize na wewe unatoa harufu gani? Harufu yako ndio inatambulisha kuwa umeokoka kweli ipasavyo!, kama ukiona tangu ulipookoka unaishi na kila mtu vizuri, watu wote wanakufurahia, hata wale mlikuwanao katika kundi moja la wahuni, wale mliokuwa mnakutana na kusengenya watu, au ukiona ndugu zako wanakuelewa na hawajaokoka hawana hata mpango wa kuokoka halafu wanakufurahia, fahamu kuwa huwenda bado upo pamoja nao..wote hamjaokoka, labda wewe umeenda tu kujisajili kanisani lakini wao hawajaenda, hapo hamna tofauti. Lakini ukiokoka kweli kweli unageuka kuwa adui kwao, kwasababu gani? Kwasababu wewe ni harufu ya mauti kwa wale wanaopotea, na harufu ya uzima kwa wale wanaookolewa. Hivyo jitathimini leo upo upande gani?

Mkristo wa kweli kweli haeleweki na watu wengi, ni wachache tu watakuelewa waliopewa neema ya Mungu. Hata Bwana wetu Yesu wakati alipokuwa kwa wazazi wake wa kimwili mwanzoni walikuwa wanamuelewa, lakini alipooanza kuhubiri habari njema za ufalme wa Mungu na kufanya miujiza mingi, ndugu zake hawakumuelewa, walitaka kumkamata maana waliona amerukwa na akili, na zaidi wale wakuu wa dini ndio kabisa walichukizwa naye.

Marko 3:21 “Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.”

Bwana atusaidie tuwe manukato yenye harufu nzuri kwake kwa ajili ya wanaookolewa.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *