
MAMBO YA ROHONI HAYATAMBULIKI KWA JINSI YA MWILINI.
1 Wakorintho 2:14 “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
[15]Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu”.
Mtu wa rohoni sio yule anayeweza kuona vitu vya rohoni kama mapepo, au malaika wa Mungu, sio yule mwenye upako mwingi wa kufanya miujiza mingi, mtu wa rohoni ni yule aliyeokoka kwa kumaanisha na akaenenda katika Roho Mtakatifu, huyo ndiyo mtu wa rohoni ambayo mtu wa mwilini hawezi kumtambua wala kumuelewa, kwasababu mambo ya rohoni hayatambulikani kwa jinsi ya mwili, mambo ya rohoni kwa mtu wa mwilini yanaonekana kama ni upuzi, ujinga, upumbavu!!
Kwa mfano kukusanyika ibadani kila week, kuomba na kufunga mara kwa mara, kutumia muda mwingi na Mungu kutafakari na kujifunza Neno lake, kuhubiri injili, kujitenga na mambo ya kidunia, kwa mtu wa mwilini anaona ni kupoteza muda, ni kama kuna upumbavu ndani yako, unakaa na kumwamini Mungu usiyemuona, tena unamtii kabisa na kusimsikiliza kwa mtu wa mwilini ni kama umerukwa na akili.
Ndio maana mtu akiokoka kweli kweli akaacha mwenendo ule wa kidunia, akaacha kuvaa vimini, na nguo za kubana, akaacha kujipamba, akaacha kusuka, akaacha kufuatilia vitu vya kidunia, akaacha kila kitu cha kidunia watu wa kidunia wanamuona kama amechanganyikiwa au amelogwa…hata Bwana wetu Yesu kuna wakati ndugu zake walimuona amerukwa na akili pale alipooanza kufanya mambo ya rohoni.
Marko 3:21 Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.
Tujiulize je! mimi na wewe tu watu wa rohoni? Je! unaeleweka na watu mwilini?
1 Wakorintho 1:18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu”.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.