AINA MBILI ZA HEKIMA 

Biblia kwa kina No Comments

AINA MBILI ZA HEKIMA 

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana Yesu Kristo, karibu tujifunze maandiko matakatifu. Na leo tutajifunza aina mbili za hekima katika biblia, Neno la Mungu linasema katika..

Yakobo 3:13-18 N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.

[14]Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.

[15] HEKIMA HIYO SIYO IlE ISHUKAYO KUTOKA JUU, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.

[16]Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.

[17] LAKINI HEKIMA ITOKAYO JUU, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.

[18]Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

Hapo ukichunguza kwa makini utajua kuwa kuna aina mbili za hekima zinatajwa hapo, kuna hekima itokayo juu (hekima ya kiMungu), na kuna hekima isiyotoka juu (hekima ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na ya shetani).

Na kila hekima ina matunda yake, kwa mfano hekima isiyotoka juu matunda yake ni wivu, uchungu, ugomvi, fitina, unafiki, uongo n.k kwa ufupi mambo yote mabaya.

14 “Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.

[15] HEKIMA HIYO SIYO Ile ISHUKAYO KUTOKA JUU, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani”.

Lakini hekima itokayo juu matunda yake ni usafi, amani, upole, rehema, kwa ufupi mambo yote mema ambayo yanatajwa pia katika wagalatia 5:22.

Sasa kwa muongozo huo, ni rahisi kubaini aina ya hekima iliyo ndani yetu. Kama tukiwa watu wenye uchungu, ugomvi mioyoni mwetu, fitina, unafiki, uongo, hasira, kiburi, kujisifu, kutokusamehe, chuki, uchafu ni wazi kuwa hatuna hekima ya kiMungu bali tunayo hekima nyingine aidha ya shetani au ya dunia. Au pengine tumepungukiwa hekima ya kiMungu.

Sasa nini cha kufanya??

Kama haujapokea kabisa hekima ya Mungu, unapaswa kupokea hiyo hekima ingie ndani yako na kukubadilisha..

Mithali 2:10 “Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako”;

Kumbuka hekima ya Mungu ni YESU KRISTO mwenyewe ndiyo hekima ya Mungu..

1 Wakorintho 1:30 “Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;

Lakini pia huwenda umempokea Yesu lakini umepungukiwa na hekima yake… hivyo biblia inatufundisha njia ya kuongezewa hekima sio nyingine zaidi ya KUOMBA.

Yakobo 1:5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, NA AOMBE DUA KWA MUNGU, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

Utajuaje kuwa hauna hekima au umepungukiwa, ni kwa kuwa na tabia za hekima ya shetani ambayo matunda yake ni hayo tuliyoyataja hapo juu, ukiona amani, furaha, upole, kusamehe, imepungua ndani yako, huwezi tena kuzungumza na watu vizuri basi hapo unapaswa kumlilia Mungu akuongezee hekima.

Je umeokoka ipasavyo??

Kama hujaokoka, Kristo yupo mlangoni, hizi ni siku za mwisho, na wokovu ndio mwanzo wa hekima..Hivyo mpokee Kristo leo kwa kumwamini na kutubu dhambi zako zote, na kubatizwa. Naye atakukubali, kama alivyosema katika Neno lake.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *