Bwana Yesu na Asifiwe. Karibu tujifunze Maneno ya Uzima.
Tunajifunza nini katika neno hilo ?
Jibu tunalipata
Zaburi 69:8 “Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu”.
Msikwao ni mgeni kutoka nchi nyingine {Stranger in English}.
Mtu kutoka taifa jingine na kwenda taifa jingine lisilo lake ndio anaitwa msikwao.
Hivyo anaposema nimekuwa msikwao kwa Wana wa mama yangu Anamaanisha nimekuwa kama mgeni mbele ya ndugu zangu au Wana wa mama yangu.
Maneno haya aliyaandika Daudi kumhusu, Lakini pia ulikuwa ni UNABII kuhusu YESU KRISTO. Zaburi nyingi za Daudi ziliongelea kuhusu UNABII wa Yesu Kristo mfano zaburi 22
Zaburi 22:1 “Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu?”
Maneno haya Bwana aliyasema pale msalabani (Mathayo 27:46)
UNABII kuhusu yuda..
Zaburi 41:9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.”
Bwana Yesu ananukuu maneno hayo..
Yohana 13:18 “Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake”
Turejee katikaZaburi 69; ambao ulikuwa ukitabiri maisha ya Yesu, kwamba kuna kipindi ataonekana mgeni kutoka mbali mbele ya nduguze kabisa ambao ni Wana wa Israel pamoja na wale ndugu wa damu kama tunavyoona katika Marko 3
Marko 3:21 “Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili”.
Soma pia Yohana 7:5
Hapana shaka kwamba zaburi sura ya 69 ni kuhusu maisha ya Bwana Yesu kwa asilimia zote. Tuangalie mfano mwingine katika sura ya 9
Zaburi 69:8 “Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu.
9 MAANA WIVU WA NYUMBA YAKO UMENILA, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata”.
Maneno hayo “wivu wa Nyumba yako umenila” Panajifunua katika Yohana 2:16-17
Yohana 2:1 “Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.
17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, WIVU WA NYUMBA YAKO UTANILA.”
Tunajifunza Nini?
Sehemu kubwa ya kitabu Cha Zaburi ni UNABII kuhusu maisha ya Bwana Yesu kama ilivyoandikwa katika Luka 24:44
Luka 24:44 “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii NA ZABURI”.
Hivyo Unaposoma zaburi kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu utaona mengi kumhusu YESU.
Lakini yanatuhusu na sisi pia, maana Yesu akiwa ndani yetu basi tunafanana nae, hivyo yanatimia pia katika Maisha yetu.
Angalia, Yesu alionekana msikwao mbele ya ndugu zake pindi anapotimiza mapenzi ya Baba wa Mbinguni, ni dhahiri nasi tutakutana na hayo tutapokuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu, hivyo tukikumbana nayo tusikate tamaa tujitie moyo tukijua kuwa hayana budi kutokea, Yalishatabiriwa
Yohana 16:32 “Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; LAKINI JIPENI MOYO; MIMI NIMEUSHINDA ULIMWENGU”.
KUMBUKA KUSOMA BIBLIA KILA SIKU!
Amen
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.