Maana ya maskini Hutumia maombi bali tajiri Hutumia ukali. Mithali 18:23

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa kristo mfalme.

Maskini Hutumia maombi pale anapohitaji kazi au jambo fulani.japo wapo matajiri wanaojisongeza mbele za bwana na kujishusha pale wanapokumbana na shida na taabu zinazotawala katika maisha yako huweza kujishusha kwa Mungu na muda mwingine kwa wanadamu pia.

Pia wapo matajiri wasioweza kujishusha kwakuwa Wana kiburi, jeuri wakijua ya kuwa pesa ndiyo Kila kitu na hata wengine huwadharau wasionacho wakijua wenye haki ya kutumia pesa ni wao tuu kumbe Mungu anainua vinyonge vilivyo dhaifu kwa wakati wake iljina lake litukuzwe.

Ikiwa unazo pesa na Mali nyingi jinyenyekeze mbele za Bwana huku ukiwasaidia wasiokuwa nacho ili  jina la Mungu litukuzwe.

Ikiwa unazo pesa na Mali nyingi jinyenyekeze mbele za Bwana huku ukiwasaidia wasionacho ili jina la Bwana liinuliwe na hizo Mali zitumike kuujenge ufalme wa Mbinguni na wengi waokolewe na Kristo mwenyewe.

Neno linasema katika mathayo 3;

3]Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Hivyo inatupasa Kila siku tuwe na shauku zaidi ya kumjua Mungu huku tukijua ya kuwa inatupasa tuwe kama watoto wadogo tu tukiutafuta uso wa Bwana.ndipo tutakwezwa na Bwana toka kiwango kwenda kiwango kingine neno linasema ufunuo 7:17_19

17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

[18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

[19]Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu

Hivyo inatupasa kuelekeza nyuso zetu kwa Bwana kwa unyenyekevu mkubwa sana ndipo tutauona mkono wa Bwana kwetu pia tunyenyekeane sisi kwa sisi.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *