KUWA MJINGA KATIKA MAMBO MABAYA!!

Biblia kwa kina No Comments

KUWA MJINGA KATIKA MAMBO MABAYA!!

Warumi 16:19 “Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya”.

Ni heri kuonekana mjinga kwa kukataa mambo mabaya ambayo watu wa kidunia wanaona ni ajabu ya sisi kutoshikamana navyo.

1Petro 4:2-5 “Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.

[3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

[4] MAMBO AMBAYO WAO HUONA KUWA NI AJABU YA NINYI KUTOKWENDA MBIO PAMOJA NAO katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.

[5]Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa”.

Ni heri ukubali kutukanwa na kuitwa mshamba kwasababu umekataa kuvaa vimini, nguo za kubana, na mapambo yote ya nje, ni heri uonekane wa ajabu kwa kujitenga na starehe na anasa za dunia, starehe za dunia ni kama kushabikia michezo yao ambayo imejaa uchafu, kutazama na kusikiliza vitu viovu, kuburudika katika vyakula vya anasa na kulewa, kufanya ngono, kufurahisha mwili katika mambo hayo maovu, vichekesho hivyo na filamu ambavyo ni uchafu wa nafsi, hivyo ndivyo sehemu ya starehe za dunia, na watu wa kidunia wakikuona haushikamani na hivyo wanakuona haupo sawa,

Kwasababu ni kawaida ya dunia hii, kama ni kijana halafu hayupo katika moja ya starehe hizo anaonekana labda anashida, kama ni binti hana rafiki wa kiume/boyfriend anayechati naye na kufanyanaye uasherati anaonekana ni mshamba, kwasababu ni kawaida ya huu ulimwengu.

Lakini ni heri kuwa mjinga katika mambo mabaya kuliko ungejifurahisha katika uchafu wa dunia hii na kuonekana mwerevu na dunia halafu unaishia jehanamu ya moto.

Ni heri wakuite mbibi kwa kukataa fashion za dunia, ni heri wakuite mshamba kwa kukataa urafiki wa dunia, ni heri wakuite mjinga kwa kukataa rushwa, ni heri uitwe hivyo kwa kuchagua utakatifu kwasababu hiyo ndiyo njia ya uzima na wapitao katika njia hiyo ijapokuwa wajinga lakini hawatapotea.

Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo”.

Maran atha (Bwana Yesu anarudi).

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *