INJILI ILIYOSTIRIKA

Biblia kwa kina No Comments

INJILI ILIYOSTIRIKA

2Wakorintho 4:3-5 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;

[4]ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

[5]Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.

Katika biblia kuna tofauti kati ya neno “mungu” na Mungu, ukikutana na neno mungu katika biblia ujue linawakilisha shetani, lakini ikianzia na herufi kubwa ujue inawakilisha MUNGU aliye hai. Na halikadhalika kuna yesu na Yesu, yesu wa herufi ndogo ni yesu wa dunia hii ambaye ndio yule yule mungu/shetani, haya ni maarifa ambayo ni vizuri pia kufahamu.

Sasa biblia inasema wapo watu ambao wamepofushwa fikira zao na mungu wa dunia hii, yaani shetani. Watu hawa wamepigwa upofu ili wasione na kujua injili ya kweli ya Kristo. Ndio maana mtu leo akiokoka kweli kweli anaambiwa amepotea au amelogwa.. lakini akiokoka ile ya kidini haambiwi lolote, kwasababu gani? Kwasababu huyo yesu aliyempokea sio yule tunayemjua yaani YESU KRISTO WA NAZARETHI, huyu ndiye anayembadilisha mtu mpaka aonekane amerukwa na akili, lakini yule yesu mwingine wa dunia hii hawezi kumbadilisha mtu na kumfanya atoke katika dhambi… isipokuwa anamfanya mtu awe wa kidunia tu, ndio yule anayehubiriwa na manabii wa uongo, huyu ndiye yule yesu wa mafanikio tu, yesu wa mafuta ya upako, maji ya upako, ni yesu wa mambo ya ulimwengu huu tu..ndiye mungu wa dunia hii ambaye amewapofusha wengi wasiotaka kuamini injili ya kweli, wamewapofushwa fikira zao ili waendelee kuipenda dunia na kudhani wanaye Yesu kumbe wana yesu.

Kwahiyo Neno la Mungu linasema.. ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; hao ambao mungu wa dunia hii amewapofusha fikira.

Kama leo utamhubiria mtu avae mavazi ya kujistiri, aache kuharibu mwili wake kwa kuweka vitu bandia, aache kuharibu kichwa chake kwa kuweka manywele ya bandia au kusuka suka, au kunyoa mitindo ya kidunia, halafu mtu huyu anasema Mungu haangalii mwili anaangalia moyo tu, ujue mtu huyu tayari amepofushwa fikira zake, mwingine anasema kunywa kidogo sio dhambi, kushabikia mipira sio dhambi, mwingine anasema hatumwabudu sanamu ya bikira Maria bali tunaiheshimu tu!, ujue ya kuwa watu hawa wanahitaji msaada mkubwa maana wamepofushwa fikira zao.

Tujiulize je! mimi na wewe tumempokea Yesu yupi? Injili ya namna hii je! Imestirika kwako? Je!inakukwaza?

“Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.”

“Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu FIKIRA ZENU, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

[4]Maana yeye ajaye akihubiri YESU MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea ROHO NYINGINE msiyoipokea, au INJILI NYINGINE msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye! (2Wakorintho11:3-4)

Maran atha (Bwana Yesu anarudi)

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *