
CHAGUA KUPITA KATIKA NJIA YA UZUSHI.
Shalom, karibu tujifunze biblia.
Ni vizuri kufahamu kuwa njia ya kwenda uzimani ni njia isiyo na mwonekano mzuri kwa wengi, ni njia ambayo wengi wanaopotea wanaita njia ya wajinga, njia ya washamba, njia ya kimasikini, njia ya kizamani, njia ya uzushi, hii ni njia isiyotamanika hata kidogo na watu wa ulimwengu huu, lakini ndio njia iendayo uzimani. Ili upite ni lazima ujikane nafsi, ukubali kuitwa mshamba, ukubali kuitwa kila jina baya lakini wewe unajua unaenda wapi.
Matendo ya Mitume 24:14 Ila neno hili naungama kwako ya kwamba kwa NJIA IlE AMBAYO WAIITA UZUSHI, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.
Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; WASIO SAFI HAWATAPITA JUU YAKE; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO.
Je! ndugu unayesoma ujumbe huu, umechagua kupita katika njia ipi? Ni kweli unaweza kuchagua kupita katika njia ile ya wengi isiyo na uzushi, isiyo na dhiki, njia ambayo unajiamuria ujiwekeje, uvae nini! hata ukiamua kuvaa nusu uchi hakuna kuambiwa neno, hata ukiamua kunywa pombe, ukiamua kuzini, ukiamua kujipamba utakavyo hakuna wa kusema na wewe..ni njia ya raha, lakini mwisho wake ni uchungu kama pakanga.
Mathayo 7:13-14 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, NA NJIA NI PANA IENDAYO UPOTEVUNI, NAO NI WENGI WAINGIAO KWA MLANGO HUO.
[14]Bali mlango ni mwembamba, NA NJIA IMESONGA IENDAYO UZIMANI, nao waionao ni wachache.
Ni heri leo ukachagua kutembea katika njia nyembamba iitwayo njia ya uzushi ili uwe miongoni mwa wale wachache waendayo uzimani.
Maran atha (Bwana Yesu anarudi)
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.